Kiranga alikuwa anasali Kanisa Katoliki. Ilikuwaje akaanza kuamini hakuna Mungu?

Kiranga alikuwa anasali Kanisa Katoliki. Ilikuwaje akaanza kuamini hakuna Mungu?

Sasa nikidai uthibitisho wa kuhakiki hilo jambo kua ni kweli unaweza kunipa?
Hilo jepesi sana,ila litafata baada ya wewe kukiri ya kuwa huwezi kukosoa nilichokiweka na Qur'aan ni maneno ya Allah.
 
Lakini hii si circular reasoning sababu matini inaelezea wazi nini katika ithibati. Kwamba ni majibu kwa wale walio kuwa wanaikana. Sasa "content" iko wazi na sababu iko wazi,sasa ili uwe na hoja unatakiwa ufikiri kwanza kisha ubatilishe yaani uonyeshe uongo wa maneno hayo. Kinyume na hapo unakuwa huna hoja zaidi ya kupoteza muda.
kutokuweka kwako uthibitisho kunaonesha ni jinsi gani jambo hilo ni uwongo

weka uthibitisho hapa kuonesha yale ni maneno ya allah na sio watu tu wameandika
 
Safi kabisa,nakubaliana nae kwamba ametumia andiko lake,sasa kinachofata tunakuja kujadili ukweli wa hicho alichokoandika je ni kwali ushahidi.
Ujadili ili kujua nini wakati ushakubali kua ni kweli?

Kwani ulivyokubali kua kweli maneno hayo ni ya mungu ulikua umekubali kwa uthibitisho au ulikubali kwa namna gani?
 
Nakuacha na swali,unaamini uwepo wa kina Aristosto au Plato au Socrates au George Washington au Isaac Newton ? Kipi kimekufanya uamini uwepo wao kama unakubali waliwahi kuwepo ?

Yaani nje ya ukosoaji huwezi kuwa na hoja katika hili,matini ziko wazi,jadili andiko hilo,usikimbie.

Nasubiri ukosoaji .... hili najua huwezi utaishia kukimbia na sisi hatulei ujinga.

Qur'aan ni maneno ya Allah kwa shahidi mbili nilizo zitoa na ziko nyingi,hizi zinakutosha sababu naona unazikimbia na ikionekana haja ya kuongeza shahidi nyingine naziongeza.

Nipo....
hayo mengine ni irrelevant jibu lolote hapo liwe negative au positive in your view halitathibitisha chochote kuhusu ukweli wa kuran

Unajuaje kua kuran imesema ukweli?
 
Jibu maswali niliyo kuuliza.

Pili,ithibati nimekupa,unachotakiwa wewe kukosoa nilicho kiweka sababu kila kitu kipo wazi.
Hakuna ulipoweka uthibitisho ila kuna sehemu umeweka aya ya kuran ikidai ni maneno ya allah....hizo ni claims zinahitaji kuthibitishwa na hujaweza kuthibitisha hilo
 
Mkuu umeona jinsi ambavyo unajaribu kupoteza lengo la swali husika? ok labda niliweke kivingine

1. Wewe ni binadamu mwenye imani ya (Atheism) au wewe ni Atheist?. Atheism in kuamini hakuna uwepo wa Mungu.
bado haujawa specific imani ya Atheism mimi siijui ni kitu gani
2. Unataka nilete uthibitisho wa kitu gani? (nimeuliza hivi kwasababu wewe ndie uliniambia nilete uthibitisho kwenye post #463)
Namimi nikakujibu vile kwasababu hapo awali ulidai ulitupa uthibitisho ila sisi hatukua tayari kuupokea huo uthibitisho.

Nimekuomba unipe uthibitisho, unaniuliza tena uthibitisho wa kitu gani. nikueleweje?
Ulikua unakusudia uthibitisho wa kitu gani ambao sisi hatupo tayari kuupokea?

3. Unaamini katika sayansi? (Bado hujanijibu)

Kwahiyo, vipengele hivyo bado haujanijibu badala yake umeniuliza tena mimi maswali.
Sijibu tu ilimradi nataka nijibu swali ambalo nimelielewa na wote tukubaliane kila point tunayoipita

Unapouliza "unaamini katika sayansi?" binafsi umeniacha njia panda kwasababu umetumia neno tata (kuamini/amini) ambalo sijajua target yako katika swali lako ni nini. nimeomba unipatie ufafanuzi wa hilo neno nikujibu kwa ufasaha swali lako
 
kutokuweka kwako uthibitisho kunaonesha ni jinsi gani jambo hilo ni uwongo

weka uthibitisho hapa kuonesha yale ni maneno ya allah na sio watu tu wameandika
Labda uniambie niweke mara ngapi ?

Nilikuuliza swali hivi tukitaka kujua ukweli hasa kuhusu wewe ni vyema kuuliza wengine au tuanze na wewe ? Hili umelikimbia.

Mpaka sasa nimeweka ithibati mbili,kwanza kuonyesha ya kuwa jambo hili halijaanza kwenu bali tangu mtume yuko hai wale waliokuwa dhidi yake walimuuliza maswali hayo,na huo ndiyo ukawa ushahidi. Kadhalika nilikwambia ya kuwa kwa ufinyu wako wewe na kukimbia kwako maswali,nilisema ya kuwa hizi shahidi mbili zinakutosha sababu hujakosoa hata moja (hili najua huwezi), nikasema tena ya kuwa nikiona haja ya kuongeza shahidi nyingine nitafanya hivyo na hizo zitaanzia namba tatu kuendelea.

Nikajua muda huu ungekuwa unajadili matini ya aya,baada ya mimi kukuwekea aya hizo.
 
Hakuna ulipoweka uthibitisho ila kuna sehemu umeweka aya ya kuran ikidai ni maneno ya allah....hizo ni claims zinahitaji kuthibitishwa na hujaweza kuthibitisha hilo
Aya zinasemaje ? Sasa kile kilichoandikwa ndiyo ushahidi wenyewe tunasema matini ya aya. Sasa kosoa,sababu hizo aya zinathibitisha ya kuwa Qur'aan ni maneno ya Allah.

Kuna madai na kuna hoja na ubainifu,madai ni kama yenu ya kwamba Mola hayupo na ushahidi hamna,ila aya ni hoja na ubainifu unao jibu zile tuhuma.

Ndiyo maana nilikuuliza wewe unaamini vipi kama Newton aliwahi kuishi au Galileo Galilei au George Washington ? Hili ukalimbia. Aya inasema wazi kabisa kama Qur'aan si maneno ya Allah basi mtengeneze mfano wake au walau kipande na muitane na mashahidi wawepo ? Hili hawakuweza wakubwa zenu kwenu hili muhali. Yaani ni sawa unaiona nyumba kisha unaomba ushahidi wa kuonyesha hiyo nyumba imejengwa.
 
Labda uniambie niweke mara ngapi ?
hujaweka uthibitisho umeweka madai. nataka uweke uthibitisho
Nilikuuliza swali hivi tukitaka kujua ukweli hasa kuhusu wewe ni vyema kuuliza wengine au tuanze na wewe ? Hili umelikimbia.
irrelevant
Mpaka sasa nimeweka ithibati mbili,kwanza kuonyesha ya kuwa jambo hili halijaanza kwenu bali tangu mtume yuko hai wale waliokuwa dhidi yake walimuuliza maswali hayo,na huo ndiyo ukawa ushahidi.
inawezekana wao waliona huo ila hiyo kwangu siipi nafasi kua ni kigezo cha mimi kukubaliana na hizo porojo eti kwasababu wazee wa zamani walikukubali.

Pengine huo ni muendelezo wa habari za kutungwa kuwafanya watu wasio wadadisi kukubali kiwepesi kwasababu kitabu kimesema wapo waliokua wakipinga kabla yao na hatimaye wakakubali

Unajuaje kuran imesema ukweli?
Kadhalika nilikwambia ya kuwa kwa ufinyu wako wewe na kukimbia kwako maswali,nilisema ya kuwa hizi shahidi mbili zinakutosha sababu hujakosoa hata moja (hili najua huwezi)
Shahidi hizo umezipimaje kujua zimeongea ukweli?

nikasema tena ya kuwa nikiona haja ya kuongeza shahidi nyingine nitafanya hivyo na hizo zitaanzia namba tatu kuendelea.

Nikajua muda huu ungekuwa unajadili matini ya aya,baada ya mimi kukuwekea aya hizo.
hujathibitisha ukweli wa kuran
 
hujaweka uthibitisho umeweka madai. nataka uweke uthibitisho

irrelevant

inawezekana wao waliona huo ila hiyo kwangu siipi nafasi kua ni kigezo cha mimi kukubaliana na hizo porojo eti kwasababu wazee wa zamani walikukubali.

Pengine huo ni muendelezo wa habari za kutungwa kuwafanya watu wasio wadadisi kukubali kiwepesi kwasababu kitabu kimesema wapo waliokua wakipinga kabla yao na hatimaye wakakubali

Unajuaje kuran imesema ukweli?

Shahidi hizo umezipimaje kujua zimeongea ukweli?

hujathibitisha ukweli wa kuran
Niweke mara ngapi hili ndiyo swali langu kwa sasa.
 
Aya zinasemaje ?
unajuaje zimesema kweli?
Sasa kile kilichoandikwa ndiyo ushahidi wenyewe tunasema matini ya aya. Sasa kosoa,sababu hizo aya zinathibitisha ya kuwa Qur'aan ni maneno ya Allah.
umeuhakiki vipi kujua ushahidi huo umesema kweli?
Kuna madai na kuna hoja na ubainifu,madai ni kama yenu ya kwamba Mola hayupo na ushahidi hamna,ila aya ni hoja na ubainifu unao jibu zile tuhuma.
aya mbona nazo hazina ushahidi kujua kama zimesema ukweli?

thibitisha hilo kwanza
Ndiyo maana nilikuuliza wewe unaamini vipi kama Newton aliwahi kuishi au Galileo Galilei au George Washington ? Hili ukalimbia.
irrelevant, hakuna correlation yeyote kati ya mimi kuwajua/kutowajua ambako kutasaidia kuthibitisha hayo madai ya kuran.
Aya inasema wazi kabisa kama Qur'aan si maneno ya Allah basi mtengeneze mfano wake au walau kipande na muitane na mashahidi wawepo ? Hili hawakuweza wakubwa zenu kwenu hili muhali. Yaani ni sawa unaiona nyumba kisha unaomba ushahidi wa kuonyesha hiyo nyumba imejengwa.
Sipingi kwamba aya haijasema hivyo, ila nachotaka mimi ni kuhakiki hizo aya nijue ukweli kwa kuletewa uthibitisho
 
Maisha ni fumbo ambalo hakuna ata atakayelifumbua milele, kuhusu uwepo wa MUNGU, nguvu za MUNGU, na nani aliyemuumba MUNGU na kumpa uwezo wote, je' kabla ya vyote ivyo yaani MUNGU kulikuwepo na nin.
 
unajuaje zimesema kweli?

umeuhakiki vipi kujua ushahidi huo umesema kweli?

aya mbona nazo hazina ushahidi kujua kama zimesema ukweli?

thibitisha hilo kwanza

irrelevant, hakuna correlation yeyote kati ya mimi kuwajua/kutowajua ambako kutasaidia kuthibitisha hayo madai ya kuran.

Sipingi kwamba aya haijasema hivyo, ila nachotaka mimi ni kuhakiki hizo aya nijue ukweli kwa kuletewa uthibitisho
Kila kitu kimejielezea humo.
 
Maisha ni fumbo ambalo hakuna ata atakayelifumbua milele, kuhusu uwepo wa MUNGU, nguvu za MUNGU, na nani aliyemuumba MUNGU na kumpa uwezo wote, je' kabla ya vyote ivyo yaani MUNGU kulikuwepo na nin.
watakwambia alikuepo tuu
 
Umepotea wewe Mkinga.

Mimi nimejaa hapa na bluetooth mpaka kwenye mswaki.

Ukiona nakosea spelling hapa ujue nilikuwa na type kwa command za kupigia mswaki.
Sawa mkinga Kuna ishu za quantum physics nlkua nasoma znanichanganya mtakushirikisha mkinga
 
Sawa mkinga Kuna ishu za quantum physics nlkua nasoma znanichanganya mtakushirikisha mkinga

"If you think you understand quantum mechanics, you don't understand quantum mechanics."

- Richard Feynman.
 
Back
Top Bottom