Dodoma moja : kweli kabisa ukulima unamtuoa mtu, mimi nimeamini coz kuna watu wameanzisha sijui niseme makampuni kaajiri watu kwenye heka kama 15 unakuwa umewagaia vyeo kabisa masupervisor mpaka kibarua then kazi yako inakuwa kusupply chakula na matumizi yote ya shamba cha kushangaza most of them ni kenyans sijui watanzania tunaogopa nini mimi nimeamua moja hata nikianguka naanza upya tena mpaka nitoke :hand:
Rafiki yangu, sisi watanzania tuna maajabu yetu kaka. Mimi nalima shamba kubwa kiasi lakini challenge kubwa inayonikabili ni nguvukazi kwa maana ya watu wa kufanya kazi.
Wenyeji wa eneo lilipo shamba langu naweza kusema hawana moyo wa kazi, mtu anakuja kufanya kazi siku moja ukimlipa anaenda kutumia hela hadi iishe ndio anarudi kufanya kazi tena, inaweza kuchukua hadi wiki ndio mtu arudi tena.
Katika hali kama hiyo nakuwa nashindwa kutimiza malengo yangu. Kwa mfano lengo langu kwa mwezi January ilikuwa nilime ekari 25 lakini niliambulia kulima ekari 11, watu hawafanyi kazi. Inanilazimu kwenda mikoani kama kanda ya ziwa na Dodoma kutafuta watu wa kuja kulima huku pwani, hao watu inabidi niwajengee kambi shambani na kuwasimamia kwelikweli ndio kazi iende, yaani kama wanafanya kwa kujitolea vile kumbe wanapata malipo.
Kwahiyo ndugu yangu usishangae kuona wakenya wanaajiriwa hadi mashambani, sisi userious wa kazi ni mdogo na ni tatizo kubwa sana. Sometimes nakuwa nikifikiria sana nagundua hata wakoloni walipoamua kujenga miundo mbinu kama reli na barabara hawakuwa na jinsi bali kuwashikia fimbo na mijeledi mababu zetu, bila hivyo wabongo hatuendi ndugu yangu.
Samahani kwa kutumia maneno yasiyo mazuri sana ila niko dissapointed mno na baadhi ya wananchi wenzangu. Tunajaribu kugawana hiki kidogo kwa kupeana viajira hivi vya mashambani lakini tunaangushana kwelikweli, jamani maofisini tunajaza raia wa kigeni (Experts),biashara zimeshikwa na wageni, sasa hata mashambani tuweke wageni?
Watanzania hebu tupende kazi bwana tunajiangusha wenyewe!