Kinana, Mbowe, Vuai, Mnyika, Chenge na Heche wajifungia kwa vikao vya saa 4 Courtyard


Please, hivyo ni vikao vya CHADEMA na CCM wanajadiliana mambo ya kufanya siasa kwa Uhuru na sio mafarakano Kama ilivyokuwa Happ nyuma. Kuhusu maendeleo ya wananchi Kuna Rais, Mawaziri, bunge, Halmashauri na wenyeviti wa vijiji na vitongoji. Walaumu hao Kama hujapata maendeleo
 
Kuwafunda akina nani???Mwizi akikufundisha wizi utamkubali kama una akili timamu???Eti majizi yawafunde CHADEMA nendeni mkawafunde TLP.
 
Km una mke zaidi ya mmoja, na wake zako wameamua kupatana kua makini sana...something fish is cooking...
Na hili tunaliona kwa jinsi walivyoukalia kimya mfumuko wa bei, Umeme na Maji...
Kama wananchi wenyewe wanakenulia meno magumu yote yanayoendelea sahau kuwa yatapiganiwa na wanasiasa.
 

Walishindwa kumfundisha kinana aache kumsema vibaya Magufuli kwenye simu ndio waje kuwandisha CHADEMA ambao hawapokei ruzuku ya serikali kwenye kipindi kigumu hiki.

Walitakiwa CCM ndio wajifunze kwa CHADEMA jinsi gani walivyoweza kusurvive miaka miwili bila rizuku ya chama.
 
Hiyo ndiyo busara. Siyo kila mazungumzo unatoka nje kuzungumza na vyombo vya habari. Siamini kama walopigania uhuru wa nchi walitumia sana media. Media inatakiwa iwe ya mwisho
 
Na hili tunaliona kwa jinsi walivyoukalia kimya mfumuko wa bei, Umeme na Maji...
Mfumko wa bei na tatizo la maji na umeme mahala pake sahihi pa kujadiliwa ni Bungeni kwenye 99.99% ya wabunge toka CCM. Sasa kama CCM ndiyo wenye serikali na Bunge ulitaka wajipinge wenyewe!!??
 
Yanaanza lini hayo maonob, niyasubiri Kwa kigoda kabisa
 
Hilo la Chenge na rasimu ya Warioba kuna uhusiano gani?
 
Bila kupewa semina na ndugu Kinana mpaka muda huu wangekuwa wameshaanza kusema kila mtu na lake Kama kawaida yao ya kutaka kuwa wakwanza,maana ndani ya Chadema kila mtu Ni kambale
 
Wewe huoni chadema walau wamebadilika kidogo kitabia na kuwa na Tabia za kiutu uzima za kuwa na Subira na utulivu
Kwa sababu CHADEMA ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo,wanapaswa kutulia ili waone ccm ndani ya muda wa miaka mitano watakavyoipaisha nchi bila ya CHADEMA na vyama vingine vya upinzani,kama waliondlewa kimakusudi inabidi nao watulie kimakusudi.
 
Kuna siku CCM, CDM na ACT wataamka watajikuta wapo out of touch na wananchi.

Hawa vijana chini ya 30 watakuja kubadilisha siasa za hii nchi.
Hawa wavaa skin jeans,washabikia nyimbo za sodoma na gomora huku wakishinda mabar na clubs wakitingisha matako usiku kucha na kwaito?!! Hawa Hawa role models zao WBC hawamjui hata Kolimba ama Imran Kombe achilia mbali Mabere Marando ama Mtikila?!!
 
Kinana atakuwa anawafundisha siasa...waachane na harakati za mahakamani..wajue siasa..
Wajue Ku compromise madogo ili wapate makubwa...
Siasa sio kushinda Kesi mahakamani
Nani amefungua kesi mahakamani?


Tuanzie hapa kwanza.
 
Hakuna upinzani Tanzania. Kinana anawaambia nyie tulieni tule wote. Familia na vilembwe wetu wafaidike. Achaneni na majority ya watanzania wajinga hohehahe.

Upinzani upo Sana tu, ndio maana 2020 mtandao wa internet ulizimwa kipindi Cha uchaguzi mkuu. Halafu ushaidi mwingine ni kuzuiliwa kwa mikutano ya siasa kwa miaka Saba saasa. Ingekuwa Tanzania hakuna upinzani mpaka Sasa hivi kungekuwa na mikutano ya hadhara na Wala internet isingezimwa kwa wiki mbili kisa kupika matokeo.

Sema upinzani wa Tanzania ni wavumilivu na wapenda amani ndio maana utafanya machukizo yote dhidi ya Upinzani lakini utaondoka na kuuacha Upinzani.
 
Km una mke zaidi ya mmoja, na wake zako wameamua kupatana kua makini sana...something fish is cooking...
Na hili tunaliona kwa jinsi walivyoukalia kimya mfumuko wa bei, Umeme na Maji...

Uchaguzi ukija mnajifanya kuipenda CCM , mkipata matatizo mnaanza kuilaumu CHADEMA. Ulitaka CHADEMA waongee kuhusu mfumuko wa Bei halafu Bei ndio itapungua?. Nendeni mkawalaumu mliowachagu 2020. Mnachagua CCM miaka yote halafu lawama ya mfumuko wa Bei unaitupia CHADEMA tuache unafiki.
 
Mambo ya chini chini kwenye issue isiyotaka usiri kama uhuru wa siasa itakuja kuzaa kashfa! Usikute kuna maslahi ya watu yanajadiliwa kabla ya makubaliano kwenda public!
 
KWAO NI KUBORESHA MAZINGIRA YA SIASA.. SIO MAISHA YA MTANZANIA...

LILE SWALI MLIKUWA MNAULIZA WALE AKINA ZITO NA MBOWE MBONA KIMYA... HILI NDILO JIBU...

MAGUFULI ALIWANYIMA MAZINGIRA YA KUFANYA SIASA NA KULA PESA ZA BURE... SAMIA KAWAPA..
Mazingira mazuri ya siasa ndiyo yatakayoketa hali nzuri za maisha ya wananchi.Siasa ndio kila kitu.leo tunalalamika maisha magumu bila kujua hiyo inatokana na matokeo ya siasa zetu.siasa iko kila mahali kwahiyo kazima ijadiliwe kwanza ili kupitia siasa nzuri wananchi waneemeke.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…