May 30, 2021 by
Global Publishers

MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Lee, ameuwawa kwa kufyatuliwa risasi pamoja na familia yake huko Wonsan Korea ya Kaskazini baada ya kukamatwa akiuza Cd na Pamoja na Flash ambazo zilikuwa na filamu kutoka nchi Jirani ya Korea ya Kusini.
Lee pamoja na familia yake walipigwa risasi uwanjani mbele ya watu 500, ikiwa ni fundisho kwa watu wengine wanaouza filamu kutoka nje.
Kiongozi wa taifa hilo Kim Jon Un alipiga marufuku kuangalia filamu za nje kwa kuhofia nchi kuingia kwenye utamaduni wa nchi za magharibi.
Taarifa zinaseama watu zaidi ya 20 wamekamatwa kwa kosa hilo la kuuza filamu na Muziki na wanatarajiwa kuhumiwa kwani wameunja sheria za nchi hiyo.
Aidha unaweza kufungwa miaka saba jela kwa kosa kutotoa taarifa za mtu anayeuza filamu na Cd za Muziki kwa polisi.