mossad007
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 1,165
- 852
<br />By mossad007<br />
Nashkuru Mkuu kubota heshma yako sana.
Aisee uliposema mnatifulia kitunguu nimeogopa sna manake iyo gharama yake naona km unaweza kulima heka nyngne tano za mahindi.
Dawa hizi ni msaada mkubwa sna mfano weed stop unapiga mara tu baada ya kupanda hii huzuia nyas yoyote ambayo haijaota isiote tena hii ni maalum tu kw sehem ambayo haijaota nyas ukipiga cc km 60 mpka 80 ivi umemaliza kaz jan halioti mpka unavuna kitunguu lakin kuna majan yanaweza yakawa yalishaanza kuota kipind unapiga weed stop so hapa ndo unapiga Galgan au Oxfan haya magugu yape wiki moja tu yote yamekauka mfano wa kuungua so kw heka moja utatumia elf 60 kudhibiti magugu kw msim mzima mpka unavuna.. kwan ww unalima wap mkuu?
<br />
Mkuu mossad007 asante sana ndugu yangu, kwa kweli umenipasha kitu muhimu sana, hakuna kitu huwa inanitafuna pesa kama palizi na kutifulia, sisi huku wanaita kupiga godi.
Ninatajiandaa panapomajaliwa siku moja nije kwenye ziara ya mafunzo huko nijionee mwenyewe. Ninalimia vitunguu maeneo ya Kilosa. Naomba niulize nyie wenzetu huko nanyi mnapandikiza vitunguu ndani ya maji kama wanavyofanya huku.
Wakulima huku wengi wamezoea kupandikiza vitunguu kama mpunga na maji wakiwemo kwenye majaruba kisha huyakausha maji baada tu ya kupandikiza, utaratibu huu binafsi naona unamadhara sana kwa udongo na afya ya mimea.
Kwa mfano mtu anaemwagilia kwa kutumia pump, siku yakupandikiza anawasha pump na kuingiza maji wakati wote hadi mwisho wa kupandikiza. Watu wanaingia gharama kubwa sana. Huko mnapandikizaje wenzetu?
Sawa saw kama unavyojua ndugu yangu gharama nyngne kwenye hiki kilimo haziepukiki ila maadam tunatengeneza mitaj mizur kw kuingia hizi gharama bas yatubidi kuziingia.
Kupandikiza kw maj (kuombeka) ipo hata huku lakin sio prefarable wanachofanya huku sna ni kufungulia maj kwenye majaruba a day before kupanda halafu wanachomea yaan unachoma choma jaruba na mjiti then kupanda inakua kesho yake so mpandaji anachomeka mbegu na kuibana vzur na udongo hapa jaruba linakua bado na unyevu then after two days unarudishia maji na kupiga hizo dawa kw jaruba moja hugarim tsh 400 mkuu wakat mwingne mpka 450 inategemea uta negotiate vp.
Nategemea kuja kilosa end of ths April nimeskia kuna maeneo huko karibu na mto gan cjui yupo member hapa JF alileta iyo habar so nimewasiliana nae karibu sna mkuu na huku ujifunze infact toka kilosa mpka ruaha mbuyun ni karibu tu!