Hapana Sina watu wa kuongea na kuhusu hili jambo! ... Ajabu ni kuwa watu wangu wengi wa karibu wananiamini Mimi mtu imara sana.
Wananitegemea kwa ushauri, malusuhishi na maelekezo ya mambo mengi sana ya kiroho! .. kama muda huu nimetoka kuongea na simu karibia 45, na jamaa angu!
Akinipa mrejesho wa semina aliyofanya na mwitikio mkubwa aliopata na kunipa shukurani kwa tips, token na maombi ninayoomba nae kwani yanampa Matokeo!
Na wengine wengi! Ila hakuna mtu anayejua Hali ninayopitia ... Wanaaminigi Mimi mtu imara sana! Pengine ni kwa Sababu ya neema ya Mungu aliyonipa kwa kupenda kucheka na kutabasamu muda wote!
Sina Cha kupoteza! Siwezi kujiua ila ikimpendeza Mungu ni vema tu nikafa!
Kila kitu kwangu kime stack! Jamii forum ndo inanipaga faraja na kucheka!
Hawa jamaa wamekuwa kama ndugu kwangu humu ndani wananijali sana na wananipa moyo wa kusonga mbele
Intelligent businessman Bolotoba Edo kissy na wengine nimewasahau!