Kipigo cha Polisi, Halima Mdee apima na kukuta kavunjwa mkono wake wa kulia

Kipigo cha Polisi, Halima Mdee apima na kukuta kavunjwa mkono wake wa kulia

Huo mkono ulitakiwa kukatika kabisa ,nasikitika umeishia kuvunjika tu,ninahuzuni sana
Kwa akili kama hizi ungesema kinyume na ulivyosema ningekushangaa
1571388928689.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
#Updates #Kutoka_Hospital

Taarifa halisi kutoka hospitali ya agha khan.

Vipimo vya saa 10:00 alfajiri vinaonyesha kuwa Mh #Halima_Mdee amevunjwa mkono wake wa kulia na ana maumivu makali sana[emoji24][emoji24]
Kunapokua na fujo popote unaweza kupigwa na pia yeyote anaweza kupigwa awe Askari au mfanyafujo mwenyewe,muhimu ni kujiepusha kufanya fujo hasa maeneo nyeti. Kiki za kisiasa zataua watu kazi kwao.

macson
 
Kuna harakati za kupigania,wamejitakia wenyewe wangevunjwa hata miguu kiboya boya,alafu utasikia ukiukwaji was haki za binadamu.
 
Wakija watasema walitumia ‘nguvu za kadri’ ndio mpaka kuvunjana mikono au kupasuana vichwa kweli.

Mbona polepole alipomfuata Mashinji na wapambe atukuona polisi nje ya jela.

Shame on the police force
 
Kiherehere gani kilimpeleka huko yeye na mpenzi wake wakati walishatoka? au siku moja tuu kukaa ndani walishazoea jela? sehemu tatu ambazo hazina mazoea ni mahakama, jela na hospitali... hivi inakuja akilini kweli geti la magereza limefungwa wewe unalazimisha kupita kwa nguvu? au walitaka kuwatorosha wafungwa waliokuwepo ndani?
 
Ki Halima kina asili ya ukiherehere, yaani unakuta waliambiwa muondoke wao wakajifanya wanaenda kuwashawishi wajeda kitu ambacho jeshi huwa lina amri tu. Mwache akome ajifunze huyu bidada, na hapo wamfugulie mashitaka afungwe tena mbuyuyu mkubwa
Hata shetan anawafuasi
 
Hao polisi walitii maagizo ya kipumbavu, yaliyotoka kwa viongozi wapumbavu.
Kukusanyika nje ya gereza kuna uvunjifu wa sheria ipi???

Ama ni kwa sababu wapumbavu flani kwa upumbavu wao, walimlipia mtu faini kipumbavu na kupigwa chenga ya mwili???

Baada ya kukosa kusifiwa wakafura kwa hasira na kutoa amri za kipuuzi kwa mapolisi wapumbavu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
#Updates #Kutoka_Hospital

Taarifa halisi kutoka hospitali ya agha khan.

Vipimo vya saa 10:00 alfajiri vinaonyesha kuwa Mh #Halima_Mdee amevunjwa mkono wake wa kulia na ana maumivu makali sana😭😭
Na bado mtachapwa sana, maana mnajifanya watukutu
Hao siyo polisi ni magereza
 
bado kuna jitu lina praise hii Sirikali ya fisiemi, Me nasem Fisiem Waendelee Tuu
Kuna watu wapo kando wanawatch Siku wakifanya yao tusishangaee
 
Kila tunapodhani hali ya uonevu imezidi kikomo, kesho yake tunakuta hali ni mbaya kuliko ilivyokuwa jana yake.

Inaumiza kichwa tunapowaza hatma ya huu uonevu wa kutumia polisi.

Wananchi wamekuwa waoga mno, wanaogopa kupigwa au hata kupotezwa na vyombo vya dola. It's a well founded fear.

Nilidhani angalau viongozi wakuu wastaafu wangeweza kukemea huu ukatili wa dola kwa wananchi, lakini naanza kuamini hata wao wameogopa. Wameogopa sana, la sivyo wangekemea kwa nguvu.

Maaskofu na mashehe wameogopa pia au imekuwaje? Kuchunguzwa uraia au kupimwa mkojo kumewaogopesha?

Inasikitisha sana polisi wanapowapiga raia, hasa wanapowapiga kina mama. Polisi kumpiga Mbunge, tena mwanamke, limekuwa jambo la kawaida Tanzania?

Mungu anawaoneni nyie viongozi dhalimu wa CCM.

Siku zinavyozidi kupita ndivyo uonevu unazidi kukua. Yule kijana aliyesikika akisema "Rais kitu gani" ana bahati alifungwa miezi sita tu. Ingekuwa ni sasa sijui hata kama tungemsikia.

Rais Magufuli angependa Chadema kiwe underground movement? His government is driving the opposition out of the open political space. And it's using brute force to do so.

Tufanyeje sisi wananchi wa kawaida, wasio na vyama? Maana tunaudhiwa sana na hivi vitendo vya ukandamizi. Ukandamizi wa kiwango cha kishetani!
 
Ulikuwa ni unyama au ndio walikuwa wanatimiza wajibu wao wakiwa kazini? Kwani ilikuwaje hadi wakavunjwa mikono, mndee si alitoka juzi? Alirudishwa jela tena? Au ni kiherehere chake?
Kulikuwa na sababu yoyote ya kumvunja mkono? I mean, well, hata kama hiyo sababu ipo, kulikuwa na ulazima wa kumvunja mkono?

Cc GODZILLA
 
Kulikuwa na sababu yoyote ya kumvunja mkono? I mean, well, hata kama hiyo sababu ipo, kulikuwa na ulazima wa kumvunja mkono?

Hili genge linalojiita polisi halina nidhamu kabisa! They are very indisciplined!

Hivi huwa hawana miongozo na miiko ya kazi? Si kuna PGO? Lakini pia kuna mamlaka za nidhamu zinazowatizama?

Kwani ukiwa polisi ghafla tu unageuka kuwa mvuta bangi?

Una uhakika walikuwa Polisi?
 
Back
Top Bottom