Kingunge: Bila tume huru, wapinzani wasahau kuingia Ikulu

Kingunge: Bila tume huru, wapinzani wasahau kuingia Ikulu

Wasalaam kumekuwepo tetesi na maneno lukuki kuhusu mh membe, napenda kuweka wazi hapa kwa tume hii ya uchaguzi ambayo inawajibika kwa mwenyekiti wa ccm hata akishuka malaika kutoka mbinguni kugombea aidha urais au ubunge bado ccm itashinda kwa kishindo kikuu. Muundo wa tume kwa asilimia mia moja imejaa makada watiifu wa ccm, na maelekezo walishapata kwamba wasije mtangaza mpinzani kashinda.( hata kama kashinda kweli)

Kuelekea uchaguzi mkuu 2020 hakika nawaambia kwa tume hii ya uchaguzi hakutakua na mbunge hata mmoja kutoka vyama vya upinzani atakaeshinda kiti cha ubunge. Waswahili wanasema dalili ya mvua ni mawingu na mawingu yameshatanda mwenye macho anaona, hakuna chama cha siasa kitachotoa mbunge wala diwani mwaka 2020. Anaebisha ni haki yake abishe tu ila 2019/2020 hakutakua hata na mwenyekiti wa serikali za mitaa atakaetangazwa kushinda uchaguzi hata km ameshinda kweli.

Mungu ibariki Tanganyika.
 
hii tume hata mimi nikigombea urais kupitia ccm nashinda asubuhi tu. tume hii rais kwa mamlaka yake aweza kumwondoa mwenyekiti wa tume hata leo kesho uchaguzi
 
...kwa tume hii ya uchaguzi ambayo inawajibika kwa mwenyekiti wa ccm hata akishuka malaika kutoka mbinguni kugombea aidha urais au ubunge bado ccm itashinda kwa kishindo kikuu. ....ila 2019/2020 hakutakua hata na mwenyekiti wa serikali za mitaa atakaetangazwa kushinda uchaguzi hata km ameshinda kweli.

Mungu ibariki Tanganyika.
duh!
 
...kwa tume hii ya uchaguzi ambayo inawajibika kwa mwenyekiti wa ccm hata akishuka malaika kutoka mbinguni kugombea aidha urais au ubunge bado ccm itashinda kwa kishindo kikuu. ....ila 2019/2020 hakutakua hata na mwenyekiti wa serikali za mitaa atakaetangazwa kushinda uchaguzi hata km ameshinda kweli.

Mungu ibariki Tanganyika.
Mkuu, unashauri nini sasa, kama wananchi wakitaka haki itendeke na kura zao ziheshimiwe, wafanye nini???
 
Mkuu, unashauri nini sasa, kama wananchi wakitaka haki itendeke na kura zao ziheshimiwe, wafanye nini???
Utafanyaje mbele ya police? Hapa ni kumwachia mwenyezi mungu; ww fikiria msimamizi wa uchaguzi anaambiwa, nimekupa gari, nakulipa mshahara ole wako umtangaze mpinzani kashinda.( hebu tafakari kauli hii)
 
Nina waambia Ukweli si tume tu ila hakuna chama cha upinzani chenye mizizi mpaka chini kwenye uhakika wa kura. CCM mizizi yake mirefu na CCM inapoenda kwenye uchaguzi inakuwa tayari ina uhakika na wapiga kura wake wangapi ambao wataenda kupiga kura hasa wanachama wake wanawasimamia ipasavyo wakapige kura.

Mwaka 2015 wakati Jaji Lubuva akitangazo matokeo nilikuwa naandika kwenye excel yangu hasa ya watu wawili ambao walipeana upinzzani wa kutosha, niliandika mwanzo mwisho alafu nikawa nakuja natoa ile fomu ambayo tume wakiitoa kupitia kwenye website yao ya matokeo kwa kila jimbo mwisho nikavitunza vyote nilichokuja kugundua ni mijini tu Ukawa iliishinda CCM hasa mikoa ya Arusha, Mara, Dsm na Mtwara na Kilimanjaro pamoja na Zanzibar, Huku Lowasa alipiga mbali sana Magufuli lakini kinyume na mikoa hiyo Magufuli alimpita Lowasa pakutosha sana.

Nilitunza yale matokeo nia ili nije nione kama wapinzani watakuja kutoka na fomu ambayo ilibatilishwa matokeo yake lakini hiko kitu hakikuwai kutokea hapo niliamini kuwa Magufuli alishinda kihalali.

Narudia tena kwa upinzani wa Tanzania hawana uhakika na kura zao, wanategemea sana ushabiki tu ndio wawapatie kura wakati CCM wanaanza kwa wanachama wao kisha ndipo wanakuja kuangalia washabiki.
 
Nina waambia Ukweli si tume tu ila hakuna chama cha upinzani chenye mizizi mpaka chini kwenye uhakika wa kura. CCM mizizi yake mirefu na CCM inapoenda kwenye uchaguzi inakuwa tayari ina uhakika na wapiga kura wake wangapi ambao wataenda kupiga kura hasa wanachama wake wanawasimamia ipasavyo wakapige kura......
Mmmmhh... Kama ni hvyo mbona wanazuia mawakala wa upinzani kuingia kushuhudia upigaji kura ili waingize kura zao feki? Kwa nn wasiache upigaji kura uwe wazi, huru na haki? Kwa nn wanakuwa na vituo HEWA vya kura?
 
Kuna dalili kama issue ya Tume Huru ya uchaguzi vyama vya upinzani wanataka kuiweka pembeni na kuzungumzia petty issues kama ongezeko la vituo na blabla kibao.

Nadhani sasa tuwaambie vyama vya upinzani kwa pamoja kuwa tumechoka na nyimbo, mamalamiko na kususiana kusiko na mwisho tunataka Tume huru tuu, maana hiyo ikiwepo mambo hayo ya vituo na mengine hayatakuwepo!

Sasa mheshimiwa Mbowe, Zitto, Maalimu, Mbatia, Lissu, Dovutwa nk achaneni na mengine piganieni Tume huru la sivyo bora na nyie tuwasusie tuiache nchi iliwe tuu na wachache hao ccm labda mpaka itakapotokea kizazi kingine kikaamua kutumia njia nyingine ya kuwaondoa.

Vikao vianze kwa makatibu wakuu wa vyama, iundwe secretariate ya kupanga mkakati kisha viongozi wakuu mkishirikisha asasi za haki za binadamu kulipigania hilo kwa pamoja.

Hivi hao viongozi nilio wataja hapo juu wakifikia mahali wameitisha press kwa pamoja au mkutano mkubwa wa hadhara pamoja mnadhani nini itakuwa repercussion yake kwa serikali, CCM na hata jumuia ya kimataifa?

Inaonekana propaganda ya CCM kuwa wengine hawarudi bungeni imewachanganya sana mpaka mnaona wao ndio wapiga kura!

Tume huru ikiwapo wabunge wazuri wa CCM watarudi na wazuri wa upinzani wataingia na ikiwezekana utawala unaotakiwa na sisi wananchi ukaingia madarakani.

Sasa ni eitha Tume huru au na nyie tuwasusie basi!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anzeni tu kujikanganya, mkipata kura tano msiseme mmeibiwa
Suala la tume mlitakiwa mlianze mara bada ya uchaguzi wa 2015.
Mnakurupuka leo na kujazana ujinga wa kususa,nyie suseni tu,sie ccm tunaingia uchaguzini 100 kwa 100
 
Anzeni tu kujikanganya,mkipata kura tano msiseme mmeibiwa
Suala la tume mlitakiwa mlianze mara bada ya uchaguzi wa 2015.
Mnakurupuka leo na kujazana ujinga wa kususa,nyie suseni tu,sie ccm tunaingia uchaguzini 100 kwa 100
Suala la Tume huru halihitaji muda mrefu kama kulea mimba, ni suala la muda mchache tuu.
Viongozi hao waliotajwa wakiamuwa kushirikiana kulipambania ni kufumba na kufumbua tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wale wasiofahamu wanafikiri kudai tume huru ya uchaguzi au kudai katiba mpya ni hoja za wapinzani. Wapo ambao hawajatambua kuwa katiba mpya iliyonzuri inamugusa kila mtanzania kama sio leo kesho yaweza kukugusa.Wanakaa kimya wasijekuvurugiwa masirai yao
 
Back
Top Bottom