Pre GE2025 Kinana: Rais Samia wanayemsema ndio ameleta uhuru uliopo nchini sasa hivi, akisema kuanzia leo hakuna maandamano itakuwa nini?

Pre GE2025 Kinana: Rais Samia wanayemsema ndio ameleta uhuru uliopo nchini sasa hivi, akisema kuanzia leo hakuna maandamano itakuwa nini?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
wenzenu wap ndugu,

asie na absolute power?

ni katika serikali ya kidini au kisiasa ndio hana absolute power 🙄
Absolute power anakuwa nayo mfalme na dictator tu. Katika democracy panakuwa na checks and balances za kuhakikisha kuwa power ya mtawala inakuwa na ukomo. Ndio maana Mwalimu aliita mfumo wetu unatoa Imperial Presidents ambao wakitaka wanaweza kuwa madikteta.

Tanzania Rais alikuwa anateua sio tu wajumbe na watendaji wa Tume bali hata wasimamizi wa Uchaguzi. Ni vigumu mno kuwa na uchaguzi huru katika mazingira hayo. Na kwa vile binadamu wote wana mapungufu yao ndio umuhimu wa kuweka checks and balances kwenye muundo. Teua lakini watathibitishwa na wengine. Na watendaji wa Tume hizi huwa hawateuliwi na Rais.

Amandla...
 
Namsubiri Lissu aje kumuwekabsawa huyu Kinana maana analozungumza haliingii akilini kabisaa 😂😂😂
Bora wangenyamaza tu maana watakuja kupigwa spana zingine za moto
 
Dawa Ya Moto Ni Maji, Sasa CCM Wamekosa Dawa Zaidi Wanafarakana Hadharani Hivi Hivi
 
Tuwasikilize hawa
 

Attachments

  • VID-20240503-WA0011.mp4
    16.7 MB
  • VID-20240504-WA0043.mp4
    1.6 MB
Mzee Kinana nina swali kidogo, hebu tueleze sasa ni VIGEZO gani mlitumia na kwa MUJIBU wa nini,ili JIMBO la Watu elfu tano,litoe MBUNGE?

Swali la Pili,Hauamini kazi iliyofanywa na Tume ya Warioba ambayo ndani yake ilikuwa na wajumbe wa chama chako cha CCM,..Muda gani tena unahitajika?.. gharama za ile tume za Warioba nani atalipa?
 
Kinana ajibu haya maswali:
1. Kwa nini leseni ya Tanzania haitumiki Zanzibar
2. Kwa nini Mtanganyika hawezi kununua ardhi Zanzibar
3. Kwa nini Mtanganyika hawezi kuwa DC Zanzibar
4. Kwa nini Wazanzibar wengi wameajiriwa Wizara ya Afya huku Tanganyika wakati afya siyo suala la Muungano
5. Kwa nini Mtanganyika hawezi kupiga kura Zanzibar
6. Kwa nini Wazanzibar wanakuwa viongozi kwenye masuala yasiyo ya Muungano Tanzania


NB: Wazanzibar wanabinya nafasi za Waislam wa bara kuwa Rais Tanzania maana mara nyingi Rais akitakiwa kuwa Muislam anatokea Zanzibar na akiwa Mkristu anatokea Bara. Hii siyo sawa maana Waislam wa Bara wanakuwa wanabaniwa nafasi ya kuwa Rais. Kati ya Marais watatu Waislam wa Tanzania wawili wametoka Zanzibar. Na JK alikuwa rais kwa sababu Zanzibar ilinyimwa zamu yake la sivyo hatungeweza kuwa na Muislam wa bara RAIS hadi leo
Hii comment yako ni nzuri sana, ungeianzishia thread yake iwe rahisi kila mtu kuisoma
 
Huyu ni CDM?
 

Attachments

  • IMG-20240501-WA0021.jpg
    IMG-20240501-WA0021.jpg
    42.2 KB · Views: 1
Back
Top Bottom