Kila nikikutana na wazee/watu wakiniuliza swali "una mchumba?" Najikuta naumia

Kila nikikutana na wazee/watu wakiniuliza swali "una mchumba?" Najikuta naumia

Kosa la mzazi hapo ni nini Abigail?
Mzazi wajibu wake ni kujua maisha yako, hata kuuliza una mchumba ni jambo la kheri
You are over thinking

je kama usingeulizwa ungeona sawa?
Sijasema ana kosa naelewa kauliza kujua mfumo wa Maisha ninavyoenda Kwa ujumla na kama Nina lolote jipya.

Mie nimeelezea hisia nnazopata since napata ugumu kwenye suala la kuwa na mwenza.Hali inayopelekea mie kuumia ndani yangu sijui nijibuje.sio kosa langu lakini Kuna muda najiona kama nafeli.

Shida ipo Kwa mtu Baki kukuuliza hivyo halafu anahoji in deep.
 
Tukiacha tabia ya kusalimiana nusu saa tutapunguza mengi.

Watanzania tunajua kusalimiana sijawahi kuona, half an hr ni salam tu, unategemea maswali gani baada ya salamu.
A - Umeamkaje
B - Salama

A - Unaendeleaje
B - Vizuri

A - Nyumbani hawajambo
B - Hawajambo

A - Mkeo/mumeo
B - Wapo salama

A - Watoto
B - Wapo salama

A - Wazazi nyumbani
B - Wapo salama

A - Habari za tangu jana
B - Salama kabisa

A - Fresh kabisa
B - Fresh

A - Mungu ni mwema
B - Amen

A - Tumeamka salama hata sisi
B - Sawa

A - Watoto walikuwa wanaumwa ila nao wapo poa
B - Safi

A - Mm mwnyw mgongo ulikuwa unauma Ila nimeamka salama
B- N vyema
 
Back
Top Bottom