Kila nikikutana na wazee/watu wakiniuliza swali "una mchumba?" Najikuta naumia

Kila nikikutana na wazee/watu wakiniuliza swali "una mchumba?" Najikuta naumia

Sijui ni mie ama Niko sensitive sana?
Nnapokutana nao katika maongezi nikipigwa Hilo swali najikuta na-blush huku ndani naumia,mchangayiko na aibu na huzuni.Natoa majibu ya hapana bado.wakiendelea najikuta nashindwa hata kujieleza napata kigugumizi.
Shida sio kupata mchumba,shida ni njia zimetofautiana,njia anayopitia mwingine haiwezi kuwa sawa na anayopitia mwingine.Jambo linaweza kuwa rahisi Kwa mwingine lakini upande wa mwingine likawa tofauti.Jamii yetu imeadapt kama ndio njia sahihi impasayo kupitia Kila mtu Kwa wakati fulani,pale utaposhindwa kuipita kwa wakati inageuka maumivu.
Binti uko over 30 huna hata mchumba,huna mtoto wanabaki eeh🙄
Na je ikiwa mtu ataamua Kwa maamuzi yake kubaki hivyo ni kosa?

Kwa upande wa wengine mapungufu yanachangia,ndio tuna mapungufu ya hapa na pale kama changamoto za kiafya,kimwili zinazopelekea kukosa mwenza.Dhahama na magumu utayokuwa unayapitia mwenyewe na Ile hisia unaipata mwenyewe lakini wengine hawawezi kuuhisi huo mzigo unaoupitia,utasikia "jikubali mbona wapo wengi tu wanaingia kwenye ndoa,Wana familia? Wanakushangaa
Shida ni hawajui ni rejection ngapi unapitia,hawahisi mzigo wa maumivu unaobeba.
Hakuna anaependa kukosa kitu,Kila mtu anatamani kukipata on time,lakini kuweka kama utamaduni mtu kuwa na kitu Fulani katika wakati fulani mi naona ni kuumiza hisia na moyo wa mtu Ambae kwake ni ngumu kupata.

Yangu ni hayo Kwa Leo🥹
MUNGU kwa wakati wake atatimiza ahadi zake kwako, kwa kadiri ya mapenzi YAKE.
 
Aah mkuu sio wote wanakuwaga warembo bana, wengine wakikuwa wakajipiga soap soap ndio vijana wanajaa! Lakini umepauka na vaselini lako mweusi tii huoni mtu serious zaidi ya wafunua sketi na usipowagundua unaonjwa sana!

dah pole sana! Lakini mkuu vitu vingine mnalalamika tu bure kuna wengine wanaongea hivi lakini unakuta alikuwa wa kusoma, sasa mkishaanza kudandiana masomoni kwa lengo la kuoana hamjajua hatma zenu si ndio chanzo cha kulaumiana na masingo maza kuongezeka mtaani? Halafu wnegi wenu mkivumiliwa kwenye shida mnakuwaga na dharau kibao mkijipata mnaanza kutafuta mnaoendana nao! Tunaijua hii.. mkipauka mnataka mwanamke fulani, mkishika vihela sasa🙌🏾

Halafu sio kila kukataliwa ndio sababu zake hizo, saingine Mungu anakuepushia mabalaa we unaforce tu unahisi huna pesa ndiomaana hutakiwi hujui huyo mke mngekuwa wapi sasa hivi! Ushukuru tu umepata mke na mtoto sasa, unajuaje kama huyo dem wako angekufaa kuwa mke? Tatizo lenu unataka ukimtongoza mwanamke hata kama hana hisia na ww akukubali ili kesho usije kuleta hizo habari sijui alikukataaga! Mambo ya kawaida hayo mkuu😎
Kwanza alikuwa hasomi maana alikuwa na miwili tupo naye tu mitaani tangu amalize kidato cha 4 na hata alipo ondoka hakuna ondoka kwa ishu ya masomo.
Alafu tatizo sio kukataliwa tatizo ni kumtolea mtu maneno ambayo yanakufanya ujione wa hovyo kabisa ndani ya dunia hii,kwa sababu yeye si mwanamje wa kwanza kunikatalia kwenye suala la utongozaji.
Alafu kama hakuwa na hisia na mm mbona sasa hivi yupo ananisumbua anataka mapenzi na mm au sasa hivi hisia dhidi tangu ndo zimekuja au ni kipi kimebadilika kwake?

Kuhusu yeye kuwa mke mwema kwangu Kuna msemo unasema mungu hakupi ukipendacho bali anakupa unacho sitahili.
 
Haaa ndo zenu nyinyi huwa kipindi mpo kwenye kilele cha uzuri wenu huwa mnafuatwa na wanaume wa maana mnawakataa tena kwa nyodo kisa wamekaa kishamba sio mabishoo,hawana hela lakini umri ukisha enda hao ulio kula nao ujana wote wamesha kukinai hawakuitaji ndo unaanza kuwatafuta hao wavaa mashati ya vitenge uliowakataa huko nyuma waje wakuoe 😀😀😀😀😀😃ila hizi Dunia.
Mm yalisha nikuta mm Kuna demu nilimfukuzia zaidi ya mwaka na nusu tena lengo likiwa ni kumuoa kabisa daah demu Kila nikajaribu anachoma ,sasa alipo ona usumbufu umezidi akaniita sehemu tukutane aisee nilijuta kwenda, demu alinitolea shombo jamani daah nilirudi geto
macho yote yamejaa ukungu sioni vizuri ilinichukua zaidi ya mwaka Yale maneno kufutika kwenye kichwa changu maana yalikuwa ni maneno yaliyo jaa dharau,kejeli,na Kila suna ya matusi.
Baadae tukapotezana na sijui
Hahahahahaa nimecheka kinyama mpaka nimedondoka chini ktk kiti, unamfukuzia mwanamke zaidi ya mwaka? Kuna jamaa hata simu au jumbe fupi zake alikuwa hajibu na akitaka kumkaza simu moja tu bila maelezo mengi.

Siku zote ukimfuata mwanamke mara moja tu na akakujibu hapana usimrudie, atakuheshimu zaidi na hata akirudi ndani ya siku chache mbele tafsiri yake ni kwamba atajua huyu ni mtu mwenye machaguzi mengi na ana mambo mengi ya msingi hana muda wa michezo michezo ya kitoto.
 
Ni kweli labda mtu wa kukutana nae tu
Sasa unakuta ni Mzee wako anaekujua since udogoni,kakulea

Unasikia wenzio wameolewa wamezaa wewe vipi?
shida yako kubwa iko hapa kwenye haya maelezo yako
binadamu ili ubadirike lazima utoke sehemu yenye watu wanaokujua uende sehemu nyingine hapo ndio utapata matokeo tofauti ikiwemo huko kuolewa au kupata mwenza

huko utakapoenda utakutana na watu wengi katika hao wengi yupo mpenzi wako hapo au mumeo kabisa.usipende kukaaa sehemu moja muda mrefu inayokupa matokeo yaleyale ambayo hayakubadirishi kimaisha

labda kama una changamoto nyingine ya kiafya nk useme tukupe ushauri unaoweza kukusaidia
 
Kuzaliwa - Kuoa/Kuolewa - Kuzaa/Kuzalisha - Kufa

Kutoka nje ya haka kamfumo uwe na roho ngumu.

Na Hizo activity za middle zinaumiza wengi na Jamii inazichukulia kama lazima.

Wengine wana changamoto za kiafya.
Wengine tofauti za Kimtazamo na mengineyo.

Zinazofanya wasipite hako ka mchakato.

Mwingine anaolewa mara kapigwa shaba, mara mwingine kachomwa na gunia la mkaa. Mwingine anakuwa na furaha. Mwingine anapojifungua ndio anaondoka hivyo.

Mambo ni mengi.............
 
Kwanza alikuwa hasomi maana alikuwa na miwili tupo naye tu mitaani tangu amalize kidato cha 4 na hata alipo ondoka hakuna ondoka kwa ishu ya masomo.
Alafu tatizo sio kukataliwa tatizo ni kumtolea mtu maneno ambayo yanakufanya ujione wa hovyo kabisa ndani ya dunia hii,kwa sababu yeye si mwanamje wa kwanza kunikatalia kwenye suala la utongozaji.
Ooh basi na utoto pia umri huo wanatongozwa sana huwezi kumjua nani mkweli nani tapeli!
Alafu kama hakuwa na hisia na mm mbona sasa hivi yupo ananisumbua anataka mapenzi na mm au sasa hivi hisia dhidi tangu ndo zimekuja au ni kipi kimebadilika kwake?
Hapo ni either una pesa au kitu anacholenga kutoka kwako, huenda umekuwa aina ya mwanaume anayemtaka sasa!
Kuhusu yeye kuwa mke mwema kwangu Kuna msemo unasema mungu hakupi ukipendacho bali anakupa unacho sitahili.
Sahihi kabisa! Basi ichukulie kama chachu!
 
Back
Top Bottom