Kilimo cha Nyanya: Aina za mbegu, mbinu za kulima na masoko yake

Kilimo cha Nyanya: Aina za mbegu, mbinu za kulima na masoko yake

Tumia selecron, inaua aina zote za wadudu, iwe ni viroboto wekundu, weupe au weusi pia funza aina zote, piga mara mbili kwa wiki kisha endelea mara moja kwa wiki na mara moja kwa siku 14. itakusaidia changanya vizuri maji na dawa. (viroboto=aphids)
 
hao wadudu wanakula aina yote ya nyanya na hata viazi.

Nimekuuliza hivi kwasababu kuna wadudu wameingia siku hizi kwenye variety ya nyanya inaitwa Hasira.
Hao wadudu wanaharibu kama unavyoelezea hapo.
Nakushauri umuone bwana shamba au kama hayupo tumia Selecrone. Ikishindikana jaribu Redomen.
 
Mm Nalima Nyanya Aina Hybrid Kipato F1 Ila Hawa Wadudu wanashambulia nyanya za aina zote kama tanya,lakini pia dawa kama selecron,na zingine ila huwa hawafi lakini jambo la kusikitisha huwa wanashambulia mpaka kitalu
 
konto ni dawa ambayo husaidia mmea kuanzia kitalu mpaka pale unapoanza kutoa maua, hivyo kwa ishu ya kitalu tumia konto, kwa nyanya inayotoa maua ndio hizo dawa za bei kubwa zinatakiwa ambazo hufika mpaka elfu 60, maana naona unajaribu dawa za buku 5 tu.
 
Mm Nalima Nyanya Aina Hybrid Kipato F1 Ila Hawa Wadudu wanashambulia nyanya za aina zote kama tanya,lakini pia dawa kama selecron,na zingine ila huwa hawafi lakini jambo la kusikitisha huwa wanashambulia mpaka kitalu
unajuwa mimi nawasaidia kama mtaalam ili mtu asipate hasara, si mshauri dawa ya kujaribu ila dawa yakukusaidi.selecron haifanyi kazi na hao wadudu wana jenga ukinzani na dawa hivyo tumia hizo dawa ili kuangamiza na mayai yake kwa arusha tumefanikiwa kudhibiti na hivyo wakulima wanavuna nyanya vizuri.
 
Ok mkuu stemcell sasa kati ya dawa ulizosema ipi ni mzuri zaidi? na je huwa inapulizwa baada ya muda gani? na je chupa zake zina ujazo gani ktk lita 20 unatumia cc ngapi? na kwa chupa moja bei gani?
 
Ok mkuu stemcell sasa kati ya dawa ulizosema ipi ni mzuri zaidi? na je huwa inapulizwa baada ya muda gani? na je chupa zake zina ujazo gani ktk lita 20 unatumia cc ngapi? na kwa chupa moja bei gani?
Nakushauri tumia coragen au LIBAX coragen kuna ujazo wa mls 30 kwa chupa na unapiga mls 6 kwa ltr 20 ya maji nani sh 18000 hadi 22000 na Libax inatoka kenya na ni mls 50 sh 15000 na unapiga mls 6 kwenye liter 20 ya maji.
 
Wakuu zingatieni sana ushauri wa Mkuu stemcell, huyu mdudu ni angamizo la kilimo cha nyanya kwa wanaokwenda kichwa kichwa bila kuzingatia utaalamu.

Huyu mdudu ni mkorofi utafikiri ametumwa kuwamaliza wakulima wa nyanya. Mdudu huyu huishi ndani ya jani ambako dawa nyingi hazipenyi zikamfikia, pia hujivingirisha katikati ya jani, dawa haimfikii, na mwisho hujificha juu ya tunda kwenye masikio ya kikonyo cha nyanya.

Mdudu huyu yuko Kilosa tayari ndani ya muda mfupi tu wakulima kibao wamenyoosha mikono juu!! Ingekuwa ni ugonjwa wa binadamu au mifugo ujio wa mdudu huyu ingetangazwa kama ni JANGA !! Mdudu huyu anazaana haraka sana na maisha yake ni siku 24. Kwa hiyo anatabia ya kuwa na ukinzani dhidi ya madawa.

Haishauriwi kutumia dawa ya aina moja zaidi ya mwezi mmoja. Unapobadili dawa lazima utumie dawa inayodhuru kwa njia tofauti na iliyotangulia (Mode of action). Unatakiwa ubadili dawa aina tofauti tatu kabla hujarudia ya kwanza. Yaani ipite miezi miwili kabla hujarudia dawa.

Ni wataalamu pekee wanaojua madawa hayo ya kubadili na si jambo la kukisia na kubahatisha.
 
Kwa faida ya wasomaji, huyu mdudu huko Kenya kabatizwa jina la Al shabaab hapa kwetu anajulikana kama KANTANGAZE.

Nilipotembelea maonesho ya nane nane Morogoro mwaka huu nilikuta dawa inauzwa kwamba ni suluhisho. Dawa hizo Biotrine, Antario na Recharge. Tulielezwa pia kuna dawa karibu itaingia sokoni inaitwa VITAKO inatajwa kwamba ni dawa kiboko kwa mdudu huyu.

Sasa kwa hivi sasa ili kupunguza makali ya mdudu wataalamu huko nane nane walieleza yafuatayo ni madawa yanatakiwa kubadilishwa kwa mzunguko ili kuepuka tatizo la wadudu kuwa sugu kwa madawa.

Match / Dynamec ikifuatiwa na Belt, kisha Ivaset, ikifuatiwa na Pegaset, kisha Karate baada ya hapo rudia mzunguko huo tena. Ndipo hapo nilipoona ukubwa wa tatizo hili.(baadhi ya majina ya madawa hayo naweza kuwa sijayapatia vema kwa vile tulikuwa tunatajiwa na mtaalamu aliekuwa ameelemewa na maswali ya wateja)
 
Kubota

Jamani huku kwetu ndio mdudu ameingia watu wengi wamepiga chini dah nina heka zang kadhaa za nyanya nipeni updates z dawa ya huyu kantangaze na kama ndio hizo naomba muongozo naweza zipata wapi kwa dar...
 
Wakuu Naomba Msaada Nyanya Zinashambuliwa Na Funza Wadogowadogo Wa Kijani Wanakaa Kwenye Majani Yakianza Matunda Wanatoboa Na Kuingia Kwenye Matunda.Nimejaribu Dawa Nyingi Kama Dudu All,ninja,konto Nk Naomba Msaada Nitumie Dawa Gani?

Wasiliana na mwakilishi wa kampuni ya East-West seed Tanzania Limited 0784/0754 466734 wanalo suluhisho la tatizo lako, huyu mdudu ni wa hatari sana, lakini kwa sasa ni historia kwa wakulima wengi wa nyanya mkoani Kilimanjaro.
 
Kwa faida ya wasomaji, huyu mdudu huko Kenya kabatizwa jina la Al shabaab hapa kwetu anajulikana kama KANTANGAZE.
Huyu mdudu nimemsikia pia kwenye maonesho hayo.

Wakasema wametengeneza dawa inaitwa hivyohivyo KANTANGAZE, sijui jina la kisasa la hii dawa.
 
mkuu wala msihangaike na dawa ambazo hamna uhakika nazo, mdudu huyu ni very resistance to any insecticide, ila hii hapa Mimi nimeijaribu Iko vizuri sana, jitahidi kuipiga Mara 2 within a week kama tatizo ni very serious, na baada ya hapo pigaw kila wiki mara 1, dosage ni 10mils/20ltrs of water, (ni muhim usome kibandiko) ....inaitwa MULTIMECTIN plus, inapatikana sana arusha na moshi.
 
mkuu, kwa upigaji huu walaji wa nyanya tutajiepushaje na kansa? huyo mdudu ni majanga kwa kweli.
 
Tafuta dawa inaitwa #Belt made in german inasambazwa na kampuni inaitwa #bayer ina ujazo wa #cc4 kwa pump la 15lt na nyingine ina ujazo wa #cc50 dukani huuzwa 35000/- ndio mwisho wa hao wadudu.
Huwa ni nzuri ukiianza tangu nyanya zipo kwenye kitalu trust me ukitumia hiyo dawa hutojutia usiogope gharama yake.
 
Back
Top Bottom