Kim Jong-Un aagiza muuza filamu kupigwa risasi hadharani

Kim Jong-Un aagiza muuza filamu kupigwa risasi hadharani

May 30, 2021 by Global Publishers

kim.jpg

MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Lee, ameuwawa kwa kufyatuliwa risasi pamoja na familia yake huko Wonsan Korea ya Kaskazini baada ya kukamatwa akiuza Cd na Pamoja na Flash ambazo zilikuwa na filamu kutoka nchi Jirani ya Korea ya Kusini.

Lee pamoja na familia yake walipigwa risasi uwanjani mbele ya watu 500, ikiwa ni fundisho kwa watu wengine wanaouza filamu kutoka nje.

Kiongozi wa taifa hilo Kim Jon Un alipiga marufuku kuangalia filamu za nje kwa kuhofia nchi kuingia kwenye utamaduni wa nchi za magharibi.

Taarifa zinaseama watu zaidi ya 20 wamekamatwa kwa kosa hilo la kuuza filamu na Muziki na wanatarajiwa kuhumiwa kwani wameunja sheria za nchi hiyo.

Aidha unaweza kufungwa miaka saba jela kwa kosa kutotoa taarifa za mtu anayeuza filamu na Cd za Muziki kwa polisi.




Siyo kila kiongozi ana akili, wengine ni weu sana. Vituko vya huyu kiduku vina hakiki kwamba huyu hazimo. Duniani tunapita, huyo kapita kwa kuondoka kikatili lakini kimu naye atapita. Anaweza kuja pita vibaya na kwa aibu...kesho ya kiduku inaweza kuja kuwa mbaya sana.
 
Ukiwa na nuclear weapons tu tayari wewe upo huru, ila Uhuru ukiutumia vibaya matokeo yake ndio hayo
 
Chama Cha Mapinduzi ni chama rafiki wa Chama Cha Kikomunisti cha China.
 
Hakuna mtu anataka kuzikwa na matundu ya risasi mwili mzima.

Hata wewe usingethubutu kama ungethubutu ungeandama peke yako nchi nzima.
Sawa ila ni udhalimu wa hali ya juu sana dhidi ya uhai wa binadamu
 
Lee pamoja na familia yake walipigwa risasi uwanjani mbele ya watu 500, ikiwa ni fundisho kwa watu wengine wanaouza filamu kutoka nje.

 
Back
Top Bottom