Kinana: Rais wa Tanzania aliyekula kiapo hawezi kufanya jambo ambalo halina maslahi na nchi yake

Labda mumpige breki ndani ya chama. Na ni lazima mtoke hadharani kusema mmeachana na ule mkataba. Kinyume chake ni kuendelea kupoteza imani ya wananchi.
 
Baada ya Uvumi mkubwa wa kumhusisha Kinana na Kupinga uwekezaji wa Bandari Kwa DP World, hatimaye afunguka.

Akihutubia mkutano wa hadhara Mkoani Mara Kinana amesema Watanzania wasiwe na Wasiwasi Kwa sababu Rais Samia ameapa kulinda na kuhifadhi Katiba ya Nchi hivyo hawezi kuwauza Kwa kufanya jambo ambalo Halima maslahi Kwa Nchi.

My Take
Hakuna wa kurudisha Wala kukwamisha uwekezaji bandarini

=======
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)-Bara, Abdulrahman Kinana amewataka Watanzania kutokuwa na wasiwasi juu ya mkataba wa ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania na ya Dubai kwani Rais Samia Suluhu Hassan, ameapa kuilinda na kuitetea Katiba kwa maslahi yao.

Kinana amesema hayo leo Jumatano, Julai 26, 2023 wakati akihutibia mkutano wa hadhara, Musoma Mjini, Mkoa wa Mara akiwa kwenye mwendelezo wa ziara zake katika mikoa ya Dodoma, Manyara, Mara, Simiyu na Tabora.

“Kuna mjadala mkuuuuubwa na mpana wa bandari, mjadala huu umefika wakati unawachanganya Watanzania. Wamuamini nani. Nataka niwahakikishie, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyekula kiapo hawezi kufanya jambo ambalo halina maslahi na nchi yake.

“Kama Rais tangu achukue nchi (Machi 19, 2021), amefanya yote haya, kwa nini auze nchi, ili iweje? lakini mkisikiliza mjadala, wote wanaotetea, wanaoupinga, wanaoukosoa hakuna anayesema tusifanye uwekezaji, hata mmoja, wote wanakubali kuna haja ya kuwekeza ili kuongeza ufanisi na kuongeza mapato,” amesema Kinana

Kinana amesema, Serikali imesema ipatokea kila ushauri na CCM imeitaka Serikali isikilize ushauri, maoni na hoja zinazotolewa. Haya yote yatafanyiwa kazi. Haiwezekani rais akapuuza yote haya na mmemuona Rais tangu mjadala umeanza, amekaa kimya, anapigwa vita.

“Kamanda mzuri wa vita si yule vita inapokuwa hivi anabadili mbinu na mikakati, kamanda mzuri ni yule anayetulia. Nahodha mzuri wa chambo si yule anayeyumbishwa bali anatulia na kuona anakabiliana nayo viti,” amesema Kinana.

Kiapo cha majizi ya kura kina maana gani? Siku hizi kiapo ni kukamilisha formalities tu, hakuna anayetekeleza wala kujali kiapo.
 
Ukisikia undumila kuwili ndio huu, hawa hawa si ndio waliokuwa wanamsakama mwendazake je mwendazake hakuwa raisi wa nchi? tunapokuwa waongo basi tusiwe wasahalifu.
 
mzee ni bola angekaa kimya Kama hakuwa na la kusema , kuliko kulopoka kiasi hiki!! wenzetu wazungu kadri umri unapokuwa mkubwa na kiwango Cha hekima kinaongezeka , lakini huku kwetu kadri unapozeeka una approach to mental health problem!!

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Tutawatoa makamasi .hatuishii hapa ,tuyahakijisha tukimaliza bandari tunahamia ngorongiro na mkataba wa gas tunautaka hapa
 
“Kama Rais tangu achukue nchi (Machi 19, 2021), amefanya yote haya, kwa nini auze nchi, ili iweje? lakini mkisikiliza mjadala, wote wanaotetea, wanaoupinga, wanaoukosoa hakuna anayesema tusifanye uwekezaji, hata mmoja, wote wanakubali kuna haja ya kuwekeza ili kuongeza ufanisi na kuongeza mapato,” amesema Kinana
Kipande hiki kinanipa taarifa nyingi tu kichwa. Nilitegemea aseme Rais HAJAUZA. Ila naye anaweka viulizo tu, anakubali ukosoaji....ah, isije kuwa ni codes kuwa inatosha sasa, tupate mwingine.
... Sijui ni mawazo ya night haya..!
 
OIG (2).jpeg
 
Hawezi vipi hata hajui au haelewi kilichomo kwenye mkataba?

Kwani Mangungo aliuza eneo lake kwa kutaka, si hakujua/kuelewa alichoelezwa!
 
Badala ya kuzungumzia yaliyomo katika mkataba anatuletea blaa blaa hapa.
 
Labda mumpige breki ndani ya chama. Na ni lazima mtoke hadharani kusema mmeachana na ule mkataba. Kinyume chake ni kuendelea kupoteza imani ya wananchi.
Hata sijui kama hawa viongozi wa CCM wanayasema haya wakiamini kwamba waTanzania watabadili mawazo kwa yale ambayo wamekwishayaona kwenye mkataba.

Mtu umekwishajua matatizo yaliyomo ndani ya mkataba, halafu Kinana ajitokeze na kauli dhaifu kama hii, huyo mtu abadili mawazo kwa alichokwisha kielewa kuwa ni mkataba mbovu?
 
Kumbe yeye ndio kasema Bandari imeuzwa?
Yeye kasema yaliyomo kwenye mkataba hayafai, ikiwemo na masharti yanayofanana na huko kuuza.
Kwa hiyo wewe hapo unadhani Profesa kausifia mkataba kuwa mzuri kwa Tanzania?
 
Kinana ana umri gani?
Wasira ana umri gani?
CCM hakuna vijana wa kuchukua nafasi za hawa ambao walishalitumikia taifa?
 
Yawezekana ni kweli lakini pia Raisi hawezi jua Mambo yote so kunauwezekani wa kukosea. Akiwa anashauriwa jambo basi asikilize huenda ashakosea
 
Back
Top Bottom