Kiranga alikuwa anasali Kanisa Katoliki. Ilikuwaje akaanza kuamini hakuna Mungu?

Kiranga alikuwa anasali Kanisa Katoliki. Ilikuwaje akaanza kuamini hakuna Mungu?

Unaniuliza hayo maswali wakati wewe ni atheist,si ujinga huo.
Kuuliza maswali ni ujinga? Au kuuliza maswali wakati ni atheist ni ujinga?

Swali litakuwaje ujinga wakati swali ndilo kitu cha kuondoa ujinga?
 
Kuna kitu chochote ambacho kipo kwenye ulimwengu unaoonekana kwa macho kinachoweza kuwepo bila kuwa na muundaji?
Ukisema muundaji una kusudia nini?

Unapo taja "muumbaji" hiyo ni dhana ambayo inapaswa kuambatana na uthibitisho usio kua na makisio kuonesha kweli ni muumbaji wa hivyo vitu

Mfano simu imeundwa, hatusemi imeundwa eti kwasababu ina exist hapana, tunasema imeundwa kwasababu muundaji tuna mjua na anathibitishika kua yupo

Lakini vipi nikisema bahari imeundwa, tunaweza tukapata uthibitisho wa huyo muundaji kama ambavyo tumempata huyo muundaji wa simu?

Kama itashindikana kuwepo uthibitisho wa muundaji wa bahari tuta hitimisha vipi kwenye hoja ya kujua nafasi ya muundaji katika ulimwengu unao onekana kwa macho?
 
Mara nyingi nimekuwa nikiwaza huyu member hapa JF atakuwa alikutana na incident iliyomfanya akamchukia Mungu.

Hapa anaeleza namna alivyokuwa anasali na Nyerere pale St Peters

My take, huyu anahitaji kuombewa ili amrudie muumba wake.
Mshana Jr
Hivi Kirang'a bado anavita na Mwenyezi Mungu?
 
Umejibu vizuri kwamba haujui kitu chochote kilichopo kwenye ulimwengu unaoonekana kwa macho ni lazima kiwe na muudaji.

Sasa nakuuliza tena hivi:-

Unaweza kuniambia vitu vifuatavyo vilitokeaje tokeaje(formation)?
1. Jua na nyota zote angani
2. Vimondo vyote angani
3. Sayari zote
4. Madini yote katika ardhi ya sayari dunia
5. Gas katika ardhi ya sayari dunia
6. Mafuta katika ardhi ya sayari dunia
7. Upepo/hali ya hewa na majira ya mvua
8. Bahari, mito na maziwa katika sayari dunia
9. Milima na mabonde katika sayari dunia
10. Miti na mimea ya aina zote katika sayari dunia
11. Ndege wa aina zote katika sayari dunia
12. Samaki wa aina zote kwenye mito, maziwa na bahari
13. Wanyama wa aina zote wa kufungwa na mwituni
14. Binadamu

NB: Nasubiri uniambie vilitokeaje tokeaje(formation)
Tunaweza kujifunza vyanzo vya vitu ndani ya ulimwengu wetu kupitia uchunguzi,

Hivyo ni vitu ambavyo bado vina chunguzwa, na kucheleweshwa kwa majibu hakutoi mwanya wa kulazimisha jibu ambalo halijapitia uchunguzi kua ndio jibu sahihi
 
Nina uhakika chochote(Matter) kilichopo kwenye ulimwengu(Space) huu tunaoishi unaoonekana kwa macho ni lazima kiwe na muda(Time) kilichoundwa na muundaji.

Hakuna chochote kinachoweza kuwepo bila kuundwa na muundaji katika ulimwengu huu unaoonekana kwa macho. Nakupa mfano tena wewe Emmanuel ni (Matter) una muda ulioundwa(Time) na aliekuunda amekuandalia mazingira rafiki uishi katika sayari hii dunia(Space). Vivyo hivyo na vitu vingine vyote (living and non living things)

Hivyo ninachokuuliza nina uhakika nacho, naomba unipe majibu niliyokuuliza kama haufahamu au hauna majibu pia niambie.

NB:Naendelea kusubiri majibu niliyokuuliza.
Weka hizo calculations zinazoonesha kivyovyote vile ni lazima kuwepo na muundaji, nioneshe muundaji wa bahari ni nani, weka uthibitisho ambao unapimika

Usiweke probability na assumptions zakufikirika nataka majibu clearly ambayo tunaweza tukaya hakikisha.

Halafu ukiweza hilo (kitu ambacho najua huwezi) uniambie huyo muundaji aliundwa na nani na muundaji wa muundaji aliundwa na nani nakuendelea
 
Haya maelezo haukunipa Mkuu, hukuniambia kama haujui formation ya hivyo vitu ndio maana nimeendelea kutaka majibu. Hivyo kwa maelezo yako haya itoshe kusema umekiri kwamba haujui hivyo vitu vimetokeaje?(formation) si ndio?

Ili tuendelee na mada.
Kwani kila kilichopo lazima kiwe na chanzo?
 
Nina uhakika hakuna chochote(Matter) kinachoweza kutokea katika muda(Time) husika na kuwepo katika ulimwengu(Space) unaoonekana kwa macho bila kuwa kimeundwa na muundaji.

Hakuna gari/pikipiki/juice/baiskeli n.k(Matter) linaloweza kutokea katika muda(Time) husika na kuwepo sehemu(Space) bila ya gari/pikipiki/juice/baiskeli n.k hiyo kuundwa na muundaji
Kwa maelezo yenu believer, Mungu sio matter?

Maana tunajua alivyielezewa kwenye vitabu vyenu, ana mikono yakushika upanga ukatao kuwili, ana macho yanayoangalia dhambi zenu, ana masikio ya kusikia shida zenu, pia ana matako ya kukalia kiti cha enzi

So Mungu naye unayemuamini anahitaji muumba maana ana sifa kama zetu (matter) hivyo hawezi kutokea bila chanzo, nani aliyemuumba?
 
Kuuliza maswali ni ujinga? Au kuuliza maswali wakati ni atheist ni ujinga?

Swali litakuwaje ujinga wakati swali ndilo kitu cha kuondoa ujinga?
Ndio maana nikakutaja kabisa kuwa wewe atheist kuuliza maswali kama hayo ni ujinga, wewe ambaye ni mpingaji wa uwepo wa Mungu utaondoaje ujinga kwa kuuliza Mungu ni nini?

Ndio maana hii mijadala huwa haisogei inazunguka palepale tu kwa sababu kama hizo za kuulizana maswali yaleyale kila siku.
 
Kwa maelezo yenu believer, Mungu sio matter?

Maana tunajua alivyielezewa kwenye vitabu vyenu, ana mikono yakushika upanga ukatao kuwili, ana macho yanayoangalia dhambi zenu, ana masikio ya kusikia shida zenu, pia ana matako ya kukalia kiti cha enzi

So Mungu naye unayemuamini anahitaji muumba maana ana sifa kama zetu (matter) hivyo hawezi kutokea bila chanzo, nani aliyemuumba?

Wewe huyo Mungu umemuona hadi useme ana sifa kama zetu? mfano ni binaadamu gani mwenye macho ya kuona kila kitu kama ambavyo huyo Mungu anaona dhambi zetu?
 
Wewe huyo Mungu umemuona hadi useme ana sifa kama zetu? mfano ni binaadamu gani mwenye macho ya kuona kila kitu kama ambavyo huyo Mungu anaona dhambi zetu?
Umeelewa kilichoandikwa?

Hapo zimezungumziwa sifa za mungu kwa speculations zangu au holy scriptures?
 
Kwani wewe akili yako inakupa jibu gani au wewe unaonaje?
Hilo ni swali kwa yeyote anayedai kilichopo kina chanzo, nawewe ni miongoni mwa hao watu wanaosema kila kilichopo kina chanzo?
 
Umeelewa kilichoandikwa?

Hapo zimezungumziwa sifa za mungu kwa speculations zangu au holy scriptures?
Wewe ndio uliyesema ana sifa kama zetu kitu ambacho ni kinyume na hivyo vitabu vinavyosema, hayo macho au mikono ya Mungu inayosemwa je we unayo idea inafananaje hadi ulinganishe na sisi binaadamu?
 
Hilo ni swali kwa yeyote anayedai kilichopo kina chanzo, nawewe ni miongoni mwa hao watu wanaosema kila kilichopo kina chanzo?
Nimekuuliza swali ningependa kujua jibu lako kwanza?
 
Ndio maana nikakutaja kabisa kuwa wewe atheist kuuliza maswali kama hayo ni ujinga, wewe ambaye ni mpingaji wa uwepo wa Mungu utaondoaje ujinga kwa kuuliza Mungu ni nini?

Ndio maana hii mijadala huwa haisogei inazunguka palepale tu kwa sababu kama hizo za kuulizana maswali yaleyale kila siku.

Naweza kuondoa ujinga kwa wanaofuatilia mjadala kwa kuuliza Mungu ni nini, wakafuatilia majibu kimantiki na kuona wenyewe kama Mungu yupo kutokana na majibu na mjadala.

Mpaka sasa hujajibu Mungu ni nini na kwa nini ni lazima Mungu yupo na habari za kuwapo kwake si hadithi za uongo tu.

Kwa nini unaogopa au unashindwa kujibu swali hili?

Mungu ni nini?

Kwa nini ni lazima yupo na habari za kuwapo kwake si hadithi za uongo tu?
 
Wewe ndio uliyesema ana sifa kama zetu kitu ambacho ni kinyume na hivyo vitabu vinavyosema, hayo macho au mikono ya Mungu inayosemwa je we unayo idea inafananaje hadi ulinganishe na sisi binaadamu?
Kwani ukisikia neno jicho unapata taswira gani nje ya sense organ inayo husisha na kuona?

Au unataka kusema umeelewa tofauti kua jicho lililokusudiwa hapo ni some sort of sex?
 
Nimekuuliza swali ningependa kujua jibu lako kwanza?
Jibu linategemeana na wewe unavyo amini hizi dhana mbili

Kila kilichopo ni lazima kiwe na chanzo, au sio lazima kuwa na chanzo?

Ukijibu hapo nitakupa jibu
 
Kwani ukisikia neno jicho unapata taswira gani nje ya sense organ inayo husisha na kuona?

Au unataka kusema umeelewa tofauti kua jicho lililokusudiwa hapo ni some sort of sex?
Ndio maana nauliza ni jicho gani la binaadamu lenye kuweza kuona mambo ya watu wote? kwa sababu jicho la binaadamu wote tunalijua lilivyo sasa kama huyo Mungu nae ana jicho kama hili letu iweje tuambiwe aweze kuona kila jambo la binaadamu kwa macho kama haya yetu?
 
Back
Top Bottom