Kiranga na jamaa zake wanaweza wasionekane kwenye thread mbalimbali lakini uzi wowote unaomsifia Mungu huwakosi

Wewe Kama Imani Yako inategemea watu wengine ushafeli Imani si lazima ifuatwe na kila mtu ni neema ya Mungu watu kuwa katika Imani, usitishike na kelele maana miruzi mingi hupoteza mbwa
 
Wewe jomba una busara ile laana.
 
Kuna wengi wamejificha kwenye kichaka cha kumwamini Mungu lakini umbea wao, ufiraji wao, umalaya wao........

Ogopa sana wale wasiochelewa kanisani wana balaa.
 
Lakini kwanini Mungu akuzwe kuliko uwezo wake?

Ni mwenye huruma lakini hatujawahi kuona akihurumia walemavu waliotapakaa dunia nzima, Amewapa ulemavu na pia wengi wao amewapa ufukara means huyo Mungu hana huruma.

Je, Ni wagonjwa wangapi wamefariki kwa kukosa pesa?

Je, Ni watoto wangapi wasiokuwa na hatia wamefariki katika vita?

Orodha ni ndefu na huenda huyo Mungu anakuzwa kuliko uwezo wake. Au anasikia ila uwezo wake ni mdogo.
 
Umesema huna ufahamu kuhusu origin ya watu na viumbe wengine na bado unabisha kuhusu uwepo wa Mungu, kwa nini usiseme kwamba huna ufahamu pia kuhusu uwepo wa Mungu badala ya kuhitimisha kwamba Mungu hayupo? wee jamaa chenga sana.
 
Umesema huna ufahamu kuhusu origin ya watu na viumbe wengine na bado unabisha kuhusu uwepo wa Mungu, kwa nini usiseme kwamba huna ufahamu pia kuhusu uwepo wa Mungu badala ya kuhitimisha kwamba Mungu hayupo? wee jamaa chenga sana.
Unaniuliza uelewe au unanisimanga?

Naweza kusema Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo kwa sababu ya contradiction iliyopo katika Epicurean paradox.

Unaelewa Epicurean Paradox ni nini?

Kwani nikiulizwa hivi.

What is the square root of 4?

Nikaajua kuwa the square root of 4 must be less than 4.

Siwezi kujua kuwa 10 haiwezi kuwa square root of 4 kabla hata sijajua square root of 4 ni nini, kwa sababu 10 ni kubwa kuliko 4 na hivyo haiwezi kuwa square root ya 4?

Kwani siwezi kujua jibu hili si sahihi, wakati natafuta jibu sahihi, bila kujua jibu sahihi?

Mbona unafanya logical non sequitur fallacy?

Unaelewa ninachoandika au unaona kizunguzungu?
 
Kama kujua origin ya watu kumekutoa jasho, nilitegemea uamini uwepo wa nguvu kubwa zaidi ambayo inaweza kuhusika na origin ya watu ambayo huijui, ambayo ndo tunaita Mungu......naona mdogo mdogo umeanza kuelewa.
 
Kama kujua origin ya watu kumekutoa jasho, nilitegemea uamini uwepo wa nguvu kubwa zaidi ambayo inaweza kuhusika na origin ya watu ambayo huijui, ambayo ndo tunaita Mungu......naona mdogo mdogo umeanza kuelewa.
Hapana,

Unachanganya mambo.

Inawezekana kujua origin ya watu kunanitoa jasho kwa sababu Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Angekuwapo, angempa kila mtu jibu la kila swali analolipata.

Angekuwapo, kwa sifa zake hizo, kusingekuwa na swali lolote ambalo watu wanajiuliza na kukosa jibu lake.

Nimekuuliza, unajua Epicurean Paradox ni nini?

Hujajibu.

Kwa nini hujajibu?
 
Sorry kwa kuwa nje ya Mada..huwa natamani siku moja nionane uso kwa uso na hawa watu
1.Nguruvi3
2.Kiranga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…