Kinachosikitisha wa Tanzania waliozamia SA wemerudi na umaskini

Kinachosikitisha wa Tanzania waliozamia SA wemerudi na umaskini

Sio sahihi, kuhama sio kufanikiwa, na kubaki sio kufanikiwa, yanayofanikiwa ni malengo dhabiti, nidhamu na mikakati!

Mimi nimekaa South Africa 5 years, na ndo mda niliweza nunua kiwanja na kujenga nyumba yangu ya kwanza.

Nisingeenda kamwe, nisingeweza kujenga Njiro miaka ya 2007, na pia nisingeweza kupanuka kifikra za Biashara.

Wewe unafikiri Kuna Mkurya au mtu wa Iringa waliolelewa mikoa hiyo anaweza aende nje arudi Kizembe? Ni Hawa waliolelewa Kinondoni na Magomeni unawapima!
Hoja inamashiko
 
Seran najua hata wewe ulirusha ndoano ukaambulia manyoya boya wewe.
Ndio maana nakwambia kua wewe ni kapumbavu,unafikiri wote hua tuna hivyo vitabia vya kitoto? Seran yupo bongo,mimi nipo huku,kwahiyo kwa akili yako jiongeze hapo,
Sasa unafikiri nikimfungulia uzi akanikataa mbele ya watu ndo kanikataa?
Tafuta kazi ya kufanya Pimbi wewe,acha kushinda jf na vinyuzi vya kijinga jinga,au ndio unatolea stress zako za malezi yako ya hovyo uliyo yapitia toka kwa Babako wa kambo?
Licha ya hivyo wewe inakuuma nini
Ndio ujiulize sasa,hao wabongo waliorudishwa toka South,Wewe kinakuuma nini?
kama sio trauma tu zinakunyonya boya wewe
Trauma unazo wewe Pimbi uliyeteswa na Baba wa kambo kwenye makuzi yako.
 
Kwa South Africa kwa nature ya nchi ilivyo ni ngumu kwa mgeni hasa kama hana rasilimali kufanikiwa. Ila kwa Ulaya na Marekani kama mtu atajituma kwa bidii bila kuchagua kazi na akaacha maisha ya anasa atafanikiwa.
Mkuu ulaya ya sasa sio ile ya Miaka ya 1990..
Now imekuwa njaa tupu,
Japokuwa huwezi lala njaa ila kufanikiwa kwa ukubwa ni ngumu sn.
 
Sio sahihi, kuhama sio kufanikiwa, na kubaki sio kufanikiwa, yanayofanikiwa ni malengo dhabiti, nidhamu na mikakati!

Mimi nimekaa South Africa 5 years, na ndo mda niliweza nunua kiwanja na kujenga nyumba yangu ya kwanza.

Nisingeenda kamwe, nisingeweza kujenga Njiro miaka ya 2007, na pia nisingeweza kupanuka kifikra za Biashara.

Wewe unafikiri Kuna Mkurya au mtu wa Iringa waliolelewa mikoa hiyo anaweza aende nje arudi Kizembe? Ni Hawa waliolelewa Kinondoni na Magomeni unawapima!
I second you
 
Mkuu ulaya ya sasa sio ile ya Miaka ya 1990..
Now imekuwa njaa tupu,
Japokuwa huwezi lala njaa ila kufanikiwa kwa ukubwa ni ngumu sn.

Ni kweli mkuu imebadilika na kufanikiwa kwa ukubwa sio rahisi mzee na sema angalau ya kula na akiba kidogo. Sio kuchoka kwa kiwango cha hao waliotoka Afrika Kusini.
 
Ni kweli mkuu imebadilika na kufanikiwa kwa ukubwa sio rahisi mzee na sema angalau ya kula na akiba kidogo. Sio kuchoka kwa kiwango cha hao waliotoka Afrika Kusini.
Uzuri wa ulaya utakula vzr utalala vzr na kazi utafanya ila haikidhi nahitaji ya kufanya makubwa tanzania,
Ila kwa japan, Canada, America, Australia,nk zipo powa
 
Uzuri wa ulaya utakula vzr utalala vzr na kazi utafanya ila haikidhi nahitaji ya kufanya makubwa tanzania,
Ila kwa japan, Canada, America, Australia,nk zipo powa

Ooh sawa sawa.

Kwa hiyo ulivyorudi Tanzania ulipata familia na maisha sio Mwandende 🤣
 
Mwaka 2010 niliwahi ishi Greece kwa miezi 6..
Kipindi hicho nipo under 30 ..
Athens nilikuta watanzania wengi sn,,wenye maisha mazuri na maisha ya kutubu.
Mimi nilikuwa miongoni mwa vijana ambao walikuwa na maisha magumu sn pale Athens.
Ndipo mzee wng mmoja mtanzania akaniweka chini akanishauri.
Mwandende"wewe bado mdogo sn,,
hapa Greece hapakufai,,utapoteza muda wako bure..
Mimi nina umri wa miaka 50 now,nipo hapa tangu 1998 , najuta kuwa hapa hadi sasa,,
Sina pesa na pia sina family zaidi ya ile niliyoacha Tanzania.
Tanzania nimeacha mke na mtoto mmoja tu,,,
sipendi na wewe yakukute.. natamani kurudi nyumbani Nashindwa.

Nakushauri tafuta maisha pia tafuta na family .
watu wengi wanaoishi ulaya hawana family .
Rudi nyumbani kajipange upya,
Tafuta maisha na tafuta family pia,
Ukikosa maisha unaweza ukapata maisha mazuri kupitia watoto wako hapo baadae...ukiwa hapa hutotengeneza family,.watu wengi hapa wanaishi kisela tu.

Nilimsikiliza yule mzee na kuamua kurudi Tanzania..

Nilichojifunza kwa watanzania wengi wanaoishi Africa kusini,na baadhi ya inchi za ulaya na America kusini zenye maisha magumu.
Wengi hawana maisha na family pia hawana..
Wamekosa vyote...
Mtu yupo south miaka 30 hana mke wala mtoto na ameshakuwa mtu mzima...
Mtu una over 55 umeishi nje zaidi ya miaka 30 hata ukirudshwa Tanzania now utafanya nn?...
Huna maisha na family pia huna.
Kwani kuwa na mke na watoto ndio maisha?

Kwani ni lazima kila mtu awe na mke na watoto?
 
Mkuu lazima uelewe kwamba majuto ya maisha ya mwanaume yanaanza ukiwa na miaka 55.
Hapo ndy utaelewa nn namaanisha..

Kwa sasa huweziona umuhimu wa kuwa na family,,
Muda utaongea

Kweli mkuu waache wajidanganye kuishi bila kuwa na familia. Au kuwa na watoto ambao hawana muda nao, kwa umri huo watakosa hata wa kumuuguza.
 
Kila siku huwa nasema ugumu wa Maisha upo popote pale usijidanganye kwamba kuhama nchi ndio kufanikiwa , wanaohama nchi na kufanikiwa ni wale waliofanikiwa kwenye nchi zao walizotoka , kama nyumbani umeshindwa kufanikiwa usidhani ugenini ndio utafanikiwa , tuliza mshono baki bongo .
Hawa watu choka mbaya kabla ya kuondoka walikuwa na sifa zipi?
 
Back
Top Bottom