Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Makamu Mwenyekiti wa CCM anazungumza na waandishi wa habari na wanaCCM katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Dodoma. Kikwete anategemewa kuzungumzia masuala mbalimbali ikiwemo kujibu shutuma mbalimbali zilizoibuliwa na upinzania ambazo CCM wameziita ni za kibaguzi dhidi ya Muungano.
Kinana
CHADEMA wametutuhumu CCM, Serikari na Rais kwa mambo ya uongo. Hatukatai kukosolewa na kusahihishwa, lakini hatukubali kuzuliwa wala kushtumiwa kwa mambo ambayo hayapo au ni ya kutunga. Kubwa walilofanya kwenye mizunguko yao ni kujenga chuki na mfarakano miongoni mwa Watanzania.
Mkishindwa hoja ndiyo zenu.yes,
kibaraka nu mjanja sana kwa mabwenyenye![]()
Tundu Lissu aliongea kama Makamu mwenyekiti hivyo anajibiwa na Makamu Mwenyekiti, hao wengine ni wepesi na rahisi sana kuingiwa na jazba.Makala na Nchimbiwazee wa "kutatua kero kisayansi" wako wapi ...
Tulitegemea wao ndio wamjibu Lissu.
Makamu Mwenyekiti wa CCM anazungumza na waandishi wa habari na wanaCCM katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Dodoma. Kikwete anategemewa kuzungumzia masuala mbalimbali ikiwemo kujibu shutuma mbalimbali zilizoibuliwa na upinzania ambazo CCM wameziita ni za kibaguzi dhidi ya Muungano.
Abdulrahman Kinana
CHADEMA wametutuhumu CCM, Serikari na Rais kwa mambo ya uongo. Hatukatai kukosolewa na kusahihishwa, lakini hatukubali kuzuliwa wala kushtumiwa kwa mambo ambayo hayapo au ni ya kutunga. Kubwa walilofanya kwenye mizunguko yao ni kujenga chuki na mfarakano miongoni mwa Watanzania.
Hoja zao na ufafanuzi wa Chama cha Mapinduzi
1. Katiba
Wanasema wanataka Katiba Mpya na kutushawishi katiba mpya ni muhimu - Mwaka jana 2023 tumekubali hoja ya katiba mpya, na wanatanzania wanaitaka katiba mpya, tunachobishania ni lini, wao wanataka ipatikane leo. Rais Samia wakati anandoa zuio la mikutano ya hadhara alikubali pia kuhusu suala la katiba. Haya mambo yanahitaji muda na tafakuri, lakini wenzetu wanasema hapana, katiba inahitajika sana.
Katiba yetu imepokea mabadiliko mara 14, na ukitazama madailiko hayo mara nyingi yalilenga siasa, madaraka na uchaguzi, hata msukumo wa sasa wa CHADEMA lengo lake ni uchaguzi. Serikali imetunga sheria tatu za uchaguzi ambazo zimepita bungeni na Rais kutia saini, sheria ambazo zilitolewa maoni na wadau mbalimbali ikiwemo mpaka bungeni kwa siku nne, ambapo hoja za msingi zilikubaliwa lakini CHADEMA hawakuridhika, bado wasema Rais asihusishwe kwenye uchaguzi wa viongozi wa Tume, sijaona nchi ambayo Rais hahusishwi kwenye maamuzi mfano China, India, Kenya, Afrika Kusini kote Rais anakuwa na maamuzi fulani juu ya Tume.
CHADEMA walitaka suala la Katiba liwe la CHADEMA na CCM kama chama kikuu cha upinzani na chama tawala, hili haliwezi kufanyika, sababu katiba sio suala la vyama hivi viwili pekee.
Kwa sheria hii nawahakikishia Tume hii itakuwa Huru na kufanya kazi kwa uadilifu, Mweyekiti, Makamu na watendaji watakula kiapo kufanya hiyo kazi, labda kama tunataka malaika kufanya hizo kazi, lakini kazi hizi lazima zifanywe na binadamu.
Sheria ya Uchaguzi
Muungano
Kuligawa taifa katika majimbo
Kinana katoa Siri Chadema mlitaka vyama vingine visihusishwe kwenye kikosi Kazi Cha Katiba mpyaBahasha za Khaki
Hawawezi propaganda hao.Makala na Nchimbiwazee wa "kutatua kero kisayansi" wako wapi ...
Tulitegemea wao ndio wamjibu Lissu.
Subiri kesho, magazeti yote yatakuwa na picha moja na kichwa cha habari kimoja. Hao waandishi tayari wamekwishapewa nini cha kuandika.Bahasha za Khaki
Mbona suala la bandari halikupewa muda? Mbona suala la Ngorongoro halikupewa muda?Haya mambo yanahitaji muda na tafakuri, lakini wenzetu wanasema hapana, katiba inahitajika sana.
Bunge la mchongoSerikali imetunga sheria tatu za uchaguzi ambazo zimepita bungeni na Rais kutia saini, sheria ambazo zilitolewa maoni na wadau mbalimbali ikiwemo mpaka bungeni kwa siku nne, ambapo hoja za msingi zilikubaliwa
Hivi kwa akili tu ya kawaida unaweza kuamini hilo. Wote tunajua basics za katiba mpya. Uzuri tulishaona mchakato wake before.Kinana katoa Siri Chadema mlitaka vyama vingine visihusishwe kwenye kikosi Kazi Cha Katiba mpya
Una akili KubwaKwa mkutano huu, ccm wamewasha moto rasmi
Uzushi hausaidiiMasikini Comrade amebaki peke yake kama kisiwa kisicho na wavuvi, CCM ni hivi sasa ni sawa na kasha tupu baada ya Mangula kuchoka na kukabidhi mitambo kwa Nape! Ukimuangalia Kinana unamuona kuwa hana mtu anayeweza kuongea naye lugha moja wakaelewana ndani ya chama.