Kiranga alikuwa anasali Kanisa Katoliki. Ilikuwaje akaanza kuamini hakuna Mungu?

Kiranga alikuwa anasali Kanisa Katoliki. Ilikuwaje akaanza kuamini hakuna Mungu?

Bart Ehrman nimemsoma, ukiwa na upeo wa kusoma waandishi kama huyu ukawaelewa bila kuleta figisu zile za ushabiki haya mambo ya imani za kidini utayaangalia kwa jicho la uelewa wa juu sana.

Tatizo hapa utataka mjadala na watu wengi ambao hawajasoma vitu kama hivi na jina kama la Bart Ehrman ndiyo kwanza wanalisikia.

Mimi mtu akinitajia kwamba kasoma waandishi kama hawa namuheshimu sana upeo wake, yani si lazima tukubaliane kila kitu, hata kama anatetea uwepo wa Mungu na Ukristo/Uislamu, akitetea kwa level ya kuweza kukanusha hoja zilizomo kwenye vitabu kama vya Ehrman anakuwa level tofauti na wafia dini wa kawaida wa JF ambao wamekaririshwa aya wanazipigania kwa identity tu hata kuzitetea kwa mantiki hawawezi.

Umenifurahisha sana kunitajia Bart Ehrman. Jamaa kasoma Princeton Theleogical Seminary, anaichambua Biblia kwa umakini wa mtu aliyesoma Priceton Theological Seminary, halafu anaikosoa.

Huyo Lawrence Brown sijamsoma nitamtafuta.
Pamoja mkuu mtafute huyo kwenye hivyo vitabu vyake viwili anza na misgoded then malizia goded ameweka maarifa mengi Sana..anakufanya uwe huru na confident kwenye kuchambua vitu....namsoma bart kwenye misquoting juses then ninalizie the lost christianity... Wanazi wengi wengi wa wa dini especially christianity nawauliza maswali kutoka kwenye bible hawana majibu ...lakini hata yale wanayojibu kila mmoja na mtazamo tofauti, and this is what makes me think why even nabii tito anakuwa na kanisa na bado akapata waumini ..what I mean is the reason why we have so many christian sects is due to different in perception about what is wrriten in the bible, mfano kunawanao kubali kwamba ndoa inaweza kutenganishwa kama alivyosema yesu kwa sababu ya zinaa lakini kunawaokwambia waliooana hawazini so kuachana ni kifo..yani dah
 
Mkuu, umeongea kitu muhimu sana.

Watu wengi matendo yao hayaoneshi kwamba wanaamini Mungu, na ironically, mara nyingine sisi tusioamini Mungu ndio tunaotenda matendo yanayoendana na imani za kuamini Mungu.

Nitakupa mfano mmoja mdogo tu.

Nilikuwa katika kundi moja, mtu mmoja akawa analalamika anaumwa katika hilo kundi.

Wale watu wa kwenye hilo kundi wote wanajinasibu na imani ya Mungu.Kila mmoja akawa anasema "tutakuweka kwenye maombi", na "Mungu atakusaidia".

Mimi siamini katika maombi wala Mungu kumsaidia mtu mwenye matatizo, kwa sababu siamini Mungu yupo. Nakwenda kwa falsafa za kwamba, matatizo ya mtu yatamalizwa na mtu, maombi ni kujiliwaza tu na Mungu hayupo.

Nikaguswa sana na kilio cha yule mtu, ni dada wote tunamjua, hana uwezo, na pale kwenye kikundi kuna watu wana uwezo wa kumsaidia wanajibalaguza kumuombea kwa Mungu.

Mimi nikatembeza muamala chapchap yule dada asaidiwe, nikamtumia rafiki yetu mwingine alikuwa Dar alikuwa na wasaa wa kuweza ku organize mgonjwa apelekwe hospitali.

Kuna rafiki yetu mwingine daktari aka arrange hospitali yule dada apokewe.

Ndani ya muda mfupi ule muamala wangu ukawa umeshawezesha yule mgonjwa akatiwe bima, aanze matibabu.

Huku wengine waliojikita kumuombea mgonjwa kwa Mungu wakawa kama wameona aibu, ukatembea mchango kusaidia mgonjwa.

To make a long story short, wale watu wanaoamini Mungu waliofundishwa usamaria mwema na kusaidia watu wenye matatizo wote walikuwa wanaangaliana wakati mwenzao, rafiki yao waliyemjua kwa miaka mingi anakaribia kufa. Na ninaposema anakaribia kufa si utani.Yule rafiki yetu daktari alikuja kutuambia kwamba pale tungechelewa kidogo tu habari ingekuwa tofauti sana.

Nikatokea gubegube tu hata siamini Mungu yupo, lakini kwa sababu siamini Mungu yupo hilo ndilo limenipa wajibu mimi kufanya kazi ya kusaidia mwenyewe bila kumsukumizia mzigo huo Mungu, kwa sababu najua Mungu hayupo. Nikaanzisha msaada chapchap.

Sasa hapo utaona wasioamini Mungu wanafanya usamaria mwema kirahisi kama vile wanaamini Mungu, wanaoamini Mungu wameendekeza ubinafsi.

Hii dunia kama watu wangekuwa kweli wanaamini Mungu yupo kama wanavyodai, maovu mengi sana yangetoweka.

Watu wanaiba mpaka misikitini. Waziri Mkuu katudanganya msikitini kwamba rais mzima anapiga kazi.

Halafu utaambiwa huyo naye anaamini Mungu.

Ni kweli anaamini Mungu?

Bora hata mimi nimesema siamini Mungu na sijadanganya msikitini kama yeye!
Kiranga hawachelewi kukuambia wewe ndio msaada uliyeletwa na Mungu baada ya maombi yao.. 😆😆

Religious people huwa wajinga sana
 
Nashangaa sana Karne ya 21 Bado Kuna mwafrika anaamini Hadith za wagiriki na wayahudi wa kale na kuendelea kuziamini
Hivi nyie watu amkeni muujue ukweli dini ni utapeli wa kale uliodumu miaka elfu nyingi kwenye bongo za watu

Amkeni mnapigwa wadau!

Enyi watu weusi amkeni narudia amkeni huyo Mungu wao hajawahi
kuwa mwema kwenu aisee
Daaaaaa inasikitisha watu kua brain washed!
[emoji22][emoji22][emoji25][emoji26][emoji26]
Unachotumia kiache kimekukataa mapema mno
 
Inakuwa sehemu ya maisha tu, mtu anakuwa muhunduliaji tu ili kito vunja sheria
Maarifa yanaweza kukufanya mwenye hekima au mpumbavu
Seminarini mnasali hadi sala inakuwa ni kawaida na sio Imani tena
 
Unachotumia kiache kimekukataa mapema mno
Hoja imeletwa kwamba dini ni hadithi za watu tu.

Kanusha hoja kama unaweza, vinginevyo hujajibu hoja, unaleta viroja.

Inawezekana ukawa na mafunzo muhimu ambayo watu wanaweza kufaidika nayo.

Kama ni hivyo, kwa jibu lako hilo umejidhulumu nafasi ya kutoa mafunzo hayo wewe mwenyewe, na pia umeidhulumu kadamnasi ya JF.
 
THE PROBLEM OF EVil
Kinachopelekea uwezekano wa kutendeka mambo ovu ya asili na yasio ya asili hapa duniani ni jambo la kutafakari sana juu ya Mungu anayefundishwa makanisani na misikitini kivipi? Kwa nini ameruhusu yatokee haya?,
Kwa namna moja au nyingine hizi dini ambazo kiundani zimekuwa ni taasisi ili kuhakikisha zinaendelea kuwapo zinaitaji msaada mkubwa sana kutoka kwa shetani ( shetani alipigwa mbinguni akatupwa shimoni, lakini ilibidi atolewe shimoni aje amshawishi eva, mbali na hivyo kapewa nguvu sawa na muumba! Yupo mahali popote) kiundani kabisa kahuna jambo jema wala baya jambo linakuwa jema au baya kutokana na tafsiri ya mwanadamu kutokana na tamaduni alizokulia hizi dini zinatoa tafsiri ambayo haipo sahii ili tu kujihakikishia ulaji ( sadaka, zaka , n.k).

Hata hivyo wanadamu hatupo sawa katika kung'amua mambo hivyo elimu ya dini ni kama basic ya juu ya ulimwengu wengi wanapenda au uwezo wao umeishia hapa katika kutafakari. Na mbaya wengi wanafikiri wamemaliza na wapo confident juu ya mambo ya dunia ( ignorance is a bliss)

Mbali na dini kuna misingi ambayo ni moral hii ni misingi ambayo mtu anajifunza kutoka kwa wazazi jinsi ya kushiriki na binadamu wenzake kama huna hiii ata ukisoma vitabu vingapi vya dini hutakuwa na heshima kwa binadamu mwenzako hata hutathmini dini au mawazo ya mwanadamu mwenzanko!
Hata hivyo tunapita ulimwengu una miaka bilioni 3.4 sisi uwepo wetu is very very small.
 
Ahsante sana mkuu kwa kutunza kumbukumbu.

Nilipata miito miwili kwa wakati mmoja, kuchagua kuwa Buddhist Monk milima ya Himalaya, au kwenda Wall St. kupiga dola.

Hapo nilikuwa natafsiri "The Dhammapada" na rafiki yangu Andy Nyerere kwenda Kiswahili.

Nikamuachia mikoba Andy mimi nikakwea pipa.

Mpaka leo sijui kama Andy alimaliza ile kazi, maana nilipotezea mawasiliano na Africa kwa muda fulani.

Kwa waliopenda kujua kwa nini niliamua kuacha kuamini uwepo wa Mungu, nitaweka kitabu kilichonishawishi mara ya mwisho kabisa, kinaitwa "The Philosophy of Religion: An Anthology".

Hususan kuna sehemu wanaongelea "the problem of evil".

Ni kitabu kizuri sana kina arguments nzuri na nyingi za kutetea uwepo wa Mungu na kupinga uwepo wa Mungu, ni falsafa pana sana.
Asante sana poti Nimekipata sasa Nakisoma
 
I will look for it and post it here.

I am an atheist.I am not anti-theist.

I can even see the reason for people believing in a God, I can explain these reasons, I even have empathy for believers.

I am also some kind of libertarian, so I am an advocate for freedom of religion as it was established by the Universal Declaration of Human Rights since December 10 1948.

President Kagame of Rwanda a few days ago announced that he will require pastors to have a degree in theology, I voiced my strong opposition to this move, as it infringes on the Human Rights of the people of Rwanda.

Even as I am an atheist, I will defend the freedom of religious people to worship as they want, justvas I will defend the freedom of atheist to reject religion.

The most important thing is freedom of choice and self determination.

I can't be anti-theist. I defend the right of religious people to worship their own God as they please. As long as they are not imposing their faith on me.

I do not acknowledge the existence of God outside of what if abstract thought experiments, particularly and starting with an all knowing, all loving and and all capable God such as the one preached about in the Bible and the Quran.

If atheism is the absence of belief in God. That is me.
.
If anti theism is the conscious, deliberate and almost activism opposition to theism. I am not that much of an anti theist. For starters, I do not initiate much in these conversations. An anti theist to me must initiate the agenda, not merely respond to something that is already in the conversation.

If you have noticed, I hardly start anything about God here. In fact I hardly start anything.

I just reply to people and air my views, especially by showing obvious contradictions.

Mostly the cognitive dissonance is so thick people shrug off these obvious contradictions.
hiki ndo kinaitwa kiburi cha uzima
kama vitu vyote tunavyoviona, hata nguo zina mtengenezaji wake, wewe ndo ukose mtengenezaji wako. na ufike hatua ya kusema hayupo
acha ujeuri ndugu
 
THE PROBLEM OF EVil
Kinachopelekea uwezekano wa kutendeka mambo ovu ya asili na yasio ya asili hapa duniani ni jambo la kutafakari sana juu ya Mungu anayefundishwa makanisani na misikitini kivipi? Kwa nini ameruhusu yatokee haya?,
Kwa namna moja au nyingine hizi dini ambazo kiundani zimekuwa ni taasisi ili kuhakikisha zinaendelea kuwapo zinaitaji msaada mkubwa sana kutoka kwa shetani ( shetani alipigwa mbinguni akatupwa shimoni, lakini ilibidi atolewe shimoni aje amshawishi eva, mbali na hivyo kapewa nguvu sawa na muumba! Yupo mahali popote) kiundani kabisa kahuna jambo jema wala baya jambo linakuwa jema au baya kutokana na tafsiri ya mwanadamu kutokana na tamaduni alizokulia hizi dini zinatoa tafsiri ambayo haipo sahii ili tu kujihakikishia ulaji ( sadaka, zaka , n.k).

Hata hivyo wanadamu hatupo sawa katika kung'amua mambo hivyo elimu ya dini ni kama basic ya juu ya ulimwengu wengi wanapenda au uwezo wao umeishia hapa katika kutafakari. Na mbaya wengi wanafikiri wamemaliza na wapo confident juu ya mambo ya dunia ( ignorance is a bliss)

Mbali na dini kuna misingi ambayo ni moral hii ni misingi ambayo mtu anajifunza kutoka kwa wazazi jinsi ya kushiriki na binadamu wenzake kama huna hiii ata ukisoma vitabu vingapi vya dini hutakuwa na heshima kwa binadamu mwenzako hata hutathmini dini au mawazo ya mwanadamu mwenzanko!
Hata hivyo tunapita ulimwengu una miaka bilioni 3.4 sisi uwepo wetu is very very small.
Nakubaliana nawewe maana ukienda nchi kama Saudi arabia wanawake wanajistili sana ila unakuta kesi za ubakaji ni nyingi ila kuna nchi bado watu wana achia matiti wazi mpaka leo lakini akuna baya linalo tendeka dhambi na dhani ipo akilini mwetu tu.
 
Quran inasema Allah kasema kuna watu Waislamu wasibishane nao, kwa sababu watu hao Allah mwenyewe kawaziba macho na masikio, kisha kawafanya mioyo yao iwe migumu kumuelewa.

Halafu, watu hao hao ambao Allah kawafanya macho yao yasimuone, masikio yao yasimsikie wala mioyo yao isimjue, wakishindwa kumjua Allah, kwa sababu Allah kawazuia wasimjue, Allah atawahukumu vikali kwa kutomjua.

Halafu unaambiwa Allah ni Mungu wa haki yote, upendo wote, ujuzi wote na uwezo wote.

Sasa mtu anayeamini Mungu huyu Allah, hataki reason wala logic, unaanzaje kubishana naye?
Ivi unaelewa ulichokiandika kweli ?

Ebu nipe proof wa hayo maneno unayosema,, nipe citations za ayah katika Qur'an zinazosema hvo !!
 
Hoja imeletwa kwamba dini ni hadithi za watu tu.

Kanusha hoja kama unaweza, vinginevyo hujajibu hoja, unaleta viroja.

Inawezekana ukawa na mafunzo muhimu ambayo watu wanaweza kufaidika nayo.

Kama ni hivyo, kwa jibu lako hilo umejidhulumu nafasi ya kutoa mafunzo hayo wewe mwenyewe, na pia umeidhulumu kadamnasi ya JF.
Unajuaje kwamba dini ni hadithi za watu tu ?
 
THE PROBLEM OF EVil
Kinachopelekea uwezekano wa kutendeka mambo ovu ya asili na yasio ya asili hapa duniani ni jambo la kutafakari sana juu ya Mungu anayefundishwa makanisani na misikitini kivipi? Kwa nini ameruhusu yatokee haya?,
Kwa namna moja au nyingine hizi dini ambazo kiundani zimekuwa ni taasisi ili kuhakikisha zinaendelea kuwapo zinaitaji msaada mkubwa sana kutoka kwa shetani ( shetani alipigwa mbinguni akatupwa shimoni, lakini ilibidi atolewe shimoni aje amshawishi eva, mbali na hivyo kapewa nguvu sawa na muumba! Yupo mahali popote) kiundani kabisa kahuna jambo jema wala baya jambo linakuwa jema au baya kutokana na tafsiri ya mwanadamu kutokana na tamaduni alizokulia hizi dini zinatoa tafsiri ambayo haipo sahii ili tu kujihakikishia ulaji ( sadaka, zaka , n.k).

Hata hivyo wanadamu hatupo sawa katika kung'amua mambo hivyo elimu ya dini ni kama basic ya juu ya ulimwengu wengi wanapenda au uwezo wao umeishia hapa katika kutafakari. Na mbaya wengi wanafikiri wamemaliza na wapo confident juu ya mambo ya dunia ( ignorance is a bliss)

Mbali na dini kuna misingi ambayo ni moral hii ni misingi ambayo mtu anajifunza kutoka kwa wazazi jinsi ya kushiriki na binadamu wenzake kama huna hiii ata ukisoma vitabu vingapi vya dini hutakuwa na heshima kwa binadamu mwenzako hata hutathmini dini au mawazo ya mwanadamu mwenzanko!
Hata hivyo tunapita ulimwengu una miaka bilioni 3.4 sisi uwepo wetu is very very small.
Kwanini Mungu asiruhusu yatokee hayo ?

Ivi unajua kusudi la kuumbwa mwanadamu ? Vp kuhusu kusudi la kuumbwa malaika unalijua ? Unaweza kutofautisha hayo makusudi mawili ?
 
Kuna mwamba anaitwa 911 kanisaidia kukiweka hapa kipo post namba 59 kama nakumbuka vizuri.

Soma vizuri sana Part 3 "The Problem of Evil" halafu tujadili kisomi zaidi ikiwezekana.

Kitabu kizuri sana kime cover mambo mengi sana ya kutetea na kupinga uwepo wa Mungu.
Thanks. Ngoja nikifuate
 
Kwanini Mungu asiruhusu yatokee hayo ?

Ivi unajua kusudi la kuumbwa mwanadamu ? Vp kuhusu kusudi la kuumbwa malaika unalijua ? Unaweza kutofautisha hayo makusudi mawili ?
Heheeeee taratibu mbona maswali mengi

Haya tulia nikupe majibu

-kuhusu malaika tafadhali acha kuniuliza vitu ambavyo ni vya kufikirika, sijawahi ona huyo kiumbe, na siamini kama kweli anaexist kwa ulimwengu huu AMBAO UPO REAL. jomba yaani ni sawa na kuniuliza kusud la kuumbwa babu chrismass au tooth fairy

-sitatofaitisha kati ya malaika na mwanadamu, nitatofsutishaje na kitu cha kufikirika, ivi ulikiwa wawaza nini kuuliza swali kama hilo. Yaani ni sawa na mtu anayeuliza tofauti ya john cena na thano.... Upo

-huwezi kuja kichwa kichwa unakuja na kuniuliza swali ambalo toka enzi na enzi halina jibu juu ya dhumuni la uwepo wetu hapa duniani ukitegemea ntakupatia jibu, ivi unafikiri jibu la hilo swali linaweza kuenea kwenye server za jamii forum, xiiu
- asiruhusu ..... Hayo tafuta sentensi zako acha kuparamia na kugeuza sentensi UNAFIKIRI NAFANYA MZAHAAA HAPAA
 
Mi najua kama kuna pepo kweli basi kiranga ataingia unajua kwanini?
Wengi wanafata dini lakin hawafati yaliyomo ktk dini that's why watu wengi no waislam na wakrtso na wayahud na wabudha lkn wizi dhuluma kuua kuiba kubaka kutapeli duniani haya mambo hayaishi
Lakin mtu kama kiranga na wengine wasioamni wanakuwa na utu na kuthamini wenzao
 
Back
Top Bottom