Kipindi siamini MUNGU, sikuwa na muda na imani za watu

Kipindi siamini MUNGU, sikuwa na muda na imani za watu

Kutotaka kuitwa mjinga ni ujinga mwingine nimekuambia.

Dunia haijali unataka nini.

Kama wewe ni mjinga, ni mjinga tu whether unataka au hutaki kuitwa mjinga.

Wewe ni mjinga sana kiasi huelewi hili?
Khaa😂😂😂 sawa mkuu
 
LEO HOJA HAKUNA!

Ni matusi tu shubamit.


YESU AMESHINDA!

PIGIA YESU MAKOFI!
 
Dr. Michael Guillen anasema:
Ukristo na Sayansi umeanza karibia wakati uleule, karibia miaka 2000 iliyopita (tuki assume sayansi ya kisasa imeanza na Aristotle).

Tangu vimeanza, Ukristo (Biblia) ni kama mlima uliosimama imara, haujabadilika. Huku sayansi ikiwa mto unaoenda ukiyumbayumba.

Tangu mto wa sanyansi uanze, je unazidi kwenda mbali na Mlima huu, au unazidi kuusogelea?

Kwa maana nyingine, je inatia akili kuamini mtazamo wa maisha wa Kikristo katika karne hii ya mtazamo wa maisha wa Kisayansi?

1) Zamani wanasayansi waliamini ulimwemgu ulikuwepo milele. Wakaja kugundua ulimwengu ulikuwa na mwanzo.

"Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na dunia."
Mwanzo.1.1.NENO


2)
Wanasayansi wamegundua kuwa Uhalisia wa ulimwengu (Reality) kwa kawaida hauonekani, ni takriban asilimia 5% tu ya uhalisia ndio inaonekana (dark matter, dark energy hazionekani, tunaona tu matokeo yake).

Ndomaana tumeagizwa:
"Kwa hivyo hatuangalii yale yanayoonekana, bali yale yasiyoonekana. Kwa maana yale yanayoonekana ni ya kitambo tu, bali yale yasiyoonekana ni ya milele."
2Wakorintho.4.18.NENO

Sayansi haipingi neno la MUNGU, inaithibisha.


3) Wanasayansi wamegundua kuwa Kweli nyingi za ulimwengu hazina mantiki, zinapita mantiki (Dr. Guillen anaziita translogical).

Mfano:
A) Quantum Physics
.
Quantum Physics ni Sayansi ya vichembe vidogo kabisa, katika kiwango ambacho sheria za kawaida za fizikia hazifanyi kazi.

Kwenye Quantum Physics:
i) Kitu kinaweza kuwa katika hali mbili tofauti kwa wakati mmoja (Superposition).

ii) Vitu viwili vinaweza kuathiriana papo hapo hata vikiwa mbali kabisa (Entanglement).

iii) Kitu kinaweza ku behave kama mawimbi na kama kitu kigumu kwa wakati mmoja.

Haya mambo matatu yako kinyume na sheria za mantiki lakini ni kweli zinazopimika na ndio msingi wa teknlojia za kisasa kama GPS.

B) Mfano mwingine: Gödel’s incompleteness theorem.

Hii nadharia ya kutokamilika ya Gödel inasema kuwa: katika mfumo wowote wa kimantiki wenye uwezo wa kuelezea hesabu, kuna kauli za kweli ambazo haziwezi kuthibitishwa kimantiki ndani ya mfumo huo.

Sasa ona: "Kauli hii haiwezi kuthibitishwa ndani ya mfumo huu."

i) Basi, Ikiwa mfumo unaweza kuthibitisha kauli hiyo, basi kauli hiyo ni ya uongo (kwa sababu imesemwa kuwa kauli hiyo haiwezi kuthibitishwa), na mfumo unakuwa unathibitisha jambo la uongo, maana yake mfumo huo si thabiti.

iii) Lakini, Ikiwa mfumo hauwezi kuithibitisha, basi kauli hiyo ni ya kweli, lakini haiwezi kuthibitishwa ndani ya mfumo huo.

iv) Kwa vyovyote vile, kuna kauli ya kweli ambayo mfumo huo hauwezi kuithibitisha.

Mfano wa mfano huu:

a) Fikiria kitabu kinacholenga kuwa na kauli zote za kweli za kihisabati. Kinatumia sheria maalum (axioms) kuthibitisha kauli hizo.

b) Gödel anaonyesha kuwa kitabu hicho kama ni thabiti, hakiwezi kuwa kamili kwasababu sikuzote kutakuwa na kauli ambazo ni za kweli lakini haziwezi kuthibitishwa kwa kutumia sheria za hicho kitabu.

c) Kuongeza sheria zaidi hakutatui tatizo bali kweli mpya zisizothibitishika zitaendelea kuonekana.

d) Hivyo, ukweli ni mkubwa kuliko uthibitisho, na sheria za mantiki zina mipaka yake. (Ukisikia Mantiki ya bei rahisi).

Ndomaana MUNGU anatuambia:
“Kwa kuwa mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu,” asema Mwenyezi Mungu.

“Kama vile mbingu zilivyo juu kuliko dunia, ndivyo njia zangu zilivyo juu kuliko njia zenu na mawazo yangu kuliko mawazo yenu."

isaya.55.8-9.NENO

Dr. Guillen anasema YESU si wa kimantiki (lakini ni moja ya kweli tunaoshuhudia ulimwenguni)


4) Uhalisia (Reality) ni wa ajabu usio na kikomo (Infinitely mysterious)

Dr. Guillen anasema alifikiri Sayansi ikipewa muda ingejibu maswali yake yote.

Lakini anakuja kugundua Sanyansi ikijibu swali moja, 100 yanazuka. Kila wakigundua kitu, wanagundua na mengine hivi kwamba wanajikuta wanahitaji teknolojia kubwa zaidi, mashine kubwa zaidi kulichunguza, ni kama shimo lisilo na mwisho!

"Yeye hutenda maajabu yasiyoweza kutambuliwa, miujiza isiyoweza kuhesabika."
Ayubu.5.9.NENO


5)
Muda ni mstari ulionyooka.

Zamani wanasayansi walifikiri muda ni duara, kwamba historia itajirudia.

(Ni kama zile imani za kule mashariki wanavyoamini kuwa ulimwengu unaanza na kuharibiwa over and over forever, na nafsi zetu zinarudi tena na tena).

Ukristo umejua kuwa ulimwengu uliumbwa mara moja, na YESU atarudi mara moja.

“Tazama, naja upesi! Thawabu yangu i mkononi mwangu, nami nitampa kila mtu sawasawa na alivyotenda.

Mimi ni Alfa na Omega, wa Kwanza na wa Mwisho, Mwanzo na Mwisho.

Ufunuo.22.12-13.NENO


6)
Kwenye kiini chale kabisa, Ulimwengu ni wa kiroho (Supernatural).

Ukisoma Sayansi ya kisasa, mfano Quantum Mechanics (Sayansi ya tabia za chembe ndogo zaidi), unaelewa kuwa ni ngumu kutofautisha kipi ni cha kimwili na kipi kimepita mwili (Supernatural, cha kiroho).

Quantum Mechanics kwakweli imepita mwili, ni ya kiroho, na ndiyo msingi wa Sayansi ya kisasa.

Bilbia ilishatuambia kuwa tunakabiliana na viumbe ambao wamepita mwili (Supernatural):

"Kwa maana kushindana kwetu si dhidi ya mwili na damu, bali dhidi ya falme na mamlaka, dhidi ya wakuu wa ulimwengu huu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho."
Waefeso.6.12.NENO


7)
Wanabayolojia wa mageuzi wanakubali kuwa Binadamu (Homo sapiens sapiens) si kama wanyama wengine. Ni wa kipekee.


8) Ulimwengu umesetiwa mahususi kwa ajili ya kutegemeza maisha. Vipimo vyake thabiti visivyobadilika visingekuwa mahususi kama vilivyo, ulimwengu usingekuwepo.

Mfano:
i) Fine Structure Constant: inashikilia atoms
ii) Electron to proton mass ratio: inaongoza sheria za kemia.
iii) Strong Nuclear Force: inaunganisha atoms.

iv) Electromagnetic Force constant: ina support sheria za kemia.
v) Gravitational constant: inashikilia nyota, sayari, anga za sayari n.k

vi) Kasi ya mwanga: inaongoza sheria za kemia.
vii) Planck's constant: ina support sheria za kemia.

9)
Dr. Guillen anasema Time, Space and Matter sio kati ya Kweli za kudumu (Absolute truths), hizo ni kweli za upande fulani (Relative truths).

Kwahiyo akisikia mkristo anabishania umri wa ulimwengu anajua hajui wanaongelea nini, ukweli ni kuwa Ulimwengu una mabilioni ya miaka au umri wake haujafika hata sekundi moja, ikitegemea unatazamia kutoka wapi.

Sayansi inaongea kutoka upande mmoja na Biblia kutoka upande mwingine na zote ni kweli kwasabu ni pande tofauti.

Muda ni mfumo rejeleo (reference frame), muda sio kweli ya kudumu.

(Taarifa: dunia ina umri wa miaka elfu chache tu)

Highlight:
1) Kweli inaweza isiwe na mantiki
2) Ukweli ni mkubwa kuliko uthibtisho
3) Sheria za mantiki zina mipaka yake.
4) Kuna kweli za kudumu na kweli za upande fulani.
(Edited)

Dr. Michael Guillen (PhD in Math, Astronomy and Physics)
 
Kukubali hilo ni mwanzo wa kutoka kwenye ujinga.

Huwezi kuuondoa ujinga bila kukubali kwanza kwamba una ujinga wa kuuondoa.
Nimekubali yaishe ila bado sijaugundua huo ujinga! Taratibu nitaugundua kama upo kweli, kama haupo nani atabaki kuwa mjinga 🤷🏽‍♀️ Je utakubali kuitwa mjinga?
 
Nimekubali yaishe ila bado sijaugundua huo ujinga! Taratibu nitaugundua kama upo kweli, kama haupo nani atabaki kuwa mjinga 🤷🏽‍♀️ Je utakubali kuitwa mjinga?
Inawezekana pia usigundue kabisa huo mjinga wako kwa sababu wewe ni mjinga sana kiasi huwezi hata kugundua ujinga wako.

Yani ujinga wako unakuzuia kugundua ujinga wako.
 
Inawezekana pia usigundue kabisa huo mjinga wako kwa sababu wewe ni mjinga sana kiasi huwezi hata kugundua ujinga wako.

Yani ujinga wako unakuzuia kugundua ujinga wako.
Hujajibu swali hapo
 
Tatizo kama wewe mjinga utajuaje nimejibu au sijajibu?
984D9D4B-8F29-4824-AEE8-ACB65BDF7977.jpeg
 
This combines logical fallacies of argument from tradition and argument from dictionary.

Hicho kitabu chenyewe kimejaa ujinga mwanzo mwisho.

Narudia, wewe ni mjinga.
Punguza hasira!
 
Punguza hasira!
Hakuna hasira hapo, wewe ndiye nyoronyoro mtu akikuambia hapo umefanya ujinga huu, kimantiki unaitwa hivi, na kitabi chako kimejaa ujinga, badala ya kujihoji kama maneno yana ukweli, unafikiria kwa emotion na kuona anayekuonesha ujinga wako kafanya hivyo kwa hasira.

Hakuna hasira hapo, kuna ukweli tu.

Hizo logical fallacies umezifanya, na kitabu chako kimejaa ujinga.

Sasa kama kitabu chako kimejaa ujinga nikikuambia ukweli tu kuwa kitabu chako kinejaa ujinga, hasira iko wapi hapo?
 
Hakuna hasira hapo, wewe ndiye nyoronyoro mtu akikuambia hapo umefanya ujinga huu, kimantiki unaitwa hivi, na kitabi chako kimejaa ujinga, badala ya kujihoji kama maneno yana ukweli, unafikiria kwa emotion na kuona anayekuonesha ujinga wako kafanya hivyo kwa hasira.

Hakuna hasira hapo, kuna ukweli tu.

Hizo logical fallacies umezifanya, na kitabu chako kimejaa ujinga.

Sasa kama kitabu chako kimejaa ujinga nikikuambia ukweli tu kuwa kitabu chako kinejaa ujinga, hasira iko wapi hapo?
Kwa leo inatosha!
 
Haitoshi, sema tu unakimbia.

Hakuna aliyekupa cheo cha kuamua inatosha.
Siruhusiwi kuamua tena! Imani mpya hii..
Nakimbia kutusiwa basi, mengine ni majibu ya mtazamo tu na yanaeleweke!
 
Siruhusiwi kuamua tena! Imani mpya hii..
Nakimbia kutusiwa basi, mengine ni majibu ya mtazamo tu na yanaeleweke!
Bado mjinga hujaelewa hoja.

Unapokuwa katika mazungumzo na mtu, wewe huna mamlaka ya kusema haya mazungumzo yaishie hapa.

Kwa sababu hufanyi mazungumzo peke yako.

Wewe unaweza kusema inatosha hapa, mimi nikasema haitoshi, hujajibu maswali fulani.

Huelewi wapi?
 
Bado mjinga hujaelewa hoja.

Unapokuwa katika mazungumzo na mtu, wewe huna mamlaka ya kusema haya mazungumzo yaishie hapa.

Kwa sababu hufanyi mazungumzo peke yako.

Wewe unaweza kusema inatosha hapa, mimi nikasema haitoshi, hujajibu maswali fulani.

Huelewi wapi?
Hujajibu swali mada imegeuka ya ujinga haina maana tena!
 
Back
Top Bottom