Wakuvelumba
JF-Expert Member
- Feb 22, 2024
- 279
- 488
😂 wakamwita na tapeli visadi mkubwa wakamtundika na msalabaniTaifa la Mungu yupi? Yule waliye muua wao wenyewe wayahudi? Au unamzungumzia Mungu yupi?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
😂 wakamwita na tapeli visadi mkubwa wakamtundika na msalabaniTaifa la Mungu yupi? Yule waliye muua wao wenyewe wayahudi? Au unamzungumzia Mungu yupi?
Unaowaita wastaarabu Spain,Brazil,Belgium hao ndio wamekataa kuwatambua Hamas kama magaidi.Dunia ya kigaidi, ile ya kistaarabu hamas ni magaidi
This is a fallacy of generalisation.Niaje waungwana?
Wazungu baada ya kuona wamefanikiwa kutawala sehemu kubwa ya dunia haswa haswa katika bara zima la Afrika, wakaona kuwa hata uongo wao pia watakaoleta kwa watawaliwa utaweza kuishi milele, bila kujua kwamba zama zinabadilika na akili za watawaliwa nazo pia zinabadilika.
1. Kwanza wazungu walitudanganya kuwa wanakuja kutukomboa kiuchumi na kiroho, kumbe nyuma ya pazia lengo lilikuwa ni kututawala, kumiliki ardhi yetu na kila kilichopo katika nchi zetu.
2. Pili walitudanganya kuwa binadamu wa kwanza au wa kale walikuwa ni manyani, lakini hapo hapo kupitia vitabu vitakatifu vya dini wakatuambia kuwa binadamu wa kwanza alikuwa ni binadam wa kawaida ambae jina lake ni Adam.
cha kushangaza katika vitabu vinavyoonesha kuwa binadamu wa kwanza walikuwa nyani, utakuta waliochorwa ni watu weusi, na vile vinavyoonesha kuwa binadam wa kwanza alikuwa Adam utakuta amechorwa mzungu, hivyo ni wazi kuwa binadam wote tulikuwa ni binadam wa kawaida kutoka kwa baba yetu Adam, hao nyani tulioambiwa ilikuwa ni uongo mahususi uliotengenezwa kwa malengo yao watawala (wazungu)
3. Tatu wanadanganya kuwa pale Mashariki ya kati nchi yenye nguvu zaidi za kijeshi ni Israel, lakini wengi tumeshuhudia kwamba Israel haina tofauti na Ukraine, kwamba kila inapotaka kupigana na adui yake, au hata kikundi cha vijana wasiozidi hata 20,000 kama vile Hamas lazima waombe msaada wa silaha kutoka Marekani, huku UK na EU nao wakiipa kwa njia ya kimya kimya ili kupambana na kakundi hako.
Bora hata Ukraine inapambana na taifa ambali ni la kwanza kwa ukubwa duniani, taifa ambalo Ukraine inaingia zaidi ya mara 10, lakini pia ni la pili kwa nguvu za kijeshi duniani, hivyo kutokana na udogo wake na pia utoauti wa nguvu za kijeshi, ina haki ya kuomba msaada kutoka katika nchi nyingine. Lakini Israel inaomba msaada wa kifedha na silaha hata pale inapopambana na kikundi cha watu wachache wasiofika hata elfu 50 ambacho sio nchi, sasa inawezaje kuwa taifa lenye nguvu kuliko nchi zote za eneo hilo?
Mbona tukifuata uhalisia wa kweli bila kutanguliza mihemko ya kipropaganda za magharibi ni kama vile Israel haiwezi kufua dafu hata mbele ya mziki wa Iran kijeshi, japo nchi hiyo ina vikwazo lukuki vilivyodumu kwa zaidi ya miaka 70. Kama vikundi vidogo vidogo vinavyodhaminiwa na Iran iliyowekewa vikwazo kwa takribani miaka 70 Hezbollah, Hamas na vinaitoa kamasi Israel inayodhaminiwa kijeshi na kifedha na Marekani kwa zaidi ya miaka 80 tena bila kikwazo hata kimoja, je hiyo ndio ya kuuita yenye nguvu hapo Mashariki ya kati zaidi ya nchi zingine? Kuna kikundi kidogo tu cha vijana kadhaa kilichopewa silaha mbili tatu na Iran hapo Yemen, kimesababisha nchi kubwa duniani zaidi ya 10 kuingia baharini kwenda kupambana nacho. Hivyo kudai kuwa Israeli ni taifa lenye nguvu kwa sasa, kwakweli ni uongo wa dhahiri ambao kwa dunia ya leo watu wanaanza kuushtukia kutokana na kile kinachoendelea katika eneo hilo.
Fikiria hiyo miaka zaidi ya 70 ambayo muisrael anapewa misaada ya kijeshi na kifedha na Marekani pamoja na vibaraka wa magharibi, kama pia ingetumika kutoiwekea vikwazo Iran hali ingekuaje, bado wangeendelea kudanganya hivi hivi au wangeongea ukweli kwa sababu ingekuwa ngumu kuuficha ukweli huo?
4. Walidanganya kuwa Russia ni nchi hatari kwa usalama na amani ya dunia, japo Russia ni wazungu wenzao, lakini ukweli ni kwamba wazungu wa nchi za West ndio wanaoongoza kwa kuhatarisha usalama na amani katika nchi za wenzao. Wengi tuliona jinsi wafaransa walivyopachika wavaa kobaz huko Mali, Niger, na kwengineko ili aweze kutumia mwanya huo kuiba rasilimali za nchi hizo kupitia maeneo yale ambayo serikali haiwezi kuyadhibiti tena. Hata miaka kadhaa iliyopita Msumbiji iligundua kuwa katika eneo la kusini mwa nchi yake kuna utajiri mkubwa wa gesi, hivyo waliingia mkataba na kampuni fulan ya kifaransa kwa lengo la kuja kuchimba gesi hiyo kwa makubaliano maalum, bila kujua kwamba nchi hiyo ya kusini mwa Afrika inakaribisha nyoka katika ardhi yake.
Miezi michache tu baada ya wafaransa kuingia eneo la kazi na kuisoma vizuri ramani, wakaunda kikundi cha wavaa kobaz kama ilivyozoea kufanya katika nchi Mali, Niger, Gabon nk. Lengo la kuunda kikundi kile ni kutaka lile eneo lisitawalike na kampuni yao ijifanye inakimbia kutokana na sababu za kiusalama, kumbe nyuma ya pazia wawe bado wapo wanachota gesi hiyo watakavyo huku wakiwapa silaha na hela ya kula viongozi wa wavaa kobazi ambao wanajua kile kinachoendelea katika eneo hilo. Hivyo kusema kuwa Russia ni nchi hatari kwa usalama na amani ya dunia ni uongo mtupu wanaojaribu kutudanganya sisi watawaliwa ambao wanahisi hatuwezi kujua lolote.
Uongo wao ni mwingi, siwezi kuuorodhesha wote, ila wajue kwamba watawaliwa tumeshaamka, sio kila tango pori watakaloturushia sisi tutalimeza bila kulimung'unya ili kujiridhisha kuwa ni lenyewe kweli au tango la miba.
Labda Spain ya mme wakoUnaowaita wastaarabu Spain,Brazil,Belgium hao ndio wamekataa kuwatambua Hamas kama magaidi.
Wewe maskini mlala hoi wa Temeke ni nani mpaka uwaite Hamas magaidi?
Spain anapata faida gani kumtetea Hamas!?
Au Spain nao nchi ya magaidi!??
Kumbe nabishana na msenge asiyefuatilia hata taarifa ya habari??Labda Spain ya mme wako
Sawa mama,salimia anayekupakuaKumbe nabishana na msenge asiyefuatilia hata taarifa ya habari??
Huna akili kaa pembeni,unaonekana hata habari hutizami.
Bwabwa hili.😂😂🤣
Uwe makini unapojadili mada za mliganyo, unasema wazungu waongo na ni watu wabaya je ni watu Gani ni wazuri kwakoAma kweli wazungu walituchukulia sisi maboya.
Sasa hapa sijui wataleta uongo gani kwa picha kama hizi 😄😄😄
Hali inazidi kuwa mbaya kwa Israel. Mwaka sasa unaisha vijana elf 20 tu wa Hamas wasiokuwa na kifaru wala ndege yoyote ya jeshi wameshindwa kumalizwa, mateka wameshindwa kuokolewa na matakwa yao ya kusimamisha yamekataliwa.Thread za kujifariji tu hizi ila mzigo wanaopiga IDF pale GAZA hakika jamaa ni watabe mno, IDF ni mojawapo ya jeshi Bora kabisa duniani.
Mbugi Inapigwa GAZA, inapigwa LEBANON inapigwa SYRIA tena kwa wakat mmoja na kwa ufanisi mkubwa sio jambo dogo.
Kuna uongo mwingi tulidanganywa na wazungu zama za giza. Lakin kama wasemavyo wahenga kuwa muda ni mwalimu mzuri anaeweza kukuonesha au kukufundisha kile usichokijua.Uongo mkubwa nilioaminishwa na wazungu kua kuna haki za binaadamu pamoja na mahakama ya uhalifu wa kivita, kumbe haki za binaadamu ni kwa ajili ya wazungu tu na mahakama ya uhalifu wa kivita ni maalumu tu kwa wale wanaenda kinyume na maslahi yao.
Hii dunia imejaa unafki wa kiwango cha standard gauge.
Hata huyo Mungu unaesema kawaumbua ni wa kwao kwaiyo hata kusanuka kwako bado hakuja kusaidia kitu.Jamaa wana uongo mwingi, bahati nzuri Mungu kaanza kuwaumbua kwa kila uongo wao.
Acha ujinga kijana. Kwani kuna mtu ana Mungu wake peke yake!!Hata huyo Mungu unaesema kawaumbua ni wa kwao kwaiyo hata kusanuka kwako bado hakuja kusaidia kitu.