Pre GE2025 Kinana: Rais Samia wanayemsema ndio ameleta uhuru uliopo nchini sasa hivi, akisema kuanzia leo hakuna maandamano itakuwa nini?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kinana ajibu haya maswali:
1. Kwa nini leseni ya Tanzania haitumiki Zanzibar
2. Kwa nini Mtanganyika hawezi kununua ardhi Zanzibar
3. Kwa nini Mtanganyika hawezi kuwa DC Zanzibar
4. Kwa nini Wazanzibar wengi wameajiriwa Wizara ya Afya huku Tanganyika wakati afya siyo suala la Muungano
5. Kwa nini Mtanganyika hawezi kupiga kura Zanzibar
6. Kwa nini Wazanzibar wanakuwa viongozi kwenye masuala yasiyo ya Muungano Tanzania


NB: Wazanzibar wanabinya nafasi za Waislam wa bara kuwa Rais Tanzania maana mara nyingi Rais akitakiwa kuwa Muislam anatokea Zanzibar na akiwa Mkristu anatokea Bara. Hii siyo sawa maana Waislam wa Bara wanakuwa wanabaniwa nafasi ya kuwa Rais. Kati ya Marais watatu Waislam wa Tanzania wawili wametoka Zanzibar. Na JK alikuwa rais kwa sababu Zanzibar ilinyimwa zamu yake la sivyo hatungeweza kuwa na Muislam wa bara RAIS hadi leo
 
Kumbe hakunaga namna Rais wa Nchi ataweza kujiweka kando na Uteuzi wa viongozi wakuu wa Tume Huru ya Uchaguzi

Hata Kenya na Africa Kusini ambako makamu Mwenyekiti wa Chadema mh Tundu Lisu anaona Tume Huru ya Uchaguzi ni Bora Bado Mwenyekiti anachaguliwa na Rais

Nasubiri majibu ya Tundu Antipas Lisu kwa makamu Mwenyekiti wa CCM komredi Kinana

Nawatakieni Dominica Njema
 
Unawateua unawaapisha wakutii wewe kisha unasema wako huru! Ni ujinga.
 
Makala na Nchimbiwazee wa "kutatua kero kisayansi" wako wapi ...

Tulitegemea wao ndio wamjibu Lissu.
Hawawezi propaganda hao.

Huoni mzee wa propaganda anavyojaribu kuspin. Eti katiba mpya inahitaji muda... Wakati mchakato ulishaanza miaka 10 iliyopita. Naona Warioba watakufa bila kuona matunda ya kazi yake.
 
Nyangumi wa siasa za Tanzania amepiga chafya katikati ya bahari ya siasa Tanzania, wimbi lake si dogo, na usiombe ukutwe na "kimbunga" cha chafya hiyo, Toleka Kibinda.

Kama ni gari, limekaa switch on, oil ipande, tayari kwa safari ya uchaguzi 2024/2025, hapa CCM huwa wanakuwa na umoja kama ruba na ngozi, au siafu
 
Tutaona kama waandishi hao watathubutu kumuuliza kuhusu ile katiba iliyoandaliwa na Jaji Warioba, thubutu.
 
Kinana katoa Siri Chadema mlitaka vyama vingine visihusishwe kwenye kikosi Kazi Cha Katiba mpya
Hivi kwa akili tu ya kawaida unaweza kuamini hilo. Wote tunajua basics za katiba mpya. Uzuri tulishaona mchakato wake before.

Kinana ni spin master wa CCM aliyebakia kwa sasa. Anachokifanya ni propaganda tu.

Hivi kajibu na maswali ya Muungano...!?
 
Uzushi hausaidii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…