Pre GE2025 Kinana: Rais Samia wanayemsema ndio ameleta uhuru uliopo nchini sasa hivi, akisema kuanzia leo hakuna maandamano itakuwa nini?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
CCM hadi leo wanaona haki za wananchi kama kukusanyika, mikutano ya siasa ni hisani ya rais na wala siyo haki za msingi za katiba yetu. Hapo ndiyo wanakwama sana na kuonekana hawana maana.

Ila hawa wazee wa ccm wake wakijua wao leo wapo kesho wakiondoka kitakuja kizazi kitagawana mbao kuanzia muungano mpaka mikoa. Ni bora wao kwa busara zao warekebishe ingali wana muda.

Kinakuja kizazi cha walafi humo humo ndani ya ccm ambacho hakitaogopa wala kujali huo muungano na ndiyo kitapigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la huo muungano. Na hao watu hawatakuwa CHADEMA, watakuwa wanaccm wenyewe.
 
Hajajibu mapigo kama Lisu alivyopiga
 
Kinana amezeeka akili?
Hoja zake tangu achukue cheo kipya zimekuwa hazina muunganiko na zenye kukosa mashiko.
 
Sema pesa ni sabuni aisee..
Huyu jamaa Magufuli alimpausha hadi sauti ikawa haitoki!
Saizi anajikuta mwamba.
Awe na akiba.

Mungu fundi bana...
 
Kuna haja kwa kipindi hiki kuangalia katiba zetu upya

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hairuhusu Rais aliyopo madarakani au kustaafu kushtakiwa kwa kosa lolote lile

Je siku akitokea Mzanzibar akawa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa makusudi ya kulindwa kisheria na kikatiba akawa anatapanya rasilimali za Tanganyika kwa maslahi yake au kwa maslahi ya kikundi fulani kilichopo Zanzibar jiulize nani wa kutetea au kuzilinda mali za Tanganyika?

Zanzibar wana serikali yao inayolinda mali na rasilimali za Zanzibar je Mali za Tanganyika zinalindwa na nani?
 
Kuna haja kwa kipindi hiki kuangalia katiba zetu upya

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hairuhusu Rais aliyopo madarakani au kustaafu kushtakiwa kwa kosa lolote lile

Je siku akitokea Mzanzibar akawa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa makusudi ya kulindwa kisheria na kikatiba akawa anatapanya rasilimali za Tanganyika kwa maslahi yake au kwa maslahi ya kikundi fulani kilichopo Zanzibar jiulize nani wa kutetea au kuzilinda mali za Tanganyika?

Zanzibar wana serikali yao inayolinda mali na rasilimali za Zanzibar je Mali za Tanganyika zinalindwa na nani?
 
Sema pesa ni sabuni aisee..
Huyu jamaa Magufuli alimpausha hadi sauti ikawa haitoki!
Saizi anajikuta mwamba.
Awe na akiba.

Mungu fundi bana...
Mzilankende Alimtia Kwenye Kona Akambana Sana Alinyimwa Pumzi
 
Sheria za Uchaguzi anazozitetea Kinana hizi hapa, hivi huyu Mzee anadhani sisi ni wajinga kiasi gani?

View attachment 2981329

🙆‍♂️🙆‍♂️🤦‍♀️🤦‍♀️


Hapo namba 3. Ongezea wanakuwa ma DED , maofisa ndio wakumwaga kama wote.
 
Mkwe nae Kasema
Mkwe nae akasema Eti kila mara Serikali itakapokuwa ikiajiri watu Basi 21 % otomane na Zanzibar tu 👌 🤔🤔

Watanganyika kazi mnayo 😊

Wakati hiyo Zanzibar ina population ya watu wangapi milioni moja au moja unusu ?
 
Hizi propaganda anazotumia kujibu hoja za Lissu zitaeleweka kwa CCM pekee na wajinga wengine ila haziwezi brainwash Watanzania waelevu na wapenda mabadiliko yanayozingatia utawala wa sheria unaotokana na katiba pamoja na taasisi imara ila sio huu upuuzi tunaoushuhudia sasa nchini. Hivyo Kinana anatakiwa arudie tena speech ya TL na kujibu hoja kwa hoja...... Leo alikuwa anafanya mazingaombwe
 
CCM ukosefu viongozi wenye kuelewa Hali halisi ya watanzania. Mtu kama kinana angea saa nzima kama vile anasimulia Watoto wa chekechea hadith za pwaguna pwaguzi. Suala la katiba watanzania wamelidai kwa zaidi ya miaka 30. Halafu bado unasema mda wake haujafika. Eti tume isimamia uchaguzi kwa uhuru na wa haki kwani kilicho msababisha isisimamie uchaguzi wa mwaka 2020 na miaka yote ya nyuma nini? Hicho kilicho kuwa kinasababisha uchaguzi usiwe huru na wa haki ni nini? Imeondolewa lini na Nani?
 
Kungekuwa na uhuru wa habari waandishi wangemuuliza kuhusu kuhusika kwake kwenye biashara haramu ya ujangili
 
Point mujarabu sana hizi?
 
Mwalimu Nyerere alituasa kuwa makini sana na wanasiasa wanaoutumia dini , kabila na rangi katika kutafuta uongozi. Wanasiasa waliokosa hoja hukimbilia mambo hayo ili kuwahadaa wananchi.
Tundu lissu wa chadema ni mfano Hai wa ambacho alikielezea Mwalimu Nyerere. Watanzania mpuuzeni maana hajui analoongea lina athari gani kwa jamii yetu.
 
Chawa mkubwa wewe, Nyerere ndiye aliasisi tume isiyo huru,matokeo ya Rais yasipingwe mahakamani. Chama chenye kuongozwa Kwa kurithiwa na Watoto wa waasisi.
Nyerere alitaka Mgombea binafsi,nani anayezuia miaka yote hiyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…