Ni fursa pekee nitakayoipigania mwaka 2020.
Iko hivi nilipanda mashimo 2200 ambapo niliweka mbegu 2 kila shimo. Hivyo nilikuwa na mashina kama 4000. Mahindi yalizaa mawili ambapo moja kubwa na lingine dogo. Nilivuna takribani mahindi 5000 na kuyauza kila moja sh 300 na kupata mil 1.5 ndani ya siku 75 na yaliyobakia nilikausha nikapata kama gunia 1. Sasa nimepanda mashimo 6000 na February nitapanda mengine 10,000.
Faida ya Kilimo Cha Mahindi.
1.Hayahitaji dawa nyingi za wadudu zaidi ya dawa moja tu.
2.Gharama zake ni ndogo.Mfano ekari moja unatumia kama laki 4 tu.
3.Wateja wa mahindi mabichi sio issue na hata yakikauka unauza makavu.
4.Hauhitaji kuwa shambani muda mwingi.
Karibuni tulime mahindi.
Sent using
Jamii Forums mobile app