Kila nikikutana na wazee/watu wakiniuliza swali "una mchumba?" Najikuta naumia

Kila nikikutana na wazee/watu wakiniuliza swali "una mchumba?" Najikuta naumia

A - Umeamkaje
B - Salama

A - Unaendeleaje
B - Vizuri

A - Nyumbani hawajambo
B - Hawajambo

A - Mkeo/mumeo
B - Wapo salama

A - Watoto
B - Wapo salama

A - Wazazi nyumbani
B - Wapo salama

A - Habari za tangu jana
B - Salama kabisa

A - Fresh kabisa
B - Fresh

A - Mungu ni mwema
B - Amen

A - Tumeamka salama hata sisi
B - Sawa

A - Watoto walikuwa wanaumwa ila nao wapo poa
B - Safi

A - Mm mwnyw mgongo ulikuwa unauma Ila nimeamka salama
B- N vyema
🤣🤣🤣🤣 hivi siku hizi uko wapi(hapo unaulizwa unafanya kazi gani)


Aisee una watoto wangapi?(tayari tunaenda kuulizana mambo private)

Unasubiri nini ona unazeeka mwanangu....


Tupunguze salamm za mda mrefu na kuulizana maswali hayana tija.
 
Sijasema ana kosa naelewa kauliza kujua mfumo wa Maisha ninavyoenda Kwa ujumla na kama Nina lolote jipya.

Mie nimeelezea hisia nnazopata since napata ugumu kwenye suala la kuwa na mwenza.Hali inayopelekea mie kuumia ndani yangu sijui nijibuje.sio kosa langu lakini Kuna muda najiona kama nafeli.

Shida ipo Kwa mtu Baki kukuuliza hivyo halafu anahoji in deep.
USipoteze mda na mwanaume hana malengo na wewe, anakunyima riziki ya kuwa na yule ni sahihi kwako

Usikute unachagua sana aina ya wanaume unaokutana nao?
High standards, like awe na nyumba, gari, sijui tenor. .
 
Kwenye huu uzi hadi dk hii sijamuona ShesRise_1

uKwa sababu hatuwezi kuwafundisha watu maswali ya kutuuliza, na kwa sababu pia Afrika hatupendi kujadili mambo ya msingi, tunapenda zaidi kujadili maisha binafsi ya watu

Basi njia zipo mbili.
Kwanza, kama unaweza kumstopisha mtu anayekuuliza maswali ya ajabu, mwambie waziwazi kwamba hupendi kuulizwa maswali ya aina hiyo

Njia ya pili ni kum ignore, umuache bila jibu lolote

Kama ana akili, ataelewa kwamba masuala ya mchumba, mpenzi, mume, mke na watoto ni mambo binafsi

Hata kama mtu hana vitu hivyo, hakuna kinachoharibika kwenye maisha ya mwingine

Wengine wanaenda mbali zaidi, wanauliza unafanya kazi gani, unalipwa shilingi ngapi na maswali mengine ya ajabu
Yaani mtu timamu kabisa anakuuliza maswali ambayo hayamhusu wala hayabadili chochote kwenye maisha yake! 😏

Sister Abigail ishi maisha baby girl ♥️
 
Nilijua kuna watu watafikiri hivi.

Hapana, logical non sequitur fallacy.

Mzazi wangu amesoma na kuishi US kabla mimi sijazaliwa, don't make that a factor.

Mzazi wangu anaheshimu maamuzi yangu tu. Usichanganye mzazi wangu kuheshimu maamuzi yangu na kuniogopa, much less kwa sababu ya kuishi US.
Anaweza akawa aliishi US lakini ndivyo hivyo tena. Na wewe sasa ndiye unawakilisha mkate mezani mwake. Katika dunia hii ogopa kitu inaitwa ngawira
 
uKwa sababu hatuwezi kuwafundisha watu maswali ya kutuuliza, na kwa sababu pia Afrika hatupendi kujadili mambo ya msingi, tunapenda zaidi kujadili maisha binafsi ya watu

Basi njia zipo mbili.
Kwanza, kama unaweza kumstopisha mtu anayekuuliza maswali ya ajabu, mwambie waziwazi kwamba hupendi kuulizwa maswali ya aina hiyo

Njia ya pili ni kum ignore, umuache bila jibu lolote

Kama ana akili, ataelewa kwamba masuala ya mchumba, mpenzi, mume, mke na watoto ni mambo binafsi

Hata kama mtu hana vitu hivyo, hakuna kinachoharibika kwenye maisha ya mwingine

Wengine wanaenda mbali zaidi, wanauliza unafanya kazi gani, unalipwa shilingi ngapi na maswali mengine ya ajabu
Yaani mtu timamu kabisa anakuuliza maswali ambayo hayamhusu wala hayabadili chochote kwenye maisha yake! 😏

Sister Abigail ishi maisha baby girl ♥️
Asante my ♥️
 
Heri mara mia akuulize hivyo mtoto Ambae hajui Dunia ikoje.changamoto za kupata wenza nk.
Lakini mtu mzima?
Labda mzazi wako sawa...ila haya mambo ni magumu kwakweli
Kwani unadhani mtu mzima ataku fanya nini? Mbona unakuwa na insecurities?

Maisha haya ni yako, kama ukiishi kwa kudhani I kuwa haustahili mwenza utakuwa single milele
 
Anaweza akawa aliishi US lakini ndivyo hivyo tena. Na wewe sasa ndiye unawakilisha mkate mezani mwake. Katika dunia hii ogopa kitu inaitwa ngawira
Baba yangu ana biashara zake tangu sijazaliwa, ana nyumba zake, ana biashara kubwa.

Hana shida ya pesa.

Mwaka jana kuna mtu alimfuata alimuomba amuuzie nyumba yake moja kwa dola za Kimarekani milioni 3, akakataa.

Hana shida ya pesa hivyo.

Usichukulie poa tu kwa sababu kwenu wazee wako hoi wanategemea watoto wao, basi kila familia iko hivyo.
 
USipoteze mda na mwanaume hana malengo na wewe, anakunyima riziki ya kuwa na yule ni sahihi kwako

Usikute unachagua sana aina ya wanaume unaokutana nao?
High standards, like awe na nyumba, gari, sijui tenor. .
Hapana sichagui but Kuna mambo lazima uzingatie.
Mfano mtu mkorofi,muhuni,mshirikina nk
Unajikuta uko mwenyewe
 
Baba yangu ana biashara zake tangu sijazaliwa, ana nyumba zake, ana biashara kubwa.

Hana shida ya pesa.

Mwaka jana kuna mtu alimfuata alimuomba amuuzie nyumba yake moja kwa dola za Kimarekani milioni 3, akakataa.

Hana shida ya pesa hivyo.

Usichukulie poa tu kwa sababu kwenu wazee wako hoi wanategemea watoto wao, basi kila familia iko hivyo.
Wewe Kiranga huwa una sifa za kijinga...

Dola million 3 unazijua wewe?

Acha kushika watu upuuzi.

Mbeba mabox
 
Back
Top Bottom