Kinana: Rais wa Tanzania aliyekula kiapo hawezi kufanya jambo ambalo halina maslahi na nchi yake

Huyu nae anaongea nini bwana..?
Mkapa wakati anakula hela za EPA kwenye re election campaign zake hakuwa ameapa kuilinda na kuitetea nchi..?
Wao wakae kimya tu wakati wanakula, that's the better thing wanaweza kufanya at the moment. Nchi yenyewe ni kama haina kiongozi tu saivi.
 
wtf…
Kinana asitufanye Sisi hamnazo
By the way hatukumchagua huyo
 
Watanzania wasiwe na wasiwasi wakatai IGA imeshasainiwa na kupitishwa bungeni, na kujinasua hapo ni mamilioni ya US dollars katika arbitration case kubwa?

What is Kinana talking about? Who is he fooling?
 
Watanzania wanaapa daily
Tunawaona na wakingia kwenye
Sekta wanapiga
Tena wanashika misaafu nq mabiblia

Ova
 
Kinana amesema, Serikali imesema ipatokea kila ushauri na CCM imeitaka Serikali isikilize ushauri, maoni na hoja zinazotolewa. Haya yote yatafanyiwa kazi
Hapa naona sawa, hiki ndiyo tunachotaka sasa, hapa hatuna neno tunasubiri.

Ila siyo zile ngonjera zingine za wapambe wengine, kwamba kila kitu kiko sawa mia kwa mia.
 
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdurhaman Kinana, amezungumzia mjadala wa uwekezaji katika Bandari ya Dar es Salaam huku akiweka wazi kuwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na Serikali anayoingoza haiwezi kuuza bandari hiyo na kuhoji Rais auze bandari kwa maslahi yapi.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Mkendo Musoma Mjini Kinana alianza kwa kueleza kuwa liko jambo la bandari linazungumzwa na mjadala mkubwa, unaendelea kuwa mrefu, mjadala mpana.

“Nataka niwahakikishie msiamini kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyekula kiapo eti atafanya jambo ambalo halina maslahi na nchi. Haiwezi kutokea, Rais ambaye tangu amechukua usukani amefanya mambo mengi mazuri, kwa nini aende kuuza bandari, sababu ni ipi?

“Ili apate nini, ili iweje na ukisikiliza huu mjadala usikilizeni kwa makini na mmeshausikiliza, wote tunaoutetea, wanaopinga pamoja na wanaokosoa hakuna anayesema kwamba kusiwe na uwekezaji hata mmoja kwani wote wanakubali kwamba kuna haja ya kuwekeza na lengo ni moja tu kuongeza ufanisi na kuongeza mapato.
 
Wanasiasa ni shida Sana kwahiyo Prof. wa Sheria ISSA Shivji ni Muongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…