Kilichofanywa na Iran ni trela tu, ila watazamaji (Israel) wakataka movie nzima wataletewa

Mwana kulitafuta mwana kulipata. Israel ameyataka mwenyewe kwa uchokozi wake atulie sasa apate anachostahili.

Wamewashindwa Hamas ambao hawana hata kifaru kimoja wala hawana ndege hata moja. Itakuwa Iran? Ngoja akutane na wanaume sasa mana kule Gaza anaua watoto na wanawake
 
😂😂😂vichekesho kama hivi vina patikana wapi ..ogopa sana mtu ana jua una nukes na bado ana kushushia ghadhabu .unazani iran hadi leo hana , afu silaha za iran sio public ni self made, sio kama za myahudi tuna jua ni zile zile za mme wake USA
 
Mnajitekenya na kucheka kifuatacho kilio.
 
Sawa kabisa ila angalia Iran yupo na nani toka maandalizi yao ya vita, au umefuatilia hii vita kuanzia jana.
Rusia kamwambi dogo mtie konzi huyoo..
Vita kubwa haikwepeki. East ndio muda wao wakujipambania uwepo wao.
West ndio muda wao wakutaka kuonyesha kuwa wao bado ni wababe wa Dunia.
Hizi chokochoko kuanzia Ukrein hadi Iran ni maandalizi ya pambano kuu la kihistoria.
Afrika tulime viazi kwa wingi na mihogo ili tuangalie huu mtanange vizuri tukiwa nashibe.

Nyerere alisema tujifunze kujitegemea.
Magufuli pia akakazia ni lazima tujitegemee.
 
Haha hahahah,eti wasindikizaji tuuu,hii ngoma kama Israel atajichanganya atafutika kwenye uso wa dunia,hao Uk,France, UK 🇬🇧 na U S A si wa kuaamini haswa kikiumana,ila huku Iran,North Korea 🇰🇵, Syria 🇸🇾, Lebanon 🇱🇧, Iraq 🇮🇶 🇨China 🇨🇳, Russia 🇷🇺 Jordan 🇯🇴 sio mchezo wanaroho ngumu wanawezapigana hata kwa baiskeli
 
marekani ina mchanganyiko wa mataifa mbali mbali ndio, lakini je ukiacha hao wazungu walioanzisha marekani hao waarabu na weusi na wachina wana sauti gani ya kimaamuzi kwenye hiyo nchi?

pili ambacho hujui ni kwamba taifa la israel limeanzishwa na wayahudi waliokua wanaishi amerca na UK (einsten na wenzake) na hao wayahudi baadhi yao walikua wako kwenye taasisi muhimu za kimaamuzi kwenye nchi hizo, na ndio maana hata katiba za marekani zinaongelea kuilinda israel kivovote, so unapoipiga israel ni kwamba unaipiga america sabab israel ni jimbo la 45 la amerca
 
Taifa la Mungu ni hyped , halina uwezo wowote watu wanapiga tu..Lazima ajiulize kwanza hapo hagusi tena kwa Iran ogopa hao watu ...
Hamas waliua watu 1400 na kuteka wengine , vp Iran kaua wayaud wangap ?

Nan aliwagusa kunako waisrael
 
ushahidi wa nini unaohitaji, unavojua wewe technolojia ya kijeshi ya iran anaipata wapi? kama hujui sema nikupe darasa
 
Hizi ni propaganda uchwara. Hao walioanzisha Israel ni wazungu waliojivika ngozi ya uyahudi kwa masilahi ya Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na mataifa mengine ya Ulaya.

Wayahudi original walikuwepo hapo Mashariki ya kati miaka na miaka na wameishi na waarab kwa amani miaka yote. Kimbembe kilianza baada ya hao wazungu kwenda kupachikwa hapo kwa kisingizia cha waisrael wa mchongo kurudi katika nchi yao ya uongo. Kitu ambacho wenye akili wamekipinga na hata sheria za kimataifa zinajua wazi kuwa hao ni wayahudi wa mchongo ndo maana sheria zao zinasema wazi kuwa hao jamaa hapo Mashariki ya kati ni wavamizi.

Hao jamaa wangekuwa na uwezo wa kufanya maamuzi wasingefanywa watumwa na wamisri, waajemi wa zamani kabla ya kristo (Persia empire) warumi, wagiriki, ottoman empire nk.

Hao jamaa ni weupe ndomaana hadi leo wanategemea kila kitu kutoka magharibi badala ya magharibi kutegemea chochote kutoka kwao. Fikiria mara mbili kabla ya kuandika, sio kulishwa matango pori na wewe kuja kujaribu kutulisha sisi wenye uwezo wa kufikiri. Israel ipo huru na inapokea misaada ya kijeshi na kiuchumi kutoka katika nchi zote zilizowapandikiza hapo Mashariki ya kati, lakini inaiogopa kweli kweli nchi iliyowekewa vikwazo zaidi ya miaka 50 iliyopita na ambayo haitegemei msaada wa sindano wala chumvi kutoka ulaya. Fikiria ulinzi wa anga wa nchi zaidi ya tano, yani Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na Jordan umeshindwa kuzuia mzigo uliotumwa na nchi iliyowekewa vikwazo vya silaha miaka 50. Je ingekuwa haina vikwazo, na hizo nchi zisingemsaidia Israel kulinda anga lake hali ingekuaje?

Tena kwa kujiamini ilishambulia kwa kutoa taarifa ili ikiamini hata mkijiandaa kuizuia itapenya tu. Na kweli ilipenya tu. Sasa ingefanya shambulizi bila taarifa kama ilivyofanya aisrael huko Lebanon hali ingekuaje kwa waisrael wa mchongo?
 
makombora 99% yametunguliwa syria na jordan hayakufika israel, israel walijua makombora yametumwa kwao na walikua wanaendelea na shughuli zao kama kawaida si dharau hizi?
 
pia iran kila kitu kijeshi anategemea urusi yeye kama yeye bila urusi hakuna anachoweza, silaha zake zote ni modified version ya silaha za urusi, so kama israel anasaidiwa na marekani, iran anasaidiwa na urusi sasa shida hapo iko wapi?
 
kuhusu suala la israel ni wazungu au sio hiyo ni mada ingine nitakupa hilo darasa siku ingine, darasa la leo ni kuhusu makombora
 
of course iran huko aliko anatetemeka balaa, hajui kifuatacho kitakuwa nini. israel wamesema ndani ya saa 48 watajibu. uingereza na marekani wameshaweka sawa kushambulia wakitokea cyprus na baharini, the only weapon iran has as of now ni kufunga mlango wa ghuba yake ili meli zisipite, anakuwa kama wahuthi tu. and, do you believe israel itanyamaza kimya tu iran ionekane imeshinda? can that ever happen?
 
😂 Sijui kama watajibu
Mwenye kutambua vizuri nguvu za Iran president Biden ashamtaarifu Israel kuwa yeye hatokuwa nyuma ya shambulizi lolote litalofanywa na Israel maana anafahamu vizuri kuwa Israel ikithubutu kujibu. Safari hii Iran haitotoa taarifa, bali itaivamia Israel kupitia angani na ardhini mchana kwa usiku.

Biden ashamuonya Netanyahu kuwa kama yeye Netanyahu anajifanya kichaa basi Ayatullah ni mwendawazimu kabisa 😂😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…