Kiranga alikuwa anasali Kanisa Katoliki. Ilikuwaje akaanza kuamini hakuna Mungu?

Labda alisoma kwa makini historia ya kanisa akagundua mambo ndani ya kanisa .
 
kwaiyo kwa lugha allah anamakusudi yake watu wengine wasiuelewi uislam ili awa adhibu vikali?????? kuna mda huo naona dini inazuia binadamu kuwa kwa kina ili hali tulishapewa hofu
 
wakati ukisubiri uthibitisho kua aliesema yale maneno ni SNDANGUNJA(ambao najua haupo zaidi ya simulizi za Scars ,ww tupe ushahidi wa QUR AN ni maneno ya MUNGU/Mwenyezi Mungu.

natanguliza shukrani.
 
hahaaaa umeamua kuturn argument katika mtindo wa yy avae viatu vyako,ila nadhani hajaliona hili!.
 
hahaaaa umeamua kuturn argument katika mtindo wa yy avae viatu vyako,ila nadhani hajaliona hili!.
Mtindo wangu na wake haufanani sababu mimi naongelea uhalisia yeye analeta utoto ambao nafsi yake inashuhudia na inajulikana wazi na ndiyo maana maswali hajibu.

Nilichokuwa nakifanya kwake ni kuonyesha ujinga wake ulipo na ndiyo maana nikamwambia kazi yangu nimemaliza na hivi ndivyo nilivyo mimi.

Narudi katika swali lako.
 
wakati ukisubiri uthibitisho kua aliesema yale maneno ni SNDANGUNJA(ambao najua haupo zaidi ya simulizi za Scars ,ww tupe ushahidi wa QUR AN ni maneno ya MUNGU/Mwenyezi Mungu.

natanguliza shukrani.
Kwanza kabisa swali hili halikuanza leo kwani Mtume zama zake walio dhidi yake walikuwa wanamtaka ushahidi juu ya ukweli wa kile anachokisema,wakawa wanamuita kwa majina mengi mara mchawi mara mwenda wazimu,mara mzushi na yasiyokuwa hayo. Allah akawapa kazi (Challange) watu hao,akasema :

88. Sema: Wangeli kusanyika watu na majini ili walete mfano wa hii Qur'ani basi hawaleti mfano wake, hata wakisaidiana wao kwa wao.(al-Israa : 88)

Lakini haikuishia hapo akasema tena Allah mtukufu.

13. Au wanasema: Ameizua? Sema: Basi leteni Sura kumi zilizo zuliwa mfano wa hii, na waiteni muwawezao badala ya Mwenyezi Mungu, ikiwa mnasema kweli.

14. Na wasipo kuitikieni, basi jueni ya kwamba (hii Qur'ani) imeteremshwa kwa ujuzi wa Mwenyezi Mungu, na kwamba hapana mungu ila Yeye. Basi je! Nyinyi ni Waislamu? (Huud : 13-14)

Akasema tena Allah mtukufu.

23. Na ikiwa mna shaka kwa hayo tuliyo mteremshia mja wetu basi leteni sura moja ya mfano wake, na muwaite mashahidi wenu badala ya Mwenyezi Mungu, ikiwa mnasema kweli. (al-Baqarah : 23)

Huu ushahidi wa kwanza....

Naendelea ....
 
Endelea ila mpaka hapo sijaona ushahidi, zaidi naona "fasihi simulizi" na mapokeo, na unatumia reference ya kitabu nnachohoji authentication yake.
 
Ibilisi mtoto wa shetani, Endelelea tu kumpoteza ndugu yako, mtakutana pamoja Fii naari jahannam, mtakua kuni za motoni.,.
kwanini umtishie mtu asie amini katika mungu kuwa na jihannam ilihali hyo jihnamu akuna alieithibisha????? wengi mna amini katka sababu ya hofu ya jihannamu akipatikana mtu hana iyo hofu inaonekana shetani
 
wakati ukisubiri uthibitisho kua aliesema yale maneno ni SNDANGUNJA(ambao najua haupo zaidi ya simulizi za Scars ,ww tupe ushahidi wa QUR AN ni maneno ya MUNGU/Mwenyezi Mungu.

natanguliza shukrani.
Ushahidi huu apa chini....
Je, ww unaweza kuniambia Qur'an ni maandiko ya nani ?.... wenzako mpaka leo wameshindwa kunijibu
 
Attachments

Unaanzaje kumkosoa mtu kuonesha hayuko sahihi kwa kujitanabaisha kwamba wewe ndio uko sahihi kwa kitu ambacho umekiri kua haukijui maana yake?
 
Ushahidi huu apa chini....
Je, ww unaweza kuniambia Qur'an ni maandiko ya nani ?.... wenzako mpaka leo wameshindwa kunijibu
kwanza sio kweli kua hujajibiwa hilo swali

kwani ule ushahidi wa muumini mwenzako niliokupa siku ile ukionesha walioandika kuran haukuuona?

gusa link hii itakupeleka kwenye jibu ambalo ulipewa na ukalikimbia
 
kabla ya yote unathibitisha vipi kua hizo ni nukuu za Allah na sio kwamba ni mtu tu kaandika kua "Allah mtukufu akasema"
 
Endelea ila mpaka hapo sijaona ushahidi, zaidi naona "fasihi simulizi" na mapokeo, na unatumia reference ya kitabu nnachohoji authentication yake.
Umeelewa kilicho andikwa hapo ?

Ulichotakiwa kufanya wewe ukosoe kilicho andikwa humo au ufanye kama yaliyo semwa yafanywe humo.

Hapa unahitimisha ya kuwa huna hoja ya kupinga nilichokiandika bali hukitaki. Maana yake ni kuwa hata nikikupa shahidi elfu moja hutakubali.

Kwanini natumia kitabu hiki hiki kuthibitisha ukweli wake,sababu shahidi wa kwanza katika jambo husika ni nafsi ya kwanza.

Nakuuuliza swali vipi wewe huwezi kuwa shahidi namba moja juu jambo lako au kukuhusu wewe,yaani tukitaka kujua ukweli halisi kukuhusu wewe,tusikuulize wewe au tuwaulize wengine ? Sasa msiwe wajinga kiasi hiki,akili zenu mnatakiwa mzitumie vizuri,ukiandikiwa kitu kifikirie kwanza.

Lakini ushahidi wa pili ni kuwa,wanadamu ni wakosaji na tunafanya makosa,laiti kama Qur'aan ingekuwa si maneno ya Allah basi mngekuta kujichanganya kwingi na makosa mengi lakini,hukuti haya katika Qur'aan.

Anasema tena Allah :

82. Hebu hawaizingatii hii Qur'ani? Na lau kuwa imetoka kwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu bila ya shaka wangeli kuta ndani yake khitilafu nyingi. (an-Nisaa : 82)

Sasa nategemea ukija uje kunikosoa si unalia lia na utoe hoja za maana.

Naendelea...nakuja na ushahidi wa tatu.
 
kwanini umtishie mtu asie amini katika mungu kuwa na jihannam ilihali hyo jihnamu akuna alieithibisha????? wengi mna amini katka sababu ya hofu ya jihannamu akipatikana mtu hana iyo hofu inaonekana shetani

Pole sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…