Kipindi siamini MUNGU, sikuwa na muda na imani za watu

Kipindi siamini MUNGU, sikuwa na muda na imani za watu

Hakukuwahi kuwa na mtu aliyeitwa Yesu kwenye historia ya ulimwengu huu. Huyo anaeitwa Yesu ni "Character wa kutungwa alliyewekwa kwenye script inayoitwa agano jipya"
BAAAAS, naku cancel rasmi:

Kudai Yesu ni Character ya kutungwa kunaonyesha kushindwa kabisa kufanya utafiti wa msingi kabisa wa kihistoria. EPIC FAIL.

YESU wa Nazareti ni miongoni mwa watu waliyothibitishwa kwa uhakika zaidi kwenye historia.

Ukikataa kuwa YESU aliishi, itabidi utupe a very big chunk of ancient history, utakuwa umetingisha historia nzima ya ulimwengu maana kuna watu maarufu kwenye historia ambao uthibitisho wa uwepo wao haufikii hata robo wa uthibtisho wa maisha ya YESU:


View: https://youtu.be/F5gBPcWxvN8?si=YyKGbHM7IfE85vq1


Kwangu mtu anayekataa kuwa YESU aliishi karne ya kwanza anaonyesha uvivu wa kufikiri na ukosefu wa fikra za kina.

Hiyo ni litmus test kwangu.

Kama mtu hawezi kuchukua muda kuthibitisha jambo lililo wazi na lililorekodiwa vema kabisa kama maisha ya YESU, siwezi kuchukulia kwa uzito chochote kingine utakachosema.

Nitakuacha na huyu mtaalam wa Crime Forensics, J. Warner Wallace, aliyetumia utaalam wake kuthibitisha kama kweli YESU aliishi, alikufa na kufufuka, ndipo akawa Mkristo.


View: https://youtu.be/ajOYym3IuRk?si=RnetGYz_CLMIy69_

BYE
 
Kwa nini watu wenye dini bado wanaua watu, wanafanya mauaji ya kimbari na halaiki?
Kwanza:

Je unaamini kuwa Mwanamume aitwaye YESU Mnazareti:

aliishi
karne ya kwanza,

alifanya miujiza ikiwemo:
kufufua wafu,
kuponya vipofu,
kuponya viwete,
kuponya magonjwa yasiyotibika,
alilisha maelfu kwa sahani chache za chakula,
aligeuza maji kuwa divai,
alitembea juu ya maji,
alituliza dhoruba,
 Alipaa angani,

aliteswa na waliokataa kuwa yeye ni yule asemaye: Mwana wa MUNGU,

aliuawa,

alifufuka siku ya 3,

kwa siku 40 baada ya kufufuka alionekana na maelfu.

Wafuasi wake wengi waliuawa kwa kutoa ushuhuda kuwa YESU amefufuka!

Kabla hata hajazaliwa yalishaandikwa matukio zaidi ya 300 ambayo angefanya maishani mwake naye kweli alifanya yote.?
 
Hivi tujiulize kwanini huyo Mungu wenu hana uwezo ws kujifunua wala kujieleza kwa watu zaidi ya kutegemea wafia dini kutumia vitabu vya karne na karne kueleza uwepo wa huyo Mungu?.

Alafu ni Mungu yupi huwa mnamzungumzia maana kuna Miungu wengi maelfu kwa maelfu, unaposema Mungu yupo unatakiwa ujibu ni yupi maana kila dini ina Mungu wake anayepingana na dini nyingine, na wote hawa wanadai wanazo Mbingu za kuwapeleka wanaomuamini pia jehanamu kwa wasio muamini, vipi jamani kutakuwa na Mbingu+jehanamu ngapi kwa kila Dini zote duniani?😂😂😂😂.

Michezo hii
 
Hivi tujiulize kwanini huyo Mungu wenu hana uwezo ws kujifunua wala kujieleza kwa watu zaidi ya kutegemea wafia dini kutumia vitabu vya karne na karne kueleza uwepo wa huyo Mungu?.
Unampangia namna ya kujifunua kwako? WHO ARE YOU?

Mara ya mwisho umeongea na rais ni lini? Na tangu umezaliwa umeongea na rais mara ngapi (assuming hauna cheo chochote huko serikalini)?

Ndo hivyo amekuandikia yote kwenye kitabu usome (Biblia) na katuma vijakazi wake, yeye utamuona kwa wakati wake au unaweza usimuone kabisa, utajipata umetupwa gizani
:2Head:

We're talking about the KING OF KINGS here, show some respect.
 
Alafu ni Mungu yupi huwa mnamzungumzia maana kuna Miungu wengi maelfu kwa maelfu, unaposema Mungu yupo unatakiwa ujibu ni yupi maana kila dini ina Mungu wake
TRUE.

Kama umesoma vizuri nimemtaja humo kati.

Ni MUNGU WA ISRAELI, mwenye Mwana mzaliwa pekee aitwaye YESU ndo namuongelea.
 
BAAAAS, naku cancel rasmi:

Kudai Yesu ni Character ya kutungwa kunaonyesha kushindwa kabisa kufanya utafiti wa msingi kabisa wa kihistoria. EPIC FAIL.

YESU wa Nazareti ni miongoni mwa watu waliyothibitishwa kwa uhakika zaidi kwenye historia.

Ukikataa kuwa YESU aliishi, itabidi utupe a very big chunk of ancient history, utakuwa umetingisha historia nzima ya ulimwengu maana kuna watu maarufu kwenye historia ambao uthibitisho wa uwepo wao haufikii hata robo wa uthibtisho wa maisha ya YESU:


View: https://youtu.be/F5gBPcWxvN8?si=YyKGbHM7IfE85vq1


Kwangu mtu anayekataa kuwa YESU aliishi karne ya kwanza anaonyesha uvivu wa kufikiri na ukosefu wa fikra za kina.

Hiyo ni litmus test kwangu.

Kama mtu hawezi kuchukua muda kuthibitisha jambo lililo wazi na lililorekodiwa vema kabisa kama maisha ya YESU, siwezi kuchukulia kwa uzito chochote kingine utakachosema.

Nitakuacha na huyu mtaalam wa Crime Forensics, J. Warner Wallace, aliyetumia utaalam wake kuthibitisha kama kweli YESU aliishi, alikufa na kufufuka, ndipo akawa Mkristo.


View: https://youtu.be/ajOYym3IuRk?si=RnetGYz_CLMIy69_

BYE

Nimefanya utafiti wa kutosha kuhusu historia ya mtu anayejulikana kama Yesu wa Nazareti, na baada ya kuchambua vyanzo mbalimbali vya kitaaluma, nimeamua kuchukua msimamo wa mythicists.


Hoja yangu kuu ni kwamba:


👉 Uhalisia wa kihistoria wa Yesu (historicity of Jesus) bado ni debatable.


Binafsi, msomi pekee ambaye ningeweza kumsikiliza kwa uzito kuhusu hoja ya “Yesu wa kihistoria” ni Emeritus Dr. Bart Ehrman. Hata hivyo, kwa mtazamo wangu, bado hajafanikiwa kupangua kwa ushahidi madhubuti hoja za Richard Carrier zinazodai kwamba simulizi ya Yesu ni simulizi ya kimatholojia zaidi kuliko ya kihistoria.




HOJA ZA MSINGI​


1. Kwa nini historia ya mtu mwenye ushawishi mkubwa kama Yesu ina ukakasi mkubwa?​


Swali langu la kwanza ni la kimantiki:


Ikiwa kweli Yesu alikuwa mtu mashuhuri sana, aliyefanya mambo makubwa sana katika karne ya kwanza, kwa nini historia yake ina mapengo makubwa, ukinzani mwingi, na utegemezi mkubwa wa simulizi za kidini badala ya ushahidi wa kihistoria?


Kwa watu wengine mashuhuri wa nyakati hizo – kama wafalme, wanajeshi na viongozi wa kisiasa – tunapata vyanzo vya kihistoria vilivyoandikwa wakati wao wakiwa hai.
Kwa Yesu, hali ni tofauti kabisa.




2. Tatizo la Waandishi wa Historia ya Yesu​


Hoja yangu ya pili ni kuhusu:


👉 NI KINA NANI WALIOANDIKA HISTORIA YA YESU?​


Ukweli wa kihistoria unaokubalika hata na wanazuoni wa Kikristo ni huu:


  • Walioandika injili hawakuwa wanafunzi wa moja kwa moja wa Yesu
  • Hawakuwahi kumuona Yesu uso kwa uso
  • Hawakuwa watu wa karibu naye
  • Waliandika habari zake kwa kusikia tu (second-hand information)

Zaidi ya hapo:


  • Injili ziliandikwa angalau miaka 30 hadi 70 baada ya kifo chake
  • Hayo ni makadirio tu – huenda muda ulikuwa mrefu zaidi

Hivyo, tunazungumzia historia iliyochelewa sana, isiyoandikwa na mashahidi wa moja kwa moja.

3. Majina ya Waandishi wa Injili Ni Majina ya Kupachikwa​


Kanisa linadai injili ziliandikwa na:


  • Marko
  • Mathayo
  • Luka
  • Yohana

Lakini ukweli wa kitaaluma ni huu:

Majina haya ni ya kupachikwa (pseudonymous)


Wanazuoni wa historia ya Ukristo wa kale wanakubaliana kwamba:

  • Waandishi halisi wa injili hawajulikani
  • Majina haya yalipewa maandiko hayo baadaye sana
  • Hakuna ushahidi wa moja kwa moja kwamba Mathayo, Marko, Luka au Yohana halisi waliandika maandiko hayo

Hii ni hoja inayokubalika katika tafiti nyingi za “peer-reviewed journals.”

4. Tatizo la Muda wa Uandishi​


Kwa mujibu wa makadirio ya kitaaluma:
  • Injili ya Marko iliandikwa takribani 70 AD
  • Mathayo takribani 80 AD
  • Luka takribani 90 AD
  • Yohana zaidi ya 90 AD
Hii ina maana kwamba:

Hakuna injili hata moja iliyoandikwa chini ya miaka 30 baada ya kifo cha Yesu.

Hivyo tunategemea simulizi zilizokusanywa kizazi kimoja au viwili baada ya tukio linalodaiwa kutokea.


5. Paulo Kama Chanzo cha Mapema – na Tatizo Lake​


Chanzo cha mapema zaidi tunachokitegemea ni maandishi ya Paulo (around 50 AD).


Lakini hapa pia kuna matatizo makubwa:


  • Paulo hakuwahi kumuona Yesu akiwa hai
  • Hakutegemea mashahidi wa moja kwa moja
  • Alidai kupata habari zake kupitia “mafunuo ya kiroho”

Zaidi ya hapo:


Paulo anapingana na simulizi za Injili​


Mfano:
  • Paulo hasemi chochote kuhusu kuzaliwa kwa Yesu kwa muujiza
  • Hasemi chochote kuhusu Bethlehem
  • Hasemi chochote kuhusu mamajusi, nyota, au bikira

Kwa mujibu wa Paulo, Yesu alizaliwa kama binadamu wa kawaida, si kwa miujiza kama injili zinavyodai.

6. Ukinzani Kati ya Injili Zenyewe​

Hata injili zenyewe zinapingana:
  • Mathayo na Luka wanatoa miaka tofauti ya kuzaliwa kwa Yesu
  • Nasaba za Yesu katika Mathayo na Luka hazifanani
  • Simulizi za kufufuka kwa Yesu zinatofautiana kati ya injili
Ukinzani huu unaonyesha kwamba simulizi hizi si historia thabiti, bali ni maandiko yaliyotungwa kwa malengo ya kidini.

7. Dalili za Hadithi za Kuazimwa (Borrowed Myths)​

Hoja nyingine muhimu ni kwamba:
Simulizi nyingi za Yesu zinafanana sana na hadithi za dini za zamani:
  • Kuzaliwa kwa muujiza – kunafanana na simulizi za miungu ya Kigiriki na Kirumi
  • Miujiza ya uponyaji – inafanana na hadithi za Elisha na Eliya
  • Kufufuka kutoka wafu – ni dhana iliyokuwepo katika dini nyingi za kale
  • Kupaa mbinguni – ni simulizi inayopatikana kwa miungu na mashujaa wengi wa kale
Hii inaashiria kwamba: Hadithi ya Yesu ina muundo wa kimaitholojia zaidi kuliko wa kihistoria.

8. Tatizo la Tarehe 25 Disemba​

  • Hakuna ushahidi wowote wa kihistoria kuwa Yesu alizaliwa tarehe 25 Disemba
  • Tarehe hiyo ilichaguliwa baadaye sana na Kanisa
  • Iliingizwa katika kalenda ya Kikristo kutokana na sherehe za kipagani za Kirumi

Hii inaonyesha jinsi simulizi ya Yesu ilivyochanganywa na mila na tamaduni za baadaye.

MWISHO:
ISAAC ASIMOV: “PROPERLY READ, THE BIBLE IS THE MOST POTENT FORCE FOR ATHEISM EVER CONCEIVED.”
 
1) Injili zinapingana. UONGO.
2) Maisha ya YESU hayana ushahidi wa kihistoria. UONGO.
3) Walioandika injili sio wanafunzi wa YESU. UONGO.
4) Hakuna unjili iliyoandikwa ndani ya miaka 30 baada ya YESU kufa. UONGO.
5) Paulo ndo chanza cha mapema cha simulizi la YESU. UONGO.
6) Paulo anapingana na injili. UONGO.
7)  Simulizi la YESU linafanaa na hadithi za zamani kwahiyo wamekopi. UPOTOSHI.
8) Wanahistoria wanasema YESU alizaliwa Desemba 25. UONGO.

Na kila mtu afanye kazi yake...

Not going to waste my energy spoonfeeding someone just pasting AI generated answers.
 
We have finally arrived in the era of great deception. Thanks to Artificial Intelligence.

Our LORD'S return is closer.
 
1) Injili zinapingana. UONGO.
2) Maisha ya YESU hayana ushahidi wa kihistoria. UONGO.
3) Walioandika injili sio wanafunzi wa YESU. UONGO.
4) Hakuna unjili iliyoandikwa ndani ya miaka 30 baada ya YESU kufa. UONGO.
5) Paulo ndo chanza cha mapema cha simulizi la YESU. UONGO.
6) Paulo anapingana na injili. UONGO.
7)  Simulizi la YESU linafanaa na hadithi za zamani kwahiyo wamekopi. UPOTOSHI.
8) Wanahistoria wanasema YESU alizaliwa Desemba 25. UONGO.

Na kila mtu afanye kazi yake...

Not going to waste my energy spoonfeeding someone just pasting AI generated answers.

1) Injili zinapingana. UONGO.
2) Maisha ya YESU hayana ushahidi wa kihistoria. UONGO.
3) Walioandika injili sio wanafunzi wa YESU. UONGO.
4) Hakuna unjili iliyoandikwa ndani ya miaka 30 baada ya YESU kufa. UONGO.
5) Paulo ndo chanza cha mapema cha simulizi la YESU. UONGO.
6) Paulo anapingana na injili. UONGO.
7)  Simulizi la YESU linafanaa na hadithi za zamani kwahiyo wamekopi. UPOTOSHI.
8) Wanahistoria wanasema YESU alizaliwa Desemba 25. UONGO.

Na kila mtu afanye kazi yake...

Not going to waste my energy spoonfeeding someone just pasting AI generated answers.
“The Bible is a human book and contains human error.”

Refer: Misquoting Jesus: The Story Behind Who Changed the Bible and Why, by Bart D. Ehrman

Also, Refer: Jesus, Interrupted: Revealing the Hidden Contradictions in the Bible (And Why We Don’t Know About Them), by Bart D. Ehrman

1. Where did Joseph and Mary live BEFORE Jesus was born?

Matthew: They already lived in Bethlehem
Matthew never mentions Nazareth at the beginning.
The story assumes Joseph and Mary are residents of Bethlehem.
Matthew 2:1 “Now after Jesus was born in Bethlehem of Judea in the days of Herod the king…”

Only AFTER returning from Egypt do they go to Nazareth:

Matthew 2:23 “And he went and lived in a city called Nazareth, so that what was spoken by the prophets might be fulfilled…”

In Matthew:
Bethlehem → Egypt → Nazareth

Luke
: They originally lived in Nazareth
Luke gives the opposite picture.
Luke 1:26-27 “God sent the angel Gabriel to Nazareth, a town in Galilee, to a virgin… Mary.”
Before Jesus is born, they are already living in Nazareth.
They go to Bethlehem only temporarily because of a census:
Luke 2:4 “So Joseph also went up from the town of Nazareth in Galilee to Judea, to Bethlehem…”
After the birth they return home:
Luke 2:39 “When Joseph and Mary had done everything required by the Law of the Lord, they returned to Galilee to their own town of Nazareth.”

In Luke:
Nazareth → Bethlehem (briefly) → Nazareth

CONTRADICTION #1 – Original Home
Matthew
: Family originally in Bethlehem
Luke: Family originally in Nazareth
Both cannot be true at the same time.


2. The Reason for Going to Bethlehem
Matthew
: No journey mentioned
Matthew never says they traveled to Bethlehem.
Jesus is simply born there with no explanation.

Luke: Census is the reason
Luke invents a Roman census requiring travel.
Luke 2:1-5 “A decree went out from Caesar Augustus that all the world should be registered… and everyone went to their own town.”

Matthew gives no census story at all.

CONTRADICTION #2
Luke
: Bethlehem trip caused by a Roman census
Matthew: No census, no trip, already living there


3. What Happened After Jesus Was Born?
Matthew
: Escape to Egypt
After the birth:
Wise men visit
Herod wants to kill the child
Family flees to Egypt
Later they return and settle in Nazareth
Matthew 2:13-14 “An angel of the Lord appeared to Joseph… ‘Take the child and his mother and escape to Egypt.’”

Luke: No Egypt, peaceful return home
Luke knows nothing about:
Wise men
Herod killing babies
Flight to Egypt

Instead:
Luke 2:22
They present Jesus at the temple in Jerusalem.
Then immediately:
Luke 2:39 “They returned to Galilee, to their own town of Nazareth.

CONTRADICTION #3 – After the Birth
Matthew: Bethlehem → Egypt → Nazareth
Luke: Bethlehem → Jerusalem → Nazareth
Egypt story is completely absent in Luke
Both timelines cannot coexist.


4. Visitors to Baby Jesus
Matthew: Wise Men
Matthew 2:1 – Magi from the east visit.
Luke: Shepherds
Luke 2:8-16 – Shepherds visit.

Matthew: No shepherds
Luke: No wise men



Refer to these scholarly books on Jesus mythologies.
  • Nailed: Ten Christian Myths That Show Jesus Never Existed at All — David Fitzgerald
  • On the Historicity of Jesus: Why We Might Have Reason for Doubt — Richard Carrier
  • Jesus from Outer Space: What the Earliest Christians Really Believed about Christ - Richard Carrier
 
Kijana hapo juu,

Mimi sipelekwi pelekwi na mawimbi.

Urudi hapa ukishakubali YESU aliishi, alikufa na kufufuka karne ya kwanza. Zaidi ya hapo, hatuna cha kuongelea.

Until then Biblia utaona maruweruwe tu...
 
Kwa kundi kubwa la atheists lililopo humu, wanazunguka kimakundi kuupinga ukristo! Hawajui imani ni ya mtu binafsi, imani ni jambo linalohitaji kutuliza fahamu zako ili kuona Mungu akitenda kazi ndani yako
Imani ni ya mtu binafsi lakini ukishaileta JF umeileta katika public square inaondoka kwenye jambo la mtu binafsi.

Huelewi wapi?
 
Sikiliza PhD ya Math, Astronomy na Physiciss (Michael Guillen) hiyo: anasema wanasayansi wenyewe inafika point wanahitaji imani, kama vile mpaka leo hawajui Dark matter ni nini hawajawahi kuiona wala kuipima moja kwa moja lakini wanaamini ipo kwasababu wanaona matokeo yake.


View: https://youtu.be/Go0H58NtoAk?si=weMIajZue1UtOTV8

Dr. Michael Guillen anasema:
Ukristo na Sayansi umeanza karibia wakati uleule, karibia miaka 2000 iliyopita (tuki assume sayansi ya kisasa imeanza na Aristotle).

Tangu vimeanza, Ukristo (Biblia) ni kama mlima uliosimama imara, haujabadilika. Huku sayansi ikiwa mto unaoenda ukiyumbayumba.

Tangu mto wa sanyansi uanze, je unazidi kwenda mbali na Mlima huu, au unazidi kuusogelea?

Kwa maana nyingine, je inatia akili kuamini mtazamo wa maisha wa Kikristo katika karne hii ya mtazamo wa maisha wa Kisayansi?

1) Zamani wanasayansi waliamini ulimwemgu ulikuwepo milele. Wakaja kugundua ulimwengu ulikuwa na mwanzo.

"Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na dunia."
Mwanzo.1.1.NENO


2)
Wanasayansi wamegundua kuwa Uhalisia wa ulimwengu (Reality) kwa kawaida hauonekani, ni takriban asilimia 5% tu ya uhalisia ndio inaonekana (dark matter, dark energy hazionekani, tunaona tu matokeo yake).

Ndomaana tumeagizwa:
"Kwa hivyo hatuangalii yale yanayoonekana, bali yale yasiyoonekana. Kwa maana yale yanayoonekana ni ya kitambo tu, bali yale yasiyoonekana ni ya milele."
2Wakorintho.4.18.NENO

Sayansi haipingi neno la MUNGU, inaithibisha.


3) Wanasayansi wamegundua kuwa Kweli nyingi za ulimwengu hazina mantiki, zinapita mantiki (Dr. Guillen anaziita translogical).

Mfano:
A) Quantum Physics
.
Quantum Physics ni Sayansi ya vichembe vidogo kabisa, katika kiwango ambacho sheria za kawaida za fizikia hazifanyi kazi.

Kwenye Quantum Physics:
i) Kitu kinaweza kuwa katika hali mbili tofauti kwa wakati mmoja (Superposition).

ii) Vitu viwili vinaweza kuathiriana papo hapo hata vikiwa mbali kabisa (Entanglement).

iii) Kitu kinaweza ku behave kama mawimbi na kama kitu kigumu kwa wakati mmoja.

Haya mambo matatu yako kinyume na sheria za mantiki lakini ni kweli zinazopimika na ndio msingi wa teknlojia za kisasa kama GPS.

B) Mfano mwingine: Gödel’s incompleteness theorem.

Hii nadharia ya kutokamilika ya Gödel inasema kuwa: katika mfumo wowote wa kimantiki wenye uwezo wa kuelezea hesabu, kuna kauli za kweli ambazo haziwezi kuthibitishwa kimantiki ndani ya mfumo huo.

Sasa ona: "Kauli hii haiwezi kuthibitishwa ndani ya mfumo huu."

i) Basi, Ikiwa mfumo unaweza kuthibitisha kauli hiyo, basi kauli hiyo ni ya uongo (kwa sababu imesemwa kuwa kauli hiyo haiwezi kuthibitishwa), na mfumo unakuwa unathibitisha jambo la uongo, maana yake mfumo huo si thabiti.

iii) Lakini, Ikiwa mfumo hauwezi kuithibitisha, basi kauli hiyo ni ya kweli, lakini haiwezi kuthibitishwa ndani ya mfumo huo.

iv) Kwa vyovyote vile, kuna kauli ya kweli ambayo mfumo huo hauwezi kuithibitisha.

Mfano wa mfano huu:

a) Fikiria kitabu kinacholenga kuwa na kauli zote za kweli za kihisabati. Kinatumia sheria maalum (axioms) kuthibitisha kauli hizo.

b) Gödel anaonyesha kuwa kitabu hicho kama ni thabiti, hakiwezi kuwa kamili kwasababu sikuzote kutakuwa na kauli ambazo ni za kweli lakini haziwezi kuthibitishwa kwa kutumia sheria za hicho kitabu.

c) Kuongeza sheria zaidi hakutatui tatizo bali kweli mpya zisizothibitishika zitaendelea kuonekana.

d) Hivyo, ukweli ni mkubwa kuliko uthibitisho, na sheria za mantiki zina mipaka yake. (Ukisikia Mantiki ya bei rahisi).

Ndomaana MUNGU anatuambia:
“Kwa kuwa mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu,” asema Mwenyezi Mungu.

“Kama vile mbingu zilivyo juu kuliko dunia, ndivyo njia zangu zilivyo juu kuliko njia zenu na mawazo yangu kuliko mawazo yenu."

isaya.55.8-9.NENO

Dr. Guillen anasema YESU si wa kimantiki (lakini ni moja ya kweli tunaoshuhudia ulimwenguni)


4) Uhalisia (Reality) ni wa ajabu usio na kikomo (Infinitely mysterious)

Dr. Guillen anasema alifikiri Sayansi ikipewa muda ingejibu maswali yake yote.

Lakini anakuja kugundua Sanyansi ikijibu swali moja, 100 yanazuka. Kila wakigundua kitu, wanagundua na mengine hivi kwamba wanajikuta wanahitaji teknolojia kubwa zaidi, mashine kubwa zaidi kulichunguza, ni kama shimo lisilo na mwisho!

"Yeye hutenda maajabu yasiyoweza kutambuliwa, miujiza isiyoweza kuhesabika."
Ayubu.5.9.NENO


5)
Muda ni mstari ulionyooka.

Zamani wanasayansi walifikiri muda ni duara, kwamba historia itajirudia.

(Ni kama zile imani za kule mashariki wanavyoamini kuwa ulimwengu unaanza na kuharibiwa over and over forever, na nafsi zetu zinarudi tena na tena).

Ukristo umejua kuwa ulimwengu uliumbwa mara moja, na YESU atarudi mara moja.

“Tazama, naja upesi! Thawabu yangu i mkononi mwangu, nami nitampa kila mtu sawasawa na alivyotenda.

Mimi ni Alfa na Omega, wa Kwanza na wa Mwisho, Mwanzo na Mwisho.

Ufunuo.22.12-13.NENO


6)
Kwenye kiini chale kabisa, Ulimwengu ni wa kiroho (Supernatural).

Ukisoma Sayansi ya kisasa, mfano Quantum Mechanics (Sayansi ya tabia za chembe ndogo zaidi), unaelewa kuwa ni ngumu kutofautisha kipi ni cha kimwili na kipi kimepita mwili (Supernatural, cha kiroho).

Quantum Mechanics kwakweli imepita mwili, ni ya kiroho, na ndiyo msingi wa Sayansi ya kisasa.

Bilbia ilishatuambia kuwa tunakabiliana na viumbe ambao wamepita mwili (Supernatural):

"Kwa maana kushindana kwetu si dhidi ya mwili na damu, bali dhidi ya falme na mamlaka, dhidi ya wakuu wa ulimwengu huu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho."
Waefeso.6.12.NENO


7)
Wanabayolojia wa mageuzi wanakubali kuwa Binadamu (Homo sapiens sapiens) si kama wanyama wengine. Ni wa kipekee.


8) Ulimwengu umesetiwa mahususi kwa ajili ya kutegemeza maisha. Vipimo vyake thabiti visivyobadilika visingekuwa mahususi kama vilivyo, ulimwengu usingekuwepo.

Mfano:
i) Fine Structure Constant: inashikilia atoms
ii) Electron to proton mass ratio: inaongoza sheria za kemia.
iii) Strong Nuclear Force: inaunganisha atoms.

iv) Electromagnetic Force constant: ina support sheria za kemia.
v) Gravitational constant: inashikilia nyota, sayari, anga za sayari n.k

vi) Kasi ya mwanga: inaongoza sheria za kemia.
vii) Planck's constant: ina support sheria za kemia.

9)
Dr. Guillen anasema Time, Space and Matter sio kati ya Kweli za kudumu (Absolute truths), hizo ni kweli za upande fulani (Relative truths).

Kwahiyo akisikia mkristo anabishania umri wa ulimwengu anajua hajui wanaongelea nini, ukweli ni kuwa Ulimwengu una mabilioni ya miaka au umri wake haujafika hata sekundi moja, ikitegemea unatazamia kutoka wapi.

Sayansi inaongea kutoka upande mmoja na Biblia kutoka upande mwingine na zote ni kweli kwasabu ni pande tofauti.

Muda ni mfumo rejeleo (reference frame), muda sio kweli ya kudumu.

(Taarifa: dunia ina umri wa miaka elfu chache tu)

Highlight:
1) Kweli inaweza isiwe na mantiki
2) Ukweli ni mkubwa kuliko uthibtisho
3) Sheria za mantiki zina mipaka yake.
4) Kuna kweli za kudumu na kweli za upande fulani.
 
Hivi tujiulize kwanini huyo Mungu wenu hana uwezo ws kujifunua wala kujieleza kwa watu zaidi ya kutegemea wafia dini kutumia vitabu vya karne na karne kueleza uwepo wa huyo Mungu?.

Alafu ni Mungu yupi huwa mnamzungumzia maana kuna Miungu wengi maelfu kwa maelfu, unaposema Mungu yupo unatakiwa ujibu ni yupi maana kila dini ina Mungu wake anayepingana na dini nyingine, na wote hawa wanadai wanazo Mbingu za kuwapeleka wanaomuamini pia jehanamu kwa wasio muamini, vipi jamani kutakuwa na Mbingu+jehanamu ngapi kwa kila Dini zote duniani?😂😂😂😂.

Michezo hii
Tangu mumuone mungu wa wahindi imewasaidia nini? Hebu hukoo🚮
 
1) Kulelewa na wazazi wakristo sio kuwa Mkristo. Kuwa Mkristo ni kukutana na Kristo kibinafsi.

Ni kama ulikuwa unasikia story za mjomba kwa miaka, hatimaye akaja nyumbani.

2) Nilipoteza imani nikiwa form 3, tena kwasababu ya kusoma posts za humu JF!

Ndomana mzungu alisema: Little knowledge is a dangerous thing.

3)
Mwanzoni na mimi nikawa kwenye kempu ya wakana MUNGU, kama vile kufuata mkumbo tu, kuhisi unafanya jambo flani la maana la kishujaa sana kuwaambia watu kuwa hakuna MUNGU.

Unajikuta muokozi: unaona kama waamini Mungu wanateseka sana kufuata sheria za Mungu wakati wangejua hakuna Mungu wangefanya chochote wanachotaka wa enjoy life, si unajua we only live once?

Wanateseka
kufuata desturi zisizo na maana kama vile kujichosha kwenda kanisani asubuhi wakati muda huo wangelala! ! !

Yani unajikuta una akili sana kuwa: kati ya mabilioni wote kwenye historia, wewe ni kati ya wachache umetambua ukweli uliofichwa, ambao kuna watu fulani huko hawataki uujue.

Au ni kati ya wachache waliowahi kuutambua, si unajua tumetokana na sokwe? Kwahiyo ni process mdogomdogo kutambua kuwa hakuna Mungu, na kuachana na imani za kisokwe sokwe.

Eti MUNGU kajifunua kupitia uumbaji, kitabu chake na kupitia YESU:

Huu ukweli ulio wazi hivi haiwezekani kuwa ndio ukweli:

kwanza watu wengi wanaukubali, tena watu wa ajabu ajabu hawajasoma, maskini.

Halafu ni mwepesi mwepesi sana, Ukweli utakuwa mgumu mgumu wa kujulikana na wasomi.

Halafu ni habari za muda mreeefu zimeboa zimepitwa na wakati, sasa hivi kila kitu kinabadilika, lazima tuwe habari mupya mupya zitutoe kwenye line zitusisimue zitushughulishe tusogoe tubishane tupigane..


4) Baadaye nikachoka mimi kinyozi wa mwandambo na hawa Waamini MUNGU wasio na akili nikabadilika:

kwanza kila kitu hakina maana, so what kama watu wameamua kujitungia mtu wa kufikirika kisha wajihangaishe naye hadi wanakufa?

Kwanini ni muhimu kwangu kubadilisha mawazo yao? ?

Mwishowe tunapotea tu into nothing, Kwanini napoteza nguvu kukaa kubishana na nothing?

Kwanini hii miaka 80 ya kuishi ni ya muhimu sana mimi kujihangaisha na chochote kile, achana hata na imani kwanini nifanye kazi? Kwanini uhai ni muhimu kiasi nijisumbue kuulinda au kuutetea? Kila kitu mwisho wake ni nothing.

Nikawa apathetic: zero interest zero concern. Nikaachana na habari za imani na dini.

Nikiona watu wanabishania imani wote waamini na wasioamini nawaona wendawazimu tu.

Nikiona watu wanahangaika kwenda kanisani kila siku kuhubiri huko barabarani naona kazi bure, hawana kazi za kufanya!

Nikawa tu occupied na maisha ya shule na nyumbani. Bado nilikuwa mdogo so bado nilikuwa nina hamu na maisha yajayo.

4) Kuingia chuo nikakutana na wale wanawahi kula maembe mabichi na chumvi wakati nyie mnasubiri yaive, akani introduce kwenye imani flani za huko Mashariki ya mbali.

Akawa ananiambia habari za Ufahamu ulio mkuu zaidi. The Supreme consciousness. Nilikuwa interested kwasababu zilikuwa taarifa mpya kwangu lakini sikuamini.

5) Baadae nikaja kupigwa na kitu kizito, nikakuguswa na waya mwekundu.

Nikajiuliza hivi wewe Mungu upo kweli?

How could you let this Great injustice fall upon me? ? This great violation of my human rights! !

Me a poor innocent helpless soul who wouldn't hurt a fly!

Ona nilishaamua Mungu hayupo lakini ghafla nikamkumbuka tena namlaumu huko huko aliko ambapo hata hayupo! ! !

Hii nguvu kuu ni nguvu gani hainisaidii? Huu Ufahamu mkuu kwanini haukunifahamisha mapema?

Hivi maisha ndo haya tu? Zaliwa, fanya kazi, teseka, kufa? ?


6) Wakati huo nilipata nafasi ya kukaa tu nyumbani muda mrefu: sisomi, sifanyi kazi yoyote, sitoki kwenda kokote. Watu wakija kuniona sitoki kuwaona.

Sanasana nilikuja kununua vifaranga, nikawa nashinda na vifaranga! !

7) Nikaanza kuwa interested, nikatafuta habari za ile Supreme Consciousness.

Nikawasoma wabudha, wahindu, nimewasikiliza ma Guru weee, rafiki yangu yule alikuwa anapost sana videos za Sadhguru, ndo nikaanzia kwake.

8) Ikafika point officially nilisadiki kuwa kuna Ufahamu Mkuu zaidi.

Niliona lazima kuna kitu beyond ulimwengu huu (space, time and matter).

9) Huko ndo mawazo / ufahamu wa watu hutokea. Ufahamu wetu ni zaidi ya kazi ya ubongo.

- Ndomaana kuna watu sehemu muhimu za ubongo zilitolewa ili kuwatibu lakini bado wali function kawaida.

- Kuna watu ingawa sehemu ya kushoto na kulia ya ubongo ilibidi zitenganishwe, bado wali function kama kawaida. Unaweza kukata komputa yako katikati ikaendelea kufanya kazi?

- Kuna watu ingawa walikuwa wamelala muda mrefu hawajitambui, walivyoamka walisema yaliyotokea wakati wamelala.

Huyu Neurosurgeon anaelezea hayo:


View: https://youtu.be/41bIJ7hYbLs?si=3m7w0NO4TuXHKFf9


10) Nikajua kutoka huko ndo kina Isaac Newton walipopokea ufunuo wa mambo waliyogundua.

11) Nikajua kama hakuna kingine zaidi ya ulimwengu huu ambamo kila kitu kinabadilika / kinaoza, hatuwezi kujua ukweli kamwe: either kila kitu ni kweli au kila kitu ni uongo.

Kwanini? Kwasababu Tunakosa msingi wa kuamua ukweli ni upi.

Na binadamu tulivyo tunataka kujua ukweli, tunataka kuelewa, tunataka sense / maana.

Hata sababu binadamu tunaweza kujadiliana ni kuwa kuna misingi ya maana tunaifuata. Otherwise ingekuwa kama kwenye mnara wa babeli.

12) Hiyo misingi ya maana imetoka wapi?


Kuna ulimwengu mwingine nje ya huu: ulimwengu wa milele, ambao haubadiliki wala kuoza, ulimwengu wenye Ufahamu Mkuu ambao uko connected na huu.

Huko ndio chanzo / msingi cha ukweli / ufahamu / maana.

Huo ulimwengu ndio mstari ulionyooka tunaotumia kupimia mistari mingine kama imepinda.

Ndio huko tunatoa sheria za mantiki.

Ndio huko tunatoa Hesabu, ulimwengu uko chini ya sheria zake.

Ndio huko tunatoa sheria za milele maadili mfano:kuua mtu asiye na hatia ni kosa. Binadamu ana haki ya kuishi. Binadamu ana haki ya uhuru.

13) Otherwise hakuna kwenye haki ya kusema ni kosa kuua mtu asiye na hatia. Ni kosa kwa misingi ipi? Kisa katiba hizi walizotunga binadamu? ? Nani kawapa hao binadamu mamlaka ya kuniamulia kipi kizuri kipi kibaya? ?

Ni kundi la watu wachache tu wanaotaka kuninyanyapaa na kuniamulia kwa nguvu jinsi ya kuishi! ! !

Hata mkiwa bilioni 7 mmekubaliana, mimi niko peke yangu nakataa, nani aliyeamua kuwa mna haki ya kutunga sheria hii juu yangu? ?Mnatumia mabavu?

Watasema oooh ni kwa ajili ya kuendeleza maisha inabidi tuweke sheria tusimalizane otherwise maisha yatapotea ulimwenguni: ni nani kasema kwamba uhai una thamani? Tuulinde kwa nguvu zote? Mimi nasema hauna thamani, sio tu tuue vichanga tumboni nikipata nyuklia namaliza wote, kuna tatizo hapo? Nani kasema? Je huu si muendelezo wa unyanyapaa kwangu kuishi navyotaka kwenye ulimwengu huu niliojipata?

Watasema oohh wewe fanya unavyotaka usiingilie uhuru wa mtu: ni nani kasema ni vibaya kumnyima mtu uhuru? Ni hizi katiba zenu mlizojitungia? Huu ni muendelezo wa matumizi ya
mabavu na unyanyapaa kwangu nayetaka kukufanya mtumwa mwangu, sikulipi na nitakutesa!
 
Sheria za milele za maadili zipo, hata wasiomuamini MUNGU dhamiri zao zinashuhudia sheria hizi.

14) Na huko zilikotoka ni nje ya ulimwemgu huu! Nje ya time, space and matter!

Utataka upaone kwa macho wakati macho ni limit ya matter.

Utasema mbona hawajapaona kwa miaka 6000 sasa, lakini miaka 6000 ni limit ya time.

Utataka upachunguze na vifaa ambavyo viko limited na space.

Tunahitaji kupita mambo hayo, ndomana tunatumia Ufahamu, unaopita yote hayo kwasababu ndio uko connected na huo ulimwengu.

Ndo inapokuja IMANI:
Unaona
bila macho.
Unakipata kabla hakijafika.
Unauishi wakati ulimwenguni hakionekani.

Kwa kutumia Ufahamu!

Kuona mtu ana furaha wakati ana matatizo / anateswa sio ajabu, huyo amepita mipaka ya Ulimwengu.

15) Kwa logic za bei rahisi: Maumivu = huzuni.

Kwa Ufahamu uliopita ulimwengu huu: Maumivu = Shangwe.

Kwa logic ya bei rahisi: Kifo = Kupoteza / kupungua

Kwa Ufahamu uliopita ulimwengu huu: Kifo = Kupata / kuongezeka.

Kwa logic za bei rahisi: Miaka 6000 = Muda mreefu

Kwa Ufahamu uliopita ulimwengu huu Miaka 6000 = Ni nukta

Piga hesabu.

16) Na hili sio swala la kumkalisha mtu kumshurutisha, kumshawishi, ku dejadiliana kila siku.

Ni swala binafsi kabisa, la moyo na ufahamu wa mtu.

Hata hoja bora zaidi duniani haiwezi kuukamata moyo, otherwise watu wangejifunza tu kutengeneza hoja nzuri wawapate wapenzi wa maisha yao.

Lakini kama mtu hakupendi hakuendi tu jamani.

17) Ndomaana ule Ufahamu Mkuu, ambaye ndio Upendo wenyewe:

ametupa wote muda na uhuru tufanye tunavyotaka humu ulimwenguni,

ametupa muda na uhuru tujifunze mema na mabaya,

ametupa muda na uhuru tumjue na tumchague kwa hiari,

ametupa haki ya kuja kuishi na kufurahi milele pamoja na makosa yote tuliyofanya kwasababu ameyalipia yeye mwenyewe,

ametupa uhuru wa kumkataa.

18)
Na wote
watakaomkataa naye atawakataa. Watatambua kuwa wamekataliwa, ndomaana tunaambiwa watalia na kusaga meno! Maumivu ya kukataliwa na ule Ufahamu Mkuu.

Na mwishowe, mapenzi yao yatatimizwa, nao watarudi into nothing (mauti wa pili).


"Hapo mfalme akawaambia watumishi, ‘Mfungeni miguu na mikono mkamtupe nje gizani; huko atalia na kusaga meno.”

Mathayo.22.13.BHN

"Lakini wale ambao ufalme huo ni wao watatupwa nje, gizani, ambako watalia na kusaga meno.”

Mathayo.8.12.BHN


"Lakini waoga, wasioamini, wachafu, wauaji, wazinzi, wachawi, waabudu sanamu, pamoja na waongo wote, mahali pao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.”
Ufunuo.21.8.NENO

"Kisha mauti na Kuzimu zikatupwa katika ziwa la moto. Hii ndio mauti ya pili, yaani hilo ziwa la moto."
Ufunuo.20.14.NENO

Hongera sana kurejea katika imani sahihi ya Yesu Kristo, wewe ni mtumishi mwenye ushuhuda ndani yake, wasaidie wengine waliochotwa huko.
Ubarikiwe sana
 
Kuna sehemu atheist mnaandamwa? Kwanini mnaingilia imani za watu?
Binafsi sijaingilia imani ya mtu.

Kuingilia imani ya mtu kimsingi labda umfuate nyumbani kwake, au umfuate msikitini, au umfuate kanisani.

Hapa ni JF. Public Square. Mada ikishakuja hapa ishakuwa kwenye pubkic square, kuijadiki si kuingikia imani ya mtu.

Na mimi hata sianzishi thread nachangia walichoanzisha wengone tu.

Sasa nawezaje kuingilia imani ya mtu kama topics zishaanzishwa kwenye public squre, tena nyingine hata sijaziona naitwa kuchangia. Ina maana kuna watu wanataka kujua fikra zangu.

Sasa hapo nikichangia utasemaje naingilia imani ya mtu?

Na hata wanaoanzisha mada, unaosema wanaingilia imani za watu, kama wewe imani yako ni ya kweli, kwa nini unaikinga sana isiingiliwe na watu? Si uwajibu tu maswali yao, uwajibu tu hoja zao mpaka wajue imani yako ni sahihi na ya kwenye ukweli?

Kwa nini unataka sana imani yako ikingwe isiingiliwe na watu?

Kwa nini unaifanya imani yako special sana?

Vipi kama kuna mtu imani yake ni kuingilia imani za watu?

Huoni kuwa ukitaka imani yako isiingiliwe na wewe utakuwa umeingilia imani ya huyo mtu ya kuingilia imani za watu?

Vipi kama imani yako ni ya kwenye uongo, unaeneza uongo na ujinga?

Huoni kuwa kutaka imani yako isiingiliwe ni kutaka ukweli na elimu visiifichue imani yako kuwa ni ya uongo na ujinga?
 
Back
Top Bottom