Kilimanjaro: Mwalimu agomea kuhama, vitu vyake vyatolewa nje Siha

Ni kosa kubwa sana na la kisheria kumhamisha mtumishi wa umma kwa mabavu? Kwanini wanagoma kumsikiliza na kuzingatia security concern anayoitoa? Hebu kuwa na ubinadamu walau kidogo mkuu. Je, ingekuwa wewe na familia yako unahamishiwa kwenye eneo lenye changamoto ya kiusalama ungekubali au kwa kuwa mkuki ni kwa nguruwe?
 
Kuna mtu ameulizwa swali?
Amelipwa stahiki zake.
Tupate jibu ni ndio au hapana
 
Hana sababu yeyote ya kukataa uhamisho maana bado yupo ndani ya Wilaya na analipohamishiwa ni mahali pa kawaida tu kijijini kidogo. Sasa imagine mwaka mzima anakula hela ya watu hataki kuhama anamaana gani?
Kule ni porini, karibia na msitu wa hifadhi ya mlima Kilimanjaro, Nina wasiwasi hata huduma kama zinapatikana?

Unajua kadhia za uhamisho?
Embu mlipe stahiki zake
 
Huu ndio uonevu usio na kichwa Wala miguu.
Halafu Cha kushangaza wanamuona tatizo ni yeye
 
Hii imekaa kimkakati
Kwamba kwenye ualimu Kuna walimu Fulani ni Bora kuliko wengine?
 
Hii imekaa kimkakati
Kwamba kwenye ualimu Kuna walimu Fulani ni Bora kuliko wengine?
Wanamtupa kule ili wamweke mtu wao
Sehemu anayo kwenda ni porini sana
 
Kupenda dezo matokeo yake anadhalilika. Hizo nyumba za bure huwa zinawalemaza sana watumishi. Mtu anaishi nyumba ya serikali hadi anastaafu hana hata kiwanja.
 
Hii imekaa kimkakati
Kwamba kwenye ualimu Kuna walimu Fulani ni Bora kuliko wengine?

How Kuna mahali tumesema hivyo?

Mkuu una assumption tu sasa hivi lakini haujui huyo mwalimu alivyombishi. Inshort huwezi kushindana na mamlaka hujajiari wewe jamaa ameitwa mara ngapi Toka mwaka Jana Hana sababu maalum ya kukataa uhamisho.

Anyway, nisielezee sana maisha ya watu.
 
Sio muelewa kivipi mkuu? Kwanini wamhamishe kwa mabavu bila kufuata utaratibu?

Unauhakika gani hawajafuata utaratibu? Wilaya nyingi walimu wamekuwa wakihamishwa kuziba mapengo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vifo vya watumishi wengine, uhaba wa walimu wa kutosha kwenye somo fulani. Kuna kitengo maalum ndani ya Wilaya ambao kazi yao ni kufanya uhamisho wa namna hii.
 
Kule ni porini, karibia na msitu wa hifadhi ya mlima Kilimanjaro, Nina wasiwasi hata huduma kama zinapatikana?

Unajua kadhia za uhamisho?
Embu mlipe stahiki zake

Dahani Kuna shida gani mkuu inamaana walimu wengine wanaishi je kule? Bado hapo alipo ni jirani tu na kwa Aggrey Mwandri, kuna matajiri huko juu kama familia ya kina Kelvin inamaana hao ni wanyama?

Huyu mwalimu ni mbishi, ameitwa atoe sababu Hana sababu maalum
 

Aliitwa akaambiwa aseme ni usalama gani hakuweza kujieleza kwa mkurugenzi jamaa akaenda hadi kwa waziri mkuu na mkurugenzi na kitengo Cha uhamisho Wilaya ya Siha kikamuita jamaa hakutoa sababu zenye mashiko sasa unataka hawa viongozi wafanye je mkuu?

Huko anapoenda hamna walimu wengine, unajua anyway ila watu wanatumia fursa za shule zenye watoto wengi kwaajili ya fursa za kibiashara wanazopata na huduma ambazo shule zinatoa kama makazi.
 

Unaipangia mamlaka cha kufanya kwenye uhamisho hamna ukongwe au ugeni walimu wote ni sawa wapo chini ya mamlaka sasa unataka huyu mkongwe asihamishwe yeye ni nani kwa mfano?

Jambo la busara ni kuangalia sababu ya huyu jamaa kugoma sio kuhamishwa maana hizi kujiamulia tu hutaki wakati kuna sehem za kutoa sababu za kutokuhamishwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…