Kim Jong-Un aagiza muuza filamu kupigwa risasi hadharani

Kim Jong-Un aagiza muuza filamu kupigwa risasi hadharani

May 30, 2021 by Global Publishers

kim.jpg

MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Lee, ameuwawa kwa kufyatuliwa risasi pamoja na familia yake huko Wonsan Korea ya Kaskazini baada ya kukamatwa akiuza Cd na Pamoja na Flash ambazo zilikuwa na filamu kutoka nchi Jirani ya Korea ya Kusini.

Lee pamoja na familia yake walipigwa risasi uwanjani mbele ya watu 500, ikiwa ni fundisho kwa watu wengine wanaouza filamu kutoka nje.

Kiongozi wa taifa hilo Kim Jon Un alipiga marufuku kuangalia filamu za nje kwa kuhofia nchi kuingia kwenye utamaduni wa nchi za magharibi.

Taarifa zinaseama watu zaidi ya 20 wamekamatwa kwa kosa hilo la kuuza filamu na Muziki na wanatarajiwa kuhumiwa kwani wameunja sheria za nchi hiyo.

Aidha unaweza kufungwa miaka saba jela kwa kosa kutotoa taarifa za mtu anayeuza filamu na Cd za Muziki kwa polisi.
Kiduku inatakiwa apigwe kama Sadamu Huseni maana anafanya upuuzi as if hakuna sheria za kidunia za haki za binadamu aanzovunja.
 
Tunatangaza ya NK ya kwetu maiti kukutwa kwenye viroba na muhuni kama sabaya kutembea na genge lake kupora na kuteka tunaona kawaida...wabadilisha fedha za kigeni waliporwa fedha wengine bila maandishi...
 
Duh,na mijananchi ya huko imekaa tu hata haindamani kupinga,yaani uhai uondokw kwa kosa la hivyo kweli,huyo dogo ni zaidi ya sheitwan aisee
Wakiandamana kuna uwezekano wakauliwa wote, anayedai ni kiongozi wao, hajali utu wa yeyote.
 
Wakiandamana kuna uwezekano wakauliwa wote, anayedai ni kiongozi wao, hajali utu wa yeyote.
Ni kweli yule dogo sijui nani atatokea amuassasinate,familia yao imeiharibu sana ile nchi aiseee,inatakiwa ajitokeze mtu/watu wa kujitoa muhanga,haiwezekani akifa huyu,anakuja let say mtoto wake and the like,ndio maana wamejimilikisha nchi wanaona wengine ni wanyama na wanaweza kuwafanya vyovyote vile wapendavyo
 
Hao jamaa wanaishi dunia yao tu ,kuuliwa huko ni jambo la kawaida tu
 
huyu naye kijana alijitakia,naamini Kama ni raia wa pale naamini anamjua vzr kiduku kichaa chake,au kijana aliamua kumtest kiduku
 
Kim dawa yake atafutiwe wazaramo wa 5 wakamchambe kwa tabia zake mbaya za kikatili...maana humanitarian reasons hazimuingii akilini
 
Mzungu sio mtu mzuri aliweza wajaza sumu ndugu leo hii wanachukiana na kuonana kama maadui
 
Jamanii na Familia yake wakauliwa aisee kumbe bora Tanzania huko kwingine ni kugumu zaidi kuishi
Ni kweli Tanzania kuna unafuu mkubwa sana. Ila ni muhimu kusema kwamba Katika miaka ya hivi karibuni, wapinzani na wakosoaji wame suffer haswa.
 
Daah UCHAWI UPO [emoji16][emoji16][emoji16].
Yaani Kim anaua lakini bado watu wanampenda
 
Hii taarifa umeipataje, wakati nchi haipo jury hata kwenye taarifa ya habari
 
Back
Top Bottom