9 July 2020
Sheikh Ponda Issa Ponda ametoa mwito huo leo Alkhamisi katika kikao na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kusisitiza kuwa, vyombo husika vinapaswa kuhakikisha kuwa uchaguzi huo mkuu unafanyika katika mazingira ya amani, uhuru na haki.
Kuhusu sifa za wagombea wa uchaguzi mkuu, Sheikh Ponda amesema waraka uliotolewa na taasisi hiyo imeorodhesha baadhi ya sifa hizo kama ifuatavyo: mgombea awe mkweli na mwenye utu, awe mwenye kuheshimu kiapo, awe mwenye sifa ya kupiga vita ubaguzi wa aina zote na awe mwenye maarifa ya kutosha ya kuongoza watu na serikali.
Sifa zingine zilizoainishwa kwenye waraka huo wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania ni mgombea awe mwenye kuheshimu uhuru na mawazo ya watu wengine, mbali na kuzijua na kuziheshimu haki za binadamu. Kadhalika taasisi hiyo ya Waislamu wa Tanzania imetaka wananchi wasiwachague watu madikteta na wadhalilishaji katika uchaguzi huo wa Oktoba 28, 2020.
HAPO AWALI KABISA MWEZI JULAI TAREHE 29 2020 KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, WAMUIBUA SHEIKH PONDA / ATOA WARAKA HUU MZITO / ATAJA SIFA ZA RAIS ANAYEPASWA KUCHAGULIWA
Waislamu Tanzania wataka uchaguzi huru na wa haki, wataja sifa za wagombea
Jul 09, 2020 15:32 UTCSheikh Ponda Issa Ponda ametoa mwito huo leo Alkhamisi katika kikao na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kusisitiza kuwa, vyombo husika vinapaswa kuhakikisha kuwa uchaguzi huo mkuu unafanyika katika mazingira ya amani, uhuru na haki.