Registered_jf
JF-Expert Member
- Nov 27, 2024
- 1,237
- 2,110
1) Kulelewa na wazazi wakristo sio kuwa Mkristo. Kuwa Mkristo ni kukutana na Kristo kibinafsi.
Ni kama ulikuwa unasikia story za mjomba kwa miaka, hatimaye akaja nyumbani.
2) Nilipoteza imani nikiwa form 3, tena kwasababu ya kusoma posts za humu JF!
Ndomana mzungu alisema: Little knowledge is a dangerous thing.
3) Mwanzoni na mimi nikawa kwenye kempu ya wakana MUNGU, kama vile kufuata mkumbo tu, kuhisi unafanya jambo flani la maana la kishujaa sana kuwaambia watu kuwa hakuna MUNGU.
Unajikuta muokozi: unaona kama waamini Mungu wanateseka sana kufuata sheria za Mungu wakati wangejua hakuna Mungu wangefanya chochote wanachotaka wa enjoy life, si unajua we only live once?
Wanateseka kufuata desturi zisizo na maana kama vile kujichosha kwenda kanisani asubuhi wakati muda huo wangelala! ! !
Yani unajikuta una akili sana kuwa: kati ya mabilioni wote kwenye historia, wewe ni kati ya wachache umetambua ukweli uliofichwa, ambao kuna watu fulani huko hawataki uujue.
Au ni kati ya wachache waliowahi kuutambua, si unajua tumetokana na sokwe? Kwahiyo ni process mdogomdogo kutambua kuwa hakuna Mungu, na kuachana na imani za kisokwe sokwe.
Eti MUNGU kajifunua kupitia uumbaji, kitabu chake na kupitia YESU:
Huu ukweli ulio wazi hivi haiwezekani kuwa ndio ukweli:
kwanza watu wengi wanaukubali, tena watu wa ajabu ajabu hawajasoma, maskini.
Halafu ni mwepesi mwepesi sana, Ukweli utakuwa mgumu mgumu wa kujulikana na wasomi.
Halafu ni habari za muda mreeefu zimeboa zimepitwa na wakati, sasa hivi kila kitu kinabadilika, lazima tuwe habari mupya mupya zitutoe kwenye line zitusisimue zitushughulishe tusogoe tubishane tupigane..
4) Baadaye nikachoka mimi kinyozi wa mwandambo na hawa Waamini MUNGU wasio na akili nikabadilika:
kwanza kila kitu hakina maana, so what kama watu wameamua kujitungia mtu wa kufikirika kisha wajihangaishe naye hadi wanakufa?
Kwanini ni muhimu kwangu kubadilisha mawazo yao? ?
Mwishowe tunapotea tu into nothing, Kwanini napoteza nguvu kukaa kubishana na nothing?
Kwanini hii miaka 80 ya kuishi ni ya muhimu sana mimi kujihangaisha na chochote kile, achana hata na imani kwanini nifanye kazi? Kwanini uhai ni muhimu kiasi nijisumbue kuulinda au kuutetea? Kila kitu mwisho wake ni nothing.
Nikawa apathetic: zero interest zero concern. Nikaachana na habari za imani na dini.
Nikiona watu wanabishania imani wote waamini na wasioamini nawaona wendawazimu tu.
Nikiona watu wanahangaika kwenda kanisani kila siku kuhubiri huko barabarani naona kazi bure, hawana kazi za kufanya!
Nikawa tu occupied na maisha ya shule na nyumbani. Bado nilikuwa mdogo so bado nilikuwa nina hamu na maisha yajayo.
4) Kuingia chuo nikakutana na wale wanawahi kula maembe mabichi na chumvi wakati nyie mnasubiri yaive, akani introduce kwenye imani flani za huko Mashariki ya mbali.
Akawa ananiambia habari za Ufahamu ulio mkuu zaidi. The Supreme consciousness. Nilikuwa interested kwasababu zilikuwa taarifa mpya kwangu lakini sikuamini.
5) Baadae nikaja kupigwa na kitu kizito, nikakuguswa na waya mwekundu.
Nikajiuliza hivi wewe Mungu upo kweli?
How could you let this Great injustice fall upon me? ? This great violation of my human rights! !
Me a poor innocent helpless soul who wouldn't hurt a fly!
Ona nilishaamua Mungu hayupo lakini ghafla nikamkumbuka tena namlaumu huko huko aliko ambapo hata hayupo! ! !
Hii nguvu kuu ni nguvu gani hainisaidii? Huu Ufahamu mkuu kwanini haukunifahamisha mapema?
Hivi maisha ndo haya tu? Zaliwa, fanya kazi, teseka, kufa? ?
6) Wakati huo nilipata nafasi ya kukaa tu nyumbani muda mrefu: sisomi, sifanyi kazi yoyote, sitoki kwenda kokote. Watu wakija kuniona sitoki kuwaona.
Sanasana nilikuja kununua vifaranga, nikawa nashinda na vifaranga! !
7) Nikaanza kuwa interested, nikatafuta habari za ile Supreme Consciousness.
Nikawasoma wabudha, wahindu, nimewasikiliza ma Guru weee, rafiki yangu yule alikuwa anapost sana videos za Sadhguru, ndo nikaanzia kwake.
8) Ikafika point officially nilisadiki kuwa kuna Ufahamu Mkuu zaidi.
Niliona lazima kuna kitu beyond ulimwengu huu (space, time and matter).
9) Huko ndo mawazo / ufahamu wa watu hutokea. Ufahamu wetu ni zaidi ya kazi ya ubongo.
- Ndomaana kuna watu sehemu muhimu za ubongo zilitolewa ili kuwatibu lakini bado wali function kawaida.
- Kuna watu ingawa sehemu ya kushoto na kulia ya ubongo ilibidi zitenganishwe, bado wali function kama kawaida. Unaweza kukata komputa yako katikati ikaendelea kufanya kazi?
- Kuna watu ingawa walikuwa wamelala muda mrefu hawajitambui, walivyoamka walisema yaliyotokea wakati wamelala.
Huyu Neurosurgeon anaelezea hayo:
View: https://youtu.be/41bIJ7hYbLs?si=3m7w0NO4TuXHKFf9
10) Nikajua kutoka huko ndo kina Isaac Newton walipopokea ufunuo wa mambo waliyogundua.
11) Nikajua kama hakuna kingine zaidi ya ulimwengu huu ambamo kila kitu kinabadilika / kinaoza, hatuwezi kujua ukweli kamwe: either kila kitu ni kweli au kila kitu ni uongo.
Kwanini? Kwasababu Tunakosa msingi wa kuamua ukweli ni upi.
Na binadamu tulivyo tunataka kujua ukweli, tunataka kuelewa, tunataka sense / maana.
Hata sababu binadamu tunaweza kujadiliana ni kuwa kuna misingi ya maana tunaifuata. Otherwise ingekuwa kama kwenye mnara wa babeli.
12) Hiyo misingi ya maana imetoka wapi?
Kuna ulimwengu mwingine nje ya huu: ulimwengu wa milele, ambao haubadiliki wala kuoza, ulimwengu wenye Ufahamu Mkuu ambao uko connected na huu.
Huko ndio chanzo / msingi cha ukweli / ufahamu / maana.
Huo ulimwengu ndio mstari ulionyooka tunaotumia kupimia mistari mingine kama imepinda.
Ndio huko tunatoa sheria za mantiki.
Ndio huko tunatoa Hesabu, ulimwengu uko chini ya sheria zake.
Ndio huko tunatoa sheria za milele maadili mfano:kuua mtu asiye na hatia ni kosa. Binadamu ana haki ya kuishi. Binadamu ana haki ya uhuru.
13) Otherwise hakuna kwenye haki ya kusema ni kosa kuua mtu asiye na hatia. Ni kosa kwa misingi ipi? Kisa katiba hizi walizotunga binadamu? ? Nani kawapa hao binadamu mamlaka ya kuniamulia kipi kizuri kipi kibaya? ?
Ni kundi la watu wachache tu wanaotaka kuninyanyapaa na kuniamulia kwa nguvu jinsi ya kuishi! ! !
Hata mkiwa bilioni 7 mmekubaliana, mimi niko peke yangu nakataa, nani aliyeamua kuwa mna haki ya kutunga sheria hii juu yangu? ?Mnatumia mabavu?
Watasema oooh ni kwa ajili ya kuendeleza maisha inabidi tuweke sheria tusimalizane otherwise maisha yatapotea ulimwenguni: ni nani kasema kwamba uhai una thamani? Tuulinde kwa nguvu zote? Mimi nasema hauna thamani, sio tu tuue vichanga tumboni nikipata nyuklia namaliza wote, kuna tatizo hapo? Nani kasema? Je huu si muendelezo wa unyanyapaa kwangu kuishi navyotaka kwenye ulimwengu huu niliojipata?
Watasema oohh wewe fanya unavyotaka usiingilie uhuru wa mtu: ni nani kasema ni vibaya kumnyima mtu uhuru? Ni hizi katiba zenu mlizojitungia? Huu ni muendelezo wa matumizi ya mabavu na unyanyapaa kwangu nayetaka kukufanya mtumwa mwangu, sikulipi na nitakutesa!
Sheria za milele za maadili zipo, hata wasiomuamini MUNGU dhamiri zao zinashuhudia sheria hizi.
14) Na huko zilikotoka ni nje ya ulimwemgu huu! Nje ya time, space and matter!
Utataka upaone kwa macho wakati macho ni limit ya matter.
Utasema mbona hawajapaona kwa miaka 6000 sasa, lakini miaka 6000 ni limit ya time.
Utataka upachunguze na vifaa ambavyo viko limited na space.
Tunahitaji kupita mambo hayo, ndomana tunatumia Ufahamu, unaopita yote hayo kwasababu ndio uko connected na huo ulimwengu.
Ndo inapokuja IMANI:
Unaona bila macho.
Unakipata kabla hakijafika.
Unauishi wakati ulimwenguni hakionekani.
Kwa kutumia Ufahamu!
Kuona mtu ana furaha wakati ana matatizo / anateswa sio ajabu, huyo amepita mipaka ya Ulimwengu.
15) Kwa logic za bei rahisi: Maumivu = huzuni.
Kwa Ufahamu uliopita ulimwengu huu: Maumivu = Shangwe.
Kwa logic ya bei rahisi: Kifo = Kupoteza / kupungua
Kwa Ufahamu uliopita ulimwengu huu: Kifo = Kupata / kuongezeka.
Kwa logic za bei rahisi: Miaka 6000 = Muda mreefu
Kwa Ufahamu uliopita ulimwengu huu Miaka 6000 = Ni nukta
Piga hesabu.
16) Na hili sio swala la kumkalisha mtu kumshurutisha, kumshawishi, ku dejadiliana kila siku.
Ni swala binafsi kabisa, la moyo na ufahamu wa mtu.
Hata hoja bora zaidi duniani haiwezi kuukamata moyo, otherwise watu wangejifunza tu kutengeneza hoja nzuri wawapate wapenzi wa maisha yao.
Lakini kama mtu hakupendi hakuendi tu jamani.
17) Ndomaana ule Ufahamu Mkuu, ambaye ndio Upendo wenyewe:
ametupa wote muda na uhuru tufanye tunavyotaka humu ulimwenguni,
ametupa muda na uhuru tujifunze mema na mabaya,
ametupa muda na uhuru tumjue na tumchague kwa hiari,
ametupa haki ya kuja kuishi na kufurahi milele pamoja na makosa yote tuliyofanya kwasababu ameyalipia yeye mwenyewe,
ametupa uhuru wa kumkataa.
18) Na wote watakaomkataa naye atawakataa. Watatambua kuwa wamekataliwa, ndomaana tunaambiwa watalia na kusaga meno! Maumivu ya kukataliwa na ule Ufahamu Mkuu.
Na mwishowe, mapenzi yao yatatimizwa, nao watarudi into nothing (mauti wa pili).
"Hapo mfalme akawaambia watumishi, ‘Mfungeni miguu na mikono mkamtupe nje gizani; huko atalia na kusaga meno.”
Mathayo.22.13.BHN
"Lakini wale ambao ufalme huo ni wao watatupwa nje, gizani, ambako watalia na kusaga meno.”
Mathayo.8.12.BHN
"Lakini waoga, wasioamini, wachafu, wauaji, wazinzi, wachawi, waabudu sanamu, pamoja na waongo wote, mahali pao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.”
Ufunuo.21.8.NENO
"Kisha mauti na Kuzimu zikatupwa katika ziwa la moto. Hii ndio mauti ya pili, yaani hilo ziwa la moto."
Ufunuo.20.14.NENO