Kila nikikutana na wazee/watu wakiniuliza swali "una mchumba?" Najikuta naumia

Kila nikikutana na wazee/watu wakiniuliza swali "una mchumba?" Najikuta naumia

Kwa mtu aliye lelewa vizuri na wazazi wake hawezi kuwajibu hivyo wazazi wake labda kwa watu baki ,linapo kuja suala la kudili na wazazi inatakiwa akili na si mihemko utajikuta umesha wakosea adabu.
Hapo wakikuuliza ww ni kuwapa jibu Moja tu ni nipo nalishughulikia basi.
Hizi habari za heshima za kikondoo ni tatizo. Malezi mazuri no pamoja na kumpa mtoto uhuri wa mawazo, uhuru wa kujieleza, uhuru wa kuamua mambo yake mwenyewe, especially kama yupo umri wa kuoa au kuolewa.

Tulivyokuwa wadogo, kuna mzee mmoja alikuwa balozi wa Tanzania nchi moja ya Ulaya enzi za u Rais wa Nyerere siku hizo. Sasa ikawaje sijui, yule balozi akarudishwa Tanzania.

Sasa akarudi akawa jirani yetu. Yule mzee alikuwa anakaa na watoto wake kitashatasha sana, kulikuwa na mtoto mmoja mdogo wa mwisho huyo ndiyo kabisa alikuwa anachezacheza naye kwa namna ambayo sisi watoto wa kibongo tulikuwa hatujazoea, tukaona kama famikla haina maadili, iko kizungu zaidi. Walikuwa wanaongea bery ooenly, hakuna mtoto kuwa na fake modesty na kumuogooa mzazi.

Lakini baadaye tukaja kugundua kuwa malezi yale yaliweza kujenga upendo vizuri zaidi, kumfanya mtoto awe hamuogopi mzazi, kumfanya mtoto awe muwazi zaidi. Kunfanya mtoto aweze kumuelezea mzazi jambo lolote bila kumficha. Nafikiri yule balozi kusoma na kukaa Ulaya kulimfungua mambo mengi katika malezi ya wale watoto.

Na wale wazazi waliokuwa wanapiga piga watoto, wanaogopwa na watoto wao kwa ukali, walijenga distance, resistance, uoga, udanganyifu etc katika familia.

Kwa hiyo, mara nyingine heshima inatakiwa kuwa ina flow pande zote mbili, mtoto aweze kumwambia baba mimi sitaki kuongelea suala hili, na baba akaelewa. Especially kama mtoto si mdogo kivile kama mtu anayeweza kuongelea suala la ndoa.

Tatizo kuna wazazi wa Kiafrika wanaji contradict, mtu mkubwa kabisa mpaka mnaongelea suala la ndoa, chances are anajitegemea, lakini mzazi ana m treat kama mtoto mdogo.
 
😹😹😹 Khaaaaa..!!
Ila kiranga, Kwahiyo hutaki tuchanganyikane?

Huyo lakini naye diaspora mwenzio na ana elimu kama yako kwa madai yake..!!
Acha kufananisha diaspora na dieakiporo 😂😂😂
 
Nadhani ni wakati wako sahihi kunywa dawa yako. Inaonesha umesahau kumeza tembe.
 
😹😹😹 Khaaaaa..!!
Ila kiranga, Kwahiyo hutaki tuchanganyikane?

Huyo lakini naye diaspora mwenzio na ana elimu kama yako kwa madai yake..!!
Kiranga ana matatizo ya akili. Ukiona magazeti mengi, ni kwa vile amesahau kumeza kidonge chake.
 
Ni ngumu lakini bado ipo nafasi
Sure mkuu, watu wanapiga porojo sijui hakuna ulazima lakini mwanaume au mwanamke aliyekamilika anajua upweke wakukosa mwenza wa kihisia, kimwili na kiakili.

Usijisikie unyonge bado hujachelewa, nina ndugu kadhaa wameolewa kwenye miaka 35+, amini nawewe siku yako yaja
 
Ni hali gani inakufanya ukose wa kukuoa?, kuna hii changamoto ya wadada siku hizi kuchagua, elimu + pesa, kuna mmoja alisema siwezi olewa na fundi seremala, huku yeye ana diploma ana mwaka wa 31 moja saizi
 
Huu uzi unaweza ukanipa wife material! Haya mwenye ako na usingle uliokubuhu aje inbox tuyajenge. Nishachoka kua single na mm 30 ndo hiyoo yaja
 
Kama ni wazee wako au watu wenye busara wamefanya vyema kukuuliza.

Ili jamii iwe stshimilivu maswali hayo ni muhimu kuulizwa, kusaidiwa majibu.

Miaka hiyo niliwahi ulizwa hivyo na mama mtu mzima, kutokana na ujana, sikufurahishwa. Ilikuwa ugenini, na yule mama alikuwa na lengo la kuniongoza niweze kufanya maamuzi sahihi.

Kwa minajili ya ustawi wa Jamii, maswali hayo yana maana na ni muhimu sana.
Vijana mtambue kuwa hakuna jambo lako peke yako - hakuna maisha yako, bali kuna maisha ya jamii. Ndio maana kwa jamii iliyostaarabika huwasaidia vijana kuvuka vihunzi muhimu kana ndoa na kazi
 
Mambo yamebadirika sana 😢

Nashangaa kuna kipindi fulani nilikuwa kijijini kwa ajili ya likizo za mwisho wa mwaka, nilikuta wasichana kwa wavulana wameshaolewa na kuowa na familia za watoto wawili au watatu. Wakati nilichunga nao Mbuzi 🐐 utotoni 🤣🤣🤣

Halafu hawana hata stress kabisa, asubuhi Shambani kulima, wakirudi kwenye nyumba ya Slope wanapika chakula wanakula na wana enjoy life.

Kinachochangia kwa vijana wengi kushindwa kuoa au kuolewa mapema ni pamoja na kuwa na vipaumbele elimu kwanza, ajira, sehemu ya kuishi nzuri hata ya kupanga lakini wakati mwingine mambo huenda hovyo na hapo ndipo changamoto zinapoanza kumbe kipaumbele cha kwanza ingekuwa kuolewa au kuoa Yawezekana isingekuwa shida kwenye hili suala la ndoa.

Ukiachana na masuala ya Kiafya naambo mengine tatizo kubwa ni vipaumbele nilivyoviandika hapo juu vikifeli kila kitu kinapoteza muelekeo na tunaoishi mjini mtindo wa maisha unaharibu sana muonekano wa miili yetu
Na hii mtandao ya kijamii - hasa hiyo ya video - imetibua utulivu wa vijana.
Huko mtandaoni inaonekana watu wote wamefanikiwa, ili hali uhalisia unagoma
 
Back
Top Bottom