Kilichofanywa na Iran ni trela tu, ila watazamaji (Israel) wakataka movie nzima wataletewa

Kilichofanywa na Iran ni trela tu, ila watazamaji (Israel) wakataka movie nzima wataletewa

Acha kujitoa ufahamu wafuasi wa taifa teule huwa wana sema kuwa Marekani na nato yote inaitegemea Israel sasa nashangaa leo anaye tegemewa leo kageuka kuwa muomba msaada kwa wanao mtegemea.
Mimi sio mfuasi wa taifa teule, waulize hao wafuasi wa taifa teule. Nilichowahi kuona ni Pro-Russia na Pro-putler wakiibeza US kwamba inaitegemea Israel kiteknolojia na kwamba makampuni yote muhimu ya Marekani yanamilikiwa na Israel.
 
Hoja nyingine za kitoto sana,
Iran ni nchi kubwa mara mbili ya Tanzania ikiwa tajiri wa mafuta, gesi na rasilimali nyingine za madini wakati Israel ni sawa na nusu tu ya mkoa wa Dodoma huku sehemu kubwa ikiwa jangwa.
Mbona Singapore ukubwa wake ni sawa na kisiwa cha pemba lakini haiishi kwa kutegea misaada kama Israel?
 
Mbona Singapore ukubwa wake ni sawa na kisiwa cha pemba lakini haiishi kwa kutegea misaada kama Israel?
Singapore imewahi kupigana vita na nani au imezungukwa na majirani gani maadui au wasioaminika wanaoiwinda muda wote??
 
Singapore imewahi kupigana vita na nani au imezungukwa na majirani gani maadui au wasioaminika wanaoiwinda muda wote??
Israel ina maadui gani wa maana walio mzunguka?
Kwahiyo Hamas na Hizbulah ndo maadui wanao ifanya mpaka Israel itegemea misaada kujilinda?

Vipi kuhusu Iran mwenye maadui tena wenye nguvu kubwa kuanzia za kijeshi na kiuchumi duniani mbona anajilinda kwa kujitegemea mwenyewe?
Vipi kuhusu Urusi aliye zungukwa na maadui mbona hategemei misaada?
 
iran sio jeshi la mtu mmoja, yupo urusi, china, north korea, washia wote. na pia teknolojia ya silaha zote anapata kutoka urusi

halaf pia hilo kundi zima la magharibi ujue kwamba ni nchi tatu tuu..US, UK na France.. na ujerumani kidogo..hao wengine hamna kitu ni wapenzi wasindikizaji
Mbona unaandika mipasho mkuu?
Hukutuwekea ushahidi wa hizo nchi ulizotaja zikiisaidia Iran, hivyo habari yako haina ukweli wala mashiko.

Ila Israel hata mtoto wa miaka 6 anajua kama nchi hiyo inategemea kila kitu kutoka Marekani, UK, Ujerumani, Ufaransa nk. I mean uchumi wao, ulinzi wao, silaha zao na mambo mengine yao yanategemea huruma wa nchi hizo hapo juu. Hizo nchi zikifunga misaada kwa miaka 2 tu hiyo nchi itaweza kutekwa hata na vijana wa Hamas.
 
Niaje waungwana,

Inashangaza mpaka leo Israel pamoja na misaada yote ya kijeshi, kiuchumi na kijamii inayopewa na wazungu lakini bado inashindwa kujisimamia yenyewe dhidi ya taifa lenye vikwazo vya silaha na uchumi ambavyo vimedumu kwa zaidi ya miaka 70. Inachokoza wenye nguvu alaf inakimbilia kuomba wazungu haswa Marekani waisaidie kupambana na aliemchokoza. Hii inanikumbusha dogo fulan wa shule mbabe "mbuzi", aliekuwa anapenda kuchokoza wenzake shuleni au mtaani, alaf ukimgusa anaita kaka zake wakupige.

Siku 1 akajichanganya kwangu, na ukizingatia mimi nilikuwa napata training za karate, hivyo siku naruhusiwa kupigana na kila mtu kuhofia madhara ninayoweza kumsababishia nitakaemtwanga.

Basi siku hiyo dogo akafanya kila awezalo ili nimkanye akaite timu yake. Baada ya uvumilivu kunishinda nikamtia tu singi. Dogo baada ya kutoka shule akaenda kuita brother zake ambae walikuwa hawaishi mbali sana na shule. Ma brother walikuwa wa4, wote walikuwa wakubwa kwangu kiumri. Wanafunzi wenzangu haswa marafiki walinishauri nikimbie kwani ningepokea kipigo kikali kutoka kwao. Nikasema mimi sikimbii na nitachokifanya kwao ndio itakuwa mwisho wa wao kufika hapa kupiga watoto wa shule na mdogo wao kuchokoza wenzake.

Wale kaka zake baada ya kufika wakamuuliza dogo, dogo akani point mimi, ghafla hawa hapa wakataka kunikunja, aisee nilianza na yule aliekuwa wa kwanza kutaka kunishika, kwa speed ambayo hawakuitegemea niliwahi kuushika mkono wake nikakikunja kiganja chake kwa upande wa vidole, jamaa akaanza kulalamika kuwa namuumiza. Wale wengine wakataka kunivamia, nikasema hamtoweza kenge nyie, nilimsukuma yule niliemkunja kiganja, nika deal na wale wa3 waliobakia. Baada ya dakika kadhaa jamaa wakawa hoi wametepeta. Mmoja analia huku kashika pu.m.pu eti nimeuwa nyezo yake ya uzazi, mungine kashika kifua anadai anashindwa kupumua (huyu nilipiga chembe) ili kumkata pumzi haraka asiendelee kunisumbua, mungine yeye analia na chaga zake (mbavu) nilimgusa kwa konzi tu ila ndo hivyo nilimuachia madhara makubwa mbavuni (si unajua ile style ya kupiga pushap kwa kutumia vidole na konzi)

Toka siku hiyo pale shuleni kulikuwa na amani mpaka namaliza shule ile. Sasa hili lililofanywa na Iran ni onyo tu, lakini Israel ishakimbilia kuita wakubwa zake waje kumsaidia kupambana na Iran jeshi la mtu mmoja dhidi ya kundi zima la wamagharibi 😄😂😂. Na bado Iran inaonekana kuwa tishio kwao ukanda mzima ikiwemo Israel yenyewe, Marekani, Uingereza na vibaraka wao.

Kama Israel inajiona ina ubavu wa kupambana na taifa lenye uwezo mkubwa kijeshi, basi iruhusu Marekan na UK wajitengene na vita hiyo ili wabaki wao wawili, ili mwisho tuje tupate jibu kuwa nani ni mbabe wa kweli wa eneo hilo bila msaada wa nchi au mtu mungine. Hawezi kuomba pambano la ngumi alaf uje ulingoni ukiwa na baba yako, mjomba wako, shemeji yako na ndugu zako wote kwa pamoja kupiganan na mtu mmoja alaf baada ya kumchangia utembee kifua mbele eti umempiga.

Ili tuone nguvu zako inabidi upigane tu peke yako. Imagine taifa linatoa kabisa taarifa kuwa litafanya mashambulizi katika nchi yako ili ujiandae kuizuia, pia washirika Marekani, UK nk wakadai wamejipanga toka Iraq, Syria, na Lebanoon kuhakikisha shambulizi halifiki katika nchi lengwa, lakini wazee wa kazi wamepenya ngome zote hadi kufikia eneo husika ambalo ni Kilometres zaidi ya 2000. Je kama wangefanya shambulizi la ambush bila taarifa kama walivyofanya waoga Israel huko Lebanon hali ingekuaje kwao?

Niliwahi kuandika hapa kuwa Iran haijawahi kutishiwa nyau na taifa lolote lile. Ukimwaga mboga, yeye anamwaga ugali tena pipa zima hadi ushindwe mwenyewe.

Kwa ambao hawajawahi kusoma thread hiyo, pitia hizo nyuzi zilizopo pichani hapo chini ili ujifunze zaidi.

Israel kaingizwa cha kike kama mwenzake Ukraine. Sasa atajuta na kusaga meno. Iran sio Iraq, Syria wala Lebanon. I mean jamaa ni waajemi na sio waarab kama wengi wafikiriavyo. Na mziki wa waajemi unafahamika miaka na miaka kabla hata ya kuzaliwa Kristo. Hata biblia inalitambua hilo.
Halafu utakuja kesho hapa tena kutia huruma kwa kichapo itakayopokea Iran
 
ambacho hujui ni kwamba israel ndo marekani mwenyewe, ni sawa na kusema mtoto bila baba hakuna kitu, bila kujua kwamba baba na mtoto ni kitu kimoja, so acha kuongea kitu ambacho hakiwezekani
Marekani hii ya wazungu imeundwa na waingereza miaka 200 tu iliyopita chini ya kijana mwenye asili ya Uingereza hayati George Washington. So usitudanganye kuwa eti Marekani ndo Israel.

Labda useme kuwa Marekani na Uingereza wanaitumia na kuilinda Israel kwa masilahi yao wenyewe pale Mashariki ya kati utaeleweka. Lakini pia Marekani kwa sasa ina mchanganyiko wa raia kutoka maeneo mbali mbali ya dunia wakiwemo wahindi, wayahudi, wazungu wa nchi zingine za ulaya, wachina, waarab, waafrika weusi nk.

So Marekani sio na haitokuwa nchi ya waisrael. Hizi porojo za kutaka kuwaaminisha watu kuhusu Israel zinaanza kuwaumbuweni siku baaada ya siku.
 
Back
Top Bottom