Pre GE2025 Kinana: Rais Samia wanayemsema ndio ameleta uhuru uliopo nchini sasa hivi, akisema kuanzia leo hakuna maandamano itakuwa nini?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Majibu mepesi ya kinana hyatamzuia lissu kuendelea alipoishia Tena atakuja na hoja zingine mpya.uwezi keleta majibu mepesi kwa maswali magumu
 
Asante sana mkuu 'Yoda' kwa mada hii. Nilikuwa nasikia tu watu wakisema Kinana kajibu hoja za Tundu Lissu, lakini sikujua kaongea nini.
Umefanya mhtasari mzuri sana, na majibu uliyotoa naona hata yeye akikusoma atajiona hoja zake zinao upungufu mkubwa.

Nadhani nyakati za hawa akina Kinana sasa zimefika, wapumzike tu, kwa sababu hawana jipya la kuichangia nchi hii. Sasa wamebaki kuwa watetezi wa viongozi wasiokuwa na dira yoyote kuhusu nchi wanayo iongoza.
Hili halishangazi sana, kwani sijawahi hata mara moja kusikia kiongozi wa nchi akijitangaza uraia wake, kwanza ni wa nchi shiriki katika Muungano, na ule wa Muungano unakuja baada ya uZanzibari Kwa hiyo sasa najiuliza, kama hata kitambulisho cha taifa cha Tanzania anacho, au kashikilia tu kile cha Zanzibar?

Kinana anataka watu wakaombe na kubembeleza kuhusu uhuru wao unaowaruhusu kukusanyika na kufanya mikutano? Hajui kuwa ingewezekana kuwepo na mtafaruku mkubwa sana wakati huu ndani ya nchi kama angeendeleza amri hiyo ya Magufuli?. Kinana anataka watu wavurugane?

Nakupongeza pia kwa lugha iliyonyooka vizuri kabisa katika uandishi wako.
 
Ni dhahiri Kinana Amezeeka na hana tena uwezo wa kufikiria, Hata hivyo huwezi kuwa na Zaidi ya miaka 80 ukabaki na uwezo wa Ujana, Lawama ziwaendee waliomtuma kujibu asiyoyaweza
Biden 81, M7 80; yule wa Equatorial Guine, nadhani zaidi ya 90! Hawa bado wanapambana na vijana!

Uwezowa Kinana umebaki katika kuipatia CCM ushindi kwa kutumia mbinu za hujuma. Hana kitu tena, hana ushawishi wa kujenga hoja.
 
Keka refu sana je ukitaka kujua wakenya hawalalamiki kuhusu time yao ya Uchaguzi muulize odinga
 
Keka refu sana je ukitaka kujua wakenya hawalalamiki kuhusu time yao ya Uchaguzi muulize odinga
kwa kiasi nakubaliana nawe, lakini kamuulize Odinga huyo huyo ilikuwaje kashindwa kuchukuwa madaraka wakati serikali na viongozi wake walikuwa upande wake. Si wangeamua tu kumpitisha Odinga? Unajuwa kwa nini ilishindikana kufanya hivyo?
 
kwa kiasi nakubaliana nawe, lakini kamuulize Odinga huyo huyo ilikuwaje kashindwa kuchukuwa madaraka wakati serikali na viongozi wake walikuwa upande wake. Si wangeamua tu kumpitisha Odinga? Unajuwa kwa nini ilishindikana kufanya hivyo?
Na viongozi wa tume walikuwa upande wa nani?
 
Na viongozi wa tume walikuwa upande wa nani?
Waligawanyika. Wengi (wanne) wakawa upande wa Odinga, lakini Mwenyekiti wa Tume katumia madaraka yake kumkingia kifua Ruto.
Na mbaya zaidi, hata kesi ilipopelekwa mahalkamani, ushindi ukawa wa Ruto.
Sasa point hapa ni hii:Angalawa palikuwepo na 'process' iliyofanyika. Haikuwa ni swala la kujinyakulia tu madaraka kwa mamlaka aliyokuwa nayo Rais Uhuru na kumpa Odinga.
Hili kamwe huwezi kulilinganisha na haya yetu hapa.
Nadhani kwa mara ya kwanza najikuta nawatetea Kenya
 
Siasa za ushindani si ndio? Subiria Samia atoke mtakoma ,nasubiria Kwa hamu sana kusikia vilio nitawakumbusha tuu
Nasema hivi, hatuhitaji huruma ya kiongozi yoyote, tunahitaji haki tu. Hata akija mlevi mwingine wa madaraka, haimanishi tutamuona Samia alikuwa wa maana, maana sisi tunachohitaji ni haki. Kama Samia angekuwa ana huruma tungeona tume huru ya uchaguzi, na Katiba mpya.
 
We nae unaona eti umeandiiiika na halafu ukaridhika kabisa kwamba umemjibu sawa sawa mh Kinana!! Machagadema mkiambiwa akili zenu ni sawa na nyumbu mnakasirika!
 
Kinana anasema wabunge hawaendi bungeni kwa idadi ya watu Bali hoja! Kwa hiyo anamaanisha Wazanzibar na uchache wao wanahoja zaidi kuliko sisi wabara! Hapo ndio nimejua hoja ya Lisu itawamaliza ccm.
 
Nilieleza na nitaeleza tena.Mtu tamim wa kujibu hoja za Lissu anatakiwa atulie na kujibu kwa akili na si kujibu ili kujibujibu tu.Usije ukadhani umejibu kumbe umejivua nguo saa sita mchana kwenye soko la kijiji na umebakia umevaa shanga tu kiunoni.Damn it!
 
Kampa hoja zaidi za kuzungumza.The old man is too tiresome to hold the agenda.Too tiresome!
 
Ni dhahiri Kinana Amezeeka na hana tena uwezo wa kufikiria, Hata hivyo huwezi kuwa na Zaidi ya miaka 80 ukabaki na uwezo wa Ujana, Lawama ziwaendee waliomtuma kujibu asiyoyaweza
Yaani hapo ndiyo wamefiwa mwisho. Kwa Sasa chama hakina mtu wa kujibu hoja. Ndiyo maana bado wanawategemea hao wazee wa Kivukoni ambao wamepitwa na wakati. Anajibu kipropaganda tu.

Akina sijui CPA Makalla na Dr. Nchimbi ndiyo wangeharibu kabisa.

Hata wana CCM wenyewe hawakuonekana wakishangilia kwa nguvu kama kawaida yao. Either hawakuridhika na majibu au na wao wa Nakubaliana na hoja za upinzani.

Pia kitendo cha kuelekea mashambulizi yote kwa CDM ni propaganda. Akina Jussa na Wazanzibar wengi amefanya mijadala ya Muungano, au Kinana na CCM hawajaiona huko mitandaoni. Wao wa nawaona CDM tu...!?
 
Biden 81, M7 80; yule wa Equatorial Guine, nadhani zaidi ya 90! Hawa bado wanapambana na vijana!

Uwezowa Kinana umebaki katika kuipatia CCM ushindi kwa kutumia mbinu za hujuma. Hana kitu tena, hana ushawishi wa kujenga hoja.
Mmmm, lakini Biden siyo dictator, hajalazimisha wala kubadiri katiba. Hao wengine ni dictators waliolazimisha katiba ili kubaki madarakani,
 
Na tatizo linguine ambalo CCM inalikabili ni kuendekeza wazee wenye siasa za uzoefu bila elimu na maarifa. Apoongea mCCM utajua tu huyu ni CCM wana ile tabia ya kulinganisha na matatizo ya wengine ili kuhalalisha ya kwao. Halafu wanarukia juu juu, na hawatoi concept kwa nini Sweden au Lesotho wana wabunge 300etc.

Lisu kinyume chake anajisomea na kweli ana full knowledge ya anayoongea na reference. Kwa mfano Kinana kasisitiza mara zaidi ya tatu kuwa Bush mdogo aligombea Urais na Hilary Clinton, (sijui lini), na kuwa ati Mahakama ndiyo iliamua. Vile vile majaji wa Supreme Court huchaguliwa na Rais wa Chama kilichoko madarakani, na hujipendelea. Kwanza inaelekea hata kujibu hotuba hakujitayarisha, hakuna hata mwaka mmoja Bush mdogo aligombea Urais na Clinton; ilikuwa ni Albert Gore. Huwezi kutamka zaidi ya mara tatu kwa bahati mbaya ati Bush aligombea na Clinton.

Kuhusu uamuzi wa Mahakama (Supreme Court) kuamua; anasahau kumbe kwa Tanzania uchaguzi ukiisha hata mahakamani hairuhusiwi kesi kupokelewa. Ati Chama hujipendelea kuchagua majaji wake, yeye na chama chake process hiyo huuishia kwenye kuiba uchaguzi, utafikaje kwenye kuchangua majaji wakati hata kesi mahakamani inakuwa haijafika? CCM + Police + Jeshi = CCM existence.

Lisu bado atwatesha sana kwa sababu anaongea facts, ingawa zingine zinauma kuzisikia, yule ni next level.
 
KINANA BADO KABISA HAJAJIBU HOJA KAPIGA KELELE TU
 
Keka refu sana je ukitaka kujua wakenya hawalalamiki kuhusu time yao ya Uchaguzi muulize odinga
Kenya walishatoka katika huo ujinga wa tume kubeba wagombea wa uchaguzi.
Hakuna mbunge, seneta, gavana au MCA waliolamika katika huo uchaguzi kuhujumiwa na tume, Odinga peke yake hatoshi kuwa rejea kuhusu tume yao.
Na pia Odinga sio mtu wa kuhujumiwa na tume na kukubali yaishe mepema tu.
Kenya wana matatizo yao mengine katika demokrasia ila tume kuibia watu kura, kuengua au kutangaza wagombea walioshindwa sio mojawapo.
 
Lisu alisemaga wenye kuishi kwa uongo hawawezi kuusema ukweli !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…