Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

By mossad007<br />
Nashkuru Mkuu kubota heshma yako sana.

Aisee uliposema mnatifulia kitunguu nimeogopa sna manake iyo gharama yake naona km unaweza kulima heka nyngne tano za mahindi.

Dawa hizi ni msaada mkubwa sna mfano weed stop unapiga mara tu baada ya kupanda hii huzuia nyas yoyote ambayo haijaota isiote tena hii ni maalum tu kw sehem ambayo haijaota nyas ukipiga cc km 60 mpka 80 ivi umemaliza kaz jan halioti mpka unavuna kitunguu lakin kuna majan yanaweza yakawa yalishaanza kuota kipind unapiga weed stop so hapa ndo unapiga Galgan au Oxfan haya magugu yape wiki moja tu yote yamekauka mfano wa kuungua so kw heka moja utatumia elf 60 kudhibiti magugu kw msim mzima mpka unavuna.. kwan ww unalima wap mkuu?
<br />
<br />
Mkuu mossad007 asante sana ndugu yangu, kwa kweli umenipasha kitu muhimu sana, hakuna kitu huwa inanitafuna pesa kama palizi na kutifulia, sisi huku wanaita kupiga godi.

Ninatajiandaa panapomajaliwa siku moja nije kwenye ziara ya mafunzo huko nijionee mwenyewe. Ninalimia vitunguu maeneo ya Kilosa. Naomba niulize nyie wenzetu huko nanyi mnapandikiza vitunguu ndani ya maji kama wanavyofanya huku.

Wakulima huku wengi wamezoea kupandikiza vitunguu kama mpunga na maji wakiwemo kwenye majaruba kisha huyakausha maji baada tu ya kupandikiza, utaratibu huu binafsi naona unamadhara sana kwa udongo na afya ya mimea.

Kwa mfano mtu anaemwagilia kwa kutumia pump, siku yakupandikiza anawasha pump na kuingiza maji wakati wote hadi mwisho wa kupandikiza. Watu wanaingia gharama kubwa sana. Huko mnapandikizaje wenzetu?

Sawa saw kama unavyojua ndugu yangu gharama nyngne kwenye hiki kilimo haziepukiki ila maadam tunatengeneza mitaj mizur kw kuingia hizi gharama bas yatubidi kuziingia.

Kupandikiza kw maj (kuombeka) ipo hata huku lakin sio prefarable wanachofanya huku sna ni kufungulia maj kwenye majaruba a day before kupanda halafu wanachomea yaan unachoma choma jaruba na mjiti then kupanda inakua kesho yake so mpandaji anachomeka mbegu na kuibana vzur na udongo hapa jaruba linakua bado na unyevu then after two days unarudishia maji na kupiga hizo dawa kw jaruba moja hugarim tsh 400 mkuu wakat mwingne mpka 450 inategemea uta negotiate vp.

Nategemea kuja kilosa end of ths April nimeskia kuna maeneo huko karibu na mto gan cjui yupo member hapa JF alileta iyo habar so nimewasiliana nae karibu sna mkuu na huku ujifunze infact toka kilosa mpka ruaha mbuyun ni karibu tu!
 
Mimi nimwana Jf lkn nilikuwa naomba ushauri kwa upande wa soko la vitunguu, hasa huwa vinasoko zuri kipindi gan nikimanisha miezi gani na bei yake hufika ngapi. Na je ningependa kupata kiundani ushauri wa ukulima wa pilipili hoho na soko lake na unaweza toa kiax gani cha hoho kwa hekari moja. Naombeni ushauri wenu wana Jf.
 
Wakuu poleni na kazi.
Mwenye utaalamu wa kilimo cha vitunguu saumu anipe mautaalamu.
Wengi tunajua kuhusu vitunguu maji ila VITUNGUU SAUMU KIDOGO HATUJUI.
 
Siyo peke yako wengine pia tutafaidika kupata utaalamu huo, meneo ya kulima tunayo.

Wakuu poleni na kazi.
Mwenye utaalamu wa kilimo cha vitunguu saumu anipe mautaalamu.
Wengi tunajua kuhusu vitunguu maji ila VITUNGUU SAUMU KIDOGO HATUJUI.
 
Wakuu naona kuna ka ukimya toka hoja iletwe hapa. Nimeona bora nichangie kidogo huenda ikawa msaada kidogo.

Kama unashauku kuzalisha kitu hii fanya kama vitunguu maji tu na wala usifikiri ni kitu cha ajabu sana. Anza na eneo dogo kwanza kisha utatanua kadri unavyoendelea na utaendelea kujua mengi zaidi pale utakapokuwa tayari umeshapanda.

1) Aina za mbegu - nenda sokoni utazikuta na majina yake pia utayakuta, vipo vyekundu na vyeupe, kwa vile hatuna taarifa hizo hadi sasa, anzia hapo. Sokoni watakueleza bei na aina yenye soko zuri. Nunua mbegu aina tofauti kajaribu kuzipanda zote uone matokeo yake wewe mwenyewe.

2) Mazingira yanayostawisha vitunguu saumu - husitawi katika mazingira yale yale kama ilivyo kwa vitunguu, hapa ninamaanisha hali ya hewa, udongo na mahitaji ya unyevu, ni kama vitunguu maji.

3) Mbegu - hupandwa kwa kutumia vipande vipande vya kitunguu, unapukuchua kitunguu saumu kisha unapandikiza vipande vipande hivyo kwa kuvisimamisha wima mizizi au shina likiwa chini. Pandikiza kina cha kuwezesha kufukia visiweze kuonekana.

4) Nafasi ya kupanda ni kama vitunguu maji

5) Magonjwa, wadudu, magugu ni kama ilivyo vitunguu maji hakuna tofauti

6) Havistahimili ukame hasa vikianza kuweka kitunguu, kwa hiyo kama mvua haitoshi mwagilia.

7) vinastawi sana kama ukitumia mboji au samadi iliyooza na pia matumizi ya mbolea zingine ni kama vitunguu tu.

Kama unaweza kuzalisha kitunguu maji jihesabu unaweza kuzalisha kitunguu saumu. Na wengine watajazia au kuboresha zaidi, nawasilisha !!

garlic-row-5-4-05-L.jpg
 
Mkuu kubota nashukuru kwa dondoo zako.
Ila shida ni hapo kwenye kuotesha mbegu. Wengine wanasema huwa zinakatwa ncha ya juu ndo uoteshe na wengine wanasema unaotesha vile vipunje ila hufukii ncha yake sasa hapo ndo shida inapoanzia mkuu.
 
Next time sema ninaomba, kuhitaji means utalipa!!! Ukipata nijulishe na mimi pia nimepata kaplot huko Kisarawe
 
Mkuu kubota nashukuru kwa dondoo zako.
Ila shida ni hapo kwenye kuotesha mbegu. Wengine wanasema huwa zinakatwa ncha ya juu ndo uoteshe na wengine wanasema unaotesha vile vipunje ila hufukii ncha yake sasa hapo ndo shida inapoanzia mkuu.
Mkuu Babalao, zoezi la kukata juu ndo uoteshe hufanyika sana kwenye vitunguu maji vinavyozalishwa kwa mbegu. Kuna mambo mengine hufanyika kwa mazoea mengine ni kwa sababu maalumu.

Ninachokuhakikishia ni kwamba hata bila kukata ukipanda vitaota tu. Kisha unatakiwa uvifukie nchi mbili na nusu ndani ya udongo. Kuna utaalamu mwingine upo siyo maarufu sana niliwahi kuelekezwa na mmarekani mmoja (peace corps) ukishapukuchua vile vi punje, unavitandaza juu ya gunia kisha unavifunika na mchanga kiasi cha kuvifanya visionekane. Zoezi hili lifanyike ndani ya siyo nje.

Kisha unalowanisha na maji hadi mchanga uwe mbichi. Baada ya wiki moja vinaota, vikimea tu pale pale unapanda mara moja. Njia hii inakusaidia kuwa na uhakika maana unapanda kitu ambacho kimeshamea tayari. Lakini kwa wakulima wakubwa njia ni ile ile ya kupanda hivyo vipande vipande hata bila ya kuvikata.

Kwa nyongeza kuhusu aina za vitunguu saumu nimefuatilia sana nimepata taarifa kuwa kuna vitunguu saumu huingizwa toka China, ni vyeupe kabisa na vina punje zake kubwa kuliko za kienyeji na zinamenyeka kirahisi sana, nimeambiwa wachina huwa wamezipulizia dawa, kwamba hazioti.

Kwa hiyo ukiamua kutumia mbegu ya vitunguu vyeupe uwe makini huenda ukakutana na vya kutoka china ambavyo huenda kweli havioti ila sina uhakika.
 
Mkuu Babalao nilisahau kukujulisha kuwa mahitaji ya samadi ni kilo 2 kwa kila mita moja ya mraba. Unahitaji uwe na vitunguu saumu vya mbegu kilo 200 hadi 300 kwa eka moja kutegemea na nafasi na aina ya vitunguu vyenyewe.

Inachukua miezi 4 na zaidi toka kupanda hadi kuvuna kutegemea na hali ya hewa na aina ya mbegu. Eka moja unaweza kuvuna tani 5 hadi 6.

Dalili ya kukomaa ni pale majani yanapoanza kuwa ya njano au kahawia kisha mashina huinama na hata kukauka kabisa.
 
Kubota nashukuru sana hapo umenipa somo zuri ntakupa matokeo yatakavyokuwa.
 
mkuu kubota kwa upande wa hali ya hewa, kuna sehemu za baridi kama pale maeneo ya karibia Uyole Mbeya wanalima kitunguu saumu, sasa je sehemu za joto inakuwaje kama mfano pale Ruaha mbuyuni au huko kisarawe kote kitunguu saumu chaweza kustawi?

maana kuna jamaa mmoja alipanda mwakajana kitunguu saumu maeneo ya mbozi sehemu ya utambalila, hali ya hewa yake ni joto la wastani cyo kama ruaha mbuyuni, kile kitunguu kilikataa kabisa japo moja ya sababu ni mvua ilikuwa chache na alichelewa kukipanda ilikuwa kama mwezi wa pili mwishoni hv!
 
Zao la vitunguu swaumu ni zao ambalo linaonekana limesahaulika japo linalipa sana,
Nilikua manyara mwaka jana nilipata jifunza haya yafuatayo:
/zao hili haliitaji maji meng kama ilivo vitunguu maji huitaji maji mengi mara moja kwa mwezi
/ zao hili huchukua mieZ 4 hadi 5 kuweza kua tayari kuingia sokoni
/ zao hili haliuzwi kimagunia wala kimadebe ni bei sana hivo linauzwa kwa neti ( net moja ni sawa na beseni moja na nusu) ambayo bei ya neti moja n shillingi elfu 56.
/ bei ya mbegu mara nyingi huwa wakulima wazao hili wananunua kwa mabeseni ambapo beseni moja la mbegu ni shillingi elfu 35
/ zao hili huna haja ya kubeba na kupeleka sokoni wanunuzi wanakufata wenyewe na mafuso yao japo ukienda navyo mombasa au sudani pia uganda ni ghari sana huuzwa huko.
/ mahali ambapo zao hili hustawi n katika udongo wa pemben mwa mabonde udongo ambao sio mgumu sana mtanisamehe aina ya udongo sijui ila mabonden lakn maji yawe yanazuiwa na kuruhusiwa mara moja kwa mwezi au hata mara mbili cio mbaya ila yawe kwa wingi yaende chini,
/ mikoa ya manyara , singida morogoro na baadh ya mikoa ya kusimi yanasupport sana
 
Mm nipo sumbwawanga vijijini je zao hili linaweza kulimwa

Pia ninaomba kama kuna mtu anaweza kunitafutia vijana wa wili wakazi kama wataalaam wangu

Pamoja tujenge uchumi
 
Back
Top Bottom