Kilimo cha Kisasa cha Mahindi: Mbegu bora, Mbolea bora na magonjwa

Kilimo cha Kisasa cha Mahindi: Mbegu bora, Mbolea bora na magonjwa

pia bei wakati wa mavuno mfuko hauzidi 25,000/= sawa na debe 5,000 au kilo 250/=.

abaki na kilimo kinachotegemea gb na mb tu sio real field farming!
Mkuu kilimo cha kusikia usipimeeeee


Gharama za kuvuna umeacha

Gharama za Kupukucha

Gharama za kusafirisha mbegu

Gharama za magunia

Gharama za kusafirisha mazao

Gharama za Dawa ya kuua wadudu

Gharama za kupakia na kushusha mzigo

Gharama za ulinz shambani


Hiki kilimo we acha tu hahahaha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni fursa pekee nitakayoipigania mwaka 2020.

Iko hivi nilipanda mashimo 2200 ambapo niliweka mbegu 2 kila shimo. Hivyo nilikuwa na mashina kama 4000. Mahindi yalizaa mawili ambapo moja kubwa na lingine dogo. Nilivuna takribani mahindi 5000 na kuyauza kila moja sh 300 na kupata mil 1.5 ndani ya siku 75 na yaliyobakia nilikausha nikapata kama gunia 1. Sasa nimepanda mashimo 6000 na February nitapanda mengine 10,000.

Faida ya Kilimo Cha Mahindi.

1.Hayahitaji dawa nyingi za wadudu zaidi ya dawa moja tu.
2.Gharama zake ni ndogo.Mfano ekari moja unatumia kama laki 4 tu.
3.Wateja wa mahindi mabichi sio issue na hata yakikauka unauza makavu.
4.Hauhitaji kuwa shambani muda mwingi.

Karibuni tulime mahindi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ningependa sana Kupata taarifa jamaa yangu Tunafanyaje hapo?
 
Habari za jioni. Nahitaji kulima mahindi ya kisasa (ya muda mfupi).

Kwa wale wataalamu wa mambo ya kilimo, ni mbegu gani inafaa ukanda wa mkoa wa Geita?

Naomba kusaidiwa aina ya mbegu ambayo natakiwa kupanda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanaume wa Dar 2020 nimekuja kivingine. Nimedhamiria kufanya hili.

Naombeni ushauri wadau, napotea ama?
 
Umeyalimaje?
Nikiwa na maana umetumia mbolea gani kuhakikisha yatakua na kwa wingi na kama umeyalima kwa taratibu zamabwana shamba tafadhali kata yote uanze upya
 
Back
Top Bottom