Kweli wewe Mbinguni kwetu kwa hiyo Mungu anaguswa na Nyumba za Ibada kutokufungwa.Aisee mnapata wapi hayo maandiko hebu tafuteni kumwabudu Mungu katika Roho na kweli halafu nenda kasome Mambo ya Walawi sura ya 13 na 14 mpaka 15 jinsi ya kudili na magonjwa ya mlipuko badala ya kuja na Mihemko
Mayahudi nao walikua wanajichanganya na mambo ya Dunia kwa kupindisha sheria na kujiona wao wana hekalu la kukutania lakini walilenga fedha na biashara ndani ya hekalu.
Walijua Mungu anakaa ndani ya hekalu lililojengwa na binadamu.
Yesu akawaambia kuwa siku zinakuja ambapo watu watamuabudu Mungu katika Roho na kweli na sio kule Yerusalem wala kwenye mlima .Matokeo yake hata Hekalu lao lilivunjwa kwa sababu ya unafiki wao wa kumkataa Masihi na Mfalme wa Haki Yesu Kristo.
Leo tunaweza kufungua milango ya misikiti na Makanisa lakini bado inatupasa kufanya toba ya kweli na kutenda haki kwa wote.
Kuna siasa za dhulma duniani na hasa miaka hii ya kuanzia 2015 kuendelea mpaka sasa Dunia imekua na viongozi wababe sana waliojiona kuwa Miungu watu. Matokeo yake wote wameufyata mbele ya kirusi cha Corona kisichoonekana kwa macho. Tanzania pia tulikuwa na baadhi ya viongozi wasiojali maumivu ya wengine. Leo nao wameanza kutubu na kujishusha kama binadam.
Ni kweli tunahitaji sana kuomba Mungu na kutubu kweli mana kwa miaka ya hivi karibuni haki ilikua inayumbishwa sana na watawala. Maisha ya watu yalikosa thamani kabisa. Kuna watu walikua wanahamasisha mauaji mpaka Bungeni na kwenye mitandao kwa sababu tu ya tofauti za kisiasa.
Hao watu kwa kweli ni lazima watubu kweli vinginevyo yanayotokea duniani ni stahili ya kizazi hiki kinachoshabikia uovu na viongozi katili wasiojali uhai wa mtu mmoja mmoja.
Hongera sana kwa wale walioona dhambi waliyoifanya kwa Taifa na kuamua kutubu na kujinyenyekeza kwa Mungu.
Waendelee na utakatifu huo huo mpaka October kwenye Uchaguzi wasimamie Uchaguzi huru na wa haki ili tupate viongozi wachaMungu na waadilifu. Huwezi kusema unamuomba Mungu akutendee haki wakati wewe hutendi haki.
Huwezi kumwomba Mungu asimamie maandiko yake wakati wewe hausimamii vyema sheria zinazoongoza eneo lako. Kila mtu atende haki na kumwona mwenzake ni bora kama yeye binafsi. Tusibaguane kisiasa wala Kikabila ndipo tutakapoona umuhimu wa kuacha milango ya nyumba za ibada wazi. Vinginevyo ni kumdhahaki Mungu. Na janga hill la Corona ni LA Dunia nzima ikiwa na maana kuwa ni pigo kama yale ya Wamisri enzi za Farao.
Watawala wa Dunia wamekua waovu sana. Walafi,wazinzi, washirikina, wabinafsi, wenye tamaa, watesaji, wapenda majivuno, wanaopenda kuogopwa na kutukuzwa kuliko Mungu unabidi wajishushe kwa kulazimishwa na kiumbe kidogo kabisa kinachoitwa Corona.
Sent using
Jamii Forums mobile app