Kilichofanywa na Iran ni trela tu, ila watazamaji (Israel) wakataka movie nzima wataletewa

Acha kujitoa ufahamu wafuasi wa taifa teule huwa wana sema kuwa Marekani na nato yote inaitegemea Israel sasa nashangaa leo anaye tegemewa leo kageuka kuwa muomba msaada kwa wanao mtegemea.
Mimi sio mfuasi wa taifa teule, waulize hao wafuasi wa taifa teule. Nilichowahi kuona ni Pro-Russia na Pro-putler wakiibeza US kwamba inaitegemea Israel kiteknolojia na kwamba makampuni yote muhimu ya Marekani yanamilikiwa na Israel.
 
Hoja nyingine za kitoto sana,
Iran ni nchi kubwa mara mbili ya Tanzania ikiwa tajiri wa mafuta, gesi na rasilimali nyingine za madini wakati Israel ni sawa na nusu tu ya mkoa wa Dodoma huku sehemu kubwa ikiwa jangwa.
Mbona Singapore ukubwa wake ni sawa na kisiwa cha pemba lakini haiishi kwa kutegea misaada kama Israel?
 
Mbona Singapore ukubwa wake ni sawa na kisiwa cha pemba lakini haiishi kwa kutegea misaada kama Israel?
Singapore imewahi kupigana vita na nani au imezungukwa na majirani gani maadui au wasioaminika wanaoiwinda muda wote??
 
Wabongo acheni shobo. Hamna kitu tunachojua kuhusu Vita. Kama ushabiki wa Simba na Yanga umewashinda, basi Fungeni mabakuli yenu.
 
Singapore imewahi kupigana vita na nani au imezungukwa na majirani gani maadui au wasioaminika wanaoiwinda muda wote??
Israel ina maadui gani wa maana walio mzunguka?
Kwahiyo Hamas na Hizbulah ndo maadui wanao ifanya mpaka Israel itegemea misaada kujilinda?

Vipi kuhusu Iran mwenye maadui tena wenye nguvu kubwa kuanzia za kijeshi na kiuchumi duniani mbona anajilinda kwa kujitegemea mwenyewe?
Vipi kuhusu Urusi aliye zungukwa na maadui mbona hategemei misaada?
 
Mbona unaandika mipasho mkuu?
Hukutuwekea ushahidi wa hizo nchi ulizotaja zikiisaidia Iran, hivyo habari yako haina ukweli wala mashiko.

Ila Israel hata mtoto wa miaka 6 anajua kama nchi hiyo inategemea kila kitu kutoka Marekani, UK, Ujerumani, Ufaransa nk. I mean uchumi wao, ulinzi wao, silaha zao na mambo mengine yao yanategemea huruma wa nchi hizo hapo juu. Hizo nchi zikifunga misaada kwa miaka 2 tu hiyo nchi itaweza kutekwa hata na vijana wa Hamas.
 
Halafu utakuja kesho hapa tena kutia huruma kwa kichapo itakayopokea Iran
 
ambacho hujui ni kwamba israel ndo marekani mwenyewe, ni sawa na kusema mtoto bila baba hakuna kitu, bila kujua kwamba baba na mtoto ni kitu kimoja, so acha kuongea kitu ambacho hakiwezekani
Marekani hii ya wazungu imeundwa na waingereza miaka 200 tu iliyopita chini ya kijana mwenye asili ya Uingereza hayati George Washington. So usitudanganye kuwa eti Marekani ndo Israel.

Labda useme kuwa Marekani na Uingereza wanaitumia na kuilinda Israel kwa masilahi yao wenyewe pale Mashariki ya kati utaeleweka. Lakini pia Marekani kwa sasa ina mchanganyiko wa raia kutoka maeneo mbali mbali ya dunia wakiwemo wahindi, wayahudi, wazungu wa nchi zingine za ulaya, wachina, waarab, waafrika weusi nk.

So Marekani sio na haitokuwa nchi ya waisrael. Hizi porojo za kutaka kuwaaminisha watu kuhusu Israel zinaanza kuwaumbuweni siku baaada ya siku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…