Kiranga alikuwa anasali Kanisa Katoliki. Ilikuwaje akaanza kuamini hakuna Mungu?

Kiranga alikuwa anasali Kanisa Katoliki. Ilikuwaje akaanza kuamini hakuna Mungu?

Nadhani wanaopinga uwepo wa Mungu wanashindwa kutumia akili zao vizuri. Mungu ni mkuu kuliko logical reasoning ya mwanadamu.

Huwezi uka reason kwa akili ya kibinadamu ukamuelewa Mungu 100%. Tunamjua Mungu kadri anavyojifunua kwetu ktk maandiko na mazingira yanayotuzunguka.

Ukikaa ukatulia na kuwaza vizuri utagundua tu kuwa yuko Mungu ijapokuwa haonekani kwa macho kwa sasa.
hayo maandiko kaandika nani?.. Unahisi yesu atakua anajua kua kuna biblia? au Muhammad ataweza kuisoma Qur an bila msaada mtu??

hayo maandiko una uhakika gan kua ni ya kweli?.(am question the authenticity)
 
Wanasayansi karibia wote wanakubali kwamba sayansi inaweza kuelezea ulimwengu tangu tukio big bang tu na si zaidi ya hapo. Hata kilicho triger hiyo big bang bado ni mjadala mkubwa kati yao

Wanasayansi wachache kama Lawrence Krauss wameibuka na imani ya ulimwengu ulioubuka pasipo chanzo cha kitu chochote.
Naiita imani kwa sababu katika imani ndipo watu wanaamini ulimwengu ulioumbwa pasipo kuwepo na kitu chochote kwa kuanzia.

Hadi hapo sayansi itakapoweza kujibu swali la nini kilikuwepo kabla ya big bang na chanzo cha uhai ni nini dini na imani vitabaki vyanzo vikuu vya kujaza ombwe hilo.
Kwanza kabisa, kitu kuwa na mtengenezaji wake si lazima mtengenezaji wake awe Mungu.

Pili, dhana nzima ya kusema Mungu asiyeonekana yupo, kwa sababu kika kinachoonekana kina mtengenezajinwake ni kichaa cha aina fulani.

Yani ni bora ungesema habari ya vitu vinavyoonekana kuhalalisha uwepo wa Mungu anayeonekana.

Zaidi, kudai kila kitu kinachoonekana kinq mtengenezaji wake, hujaongelea visivyoonekana.

Na unaonesha hujasoma Quantum Physics ambayo inavunja cause and effect.

Umeonesha ujinga wako.
 
Wanasayansi karibia wote wanakubali kwamba sayansi inaweza kuelezea ulimwengu tangu tukio big bang tu na si zaidi ya hapo. Hata kilicho triger hiyo big bang bado ni mjadala mkubwa kati yao

Wanasayansi wachache kama Lawrence Krauss wameibuka na imani ya ulimwengu ulioubuka pasipo chanzo cha kitu chochote.
Naiita imani kwa sababu katika imani ndipo watu wanaamini ulimwengu uliombwa pasipo kuwepo na kitu chochote kwa kuanzia.

Hadi hapo sayansi itakapoweza kujibu swali la nini kilikuwepo kabla ya big bang na chanzo cha uhai ni nini dini na imani vitabaki vyanzo vikuu vya kujaza ombwe hilo.
Msingi wako mzima wa kuuliza swali wa "nini kilikuwapo kabla ya big bang" unatokana na uzoefu wako wa sasa, ambao upo katika time.

Time supposedly ina past, present and future. Causality inaenda kwa vitu vinavyoanza mwanzo kusababisha vitu vinavyokuja baadaye.

Sasa ukisoma Physics sana, hususan Quantum Physics unakutana na habari kwamba time si kitu fundamental.

Katika multiverse theory kuna universes hazina time, nyingine zina multi dimensions za time, nyingine zina reversible time.

Katika universe yetu hii, from the perspective of a ray of light moving at the speed of light in a vacuum, time is standing still.

Kwa universe yetu hii, per Big Bang Theory, utasoma kwamba time nayo ilianza takriban miaka bilioni 13.8 iliyopita.

Na ukiuliza nini kilikuwapo kabla ya time kuanza ni sawa na kuuliza rangi ya wimbo wa taifa ni rangi gani, au kuuliza "what is north of the north pole?", swali halina jibu kwa sababu msingi wa kuulizwa kwake una makosa.

Unahitaji the right perspective kabla ya kuanza kuuliza maswali katika level hiyo.

Unahitaji kusoma sana hesabu na theoretical physics, uzame sana kwenye Einstein's Relativity na Quantum Physics.

By the way thanks for mentioning Krauss, ninavyo vitabu vyake. Umenifanya niamke niangalie bookshelf nimekutana na kitabu chake "Quintessence :The Mystery of Missing Mass In The Universe". Ninavyo vingine hata sivioni viko wapi.Too many books.

Nikijibizana na mtu ananitajia wandishi kama hawa napata nafuu kwa kujua huyu anasoma waandishi wa kueleweka, si kuishia kunukuu Biblia na Quran tu.
 
Back
Top Bottom