Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
SHEIKHE PONDA ANAWEZA NISHAWISHI NIWE MUISLAM
Na, Robert Heriel
Kama ningeambiwa nibadili dini na kuwa muislamu basi ambaye angeweza kunishawishi kujiunga na dini hiyo basi ni ni mtu mmoja tuu, naye ni SHEIKH PONDA ISSA.
Unajua Taikon ni wale watu tunaovutiwa zaidi na misimamo isiyoyumba, watu tunaovutiwa na wapigania haki bila kujali matokeo. Watu tunaovutiwa na wapinga ubaguzi na Upendeleo.
Sheikh Ponda ni moja ya viongozi mahiri na shupavu sana katika eneo la msimamo, na kutetea haki, pia kupinga ubaguzi au uonevu hasa unaofanywa na viongozi wakubwa. Ni nadra sana kwa Ponda kukaa kimya pale aonapo mambo yanaenda kombo alafu yeye asiseme.
Jina lake nimeanza kulisikia miaka 10 iliyopita, na mpaka sasa nauona msimamo wake ni ule ule.
Katika ulingo wa mapambano hasa ya vita baina ya WEMA NA UOVU kunahitaji viongozi shupavu, jasiri na mashujaa wasio na woga.
Wanadamu lazima tutambue kuwa maisha ni vita baina ya wema na ubaya. Na wote tupo kwenye mapambano na kila mmoja anashiriki kwa sehemu yake.
Hii ni kusema kuna pande mbili zinapambana; WEMA NA UOVU.
Kila upande unawapiganaji, kila upande una silaha zake, kila upande una mbinu zake.
Sijajua ndugu yangu unayesoma upo upande gani, je ni WEMA au UBAYA.
Majemadari wa vita katika Upande wa WEMA ni Viongozi wa dini kama vile Wachungaji, mitume, masheikhe, maimamu, maostadhi, Maaskofu, wainjilist n.k.
Waumini ndio wapiganaji ambao wapo kwenye uwanja wa vita wakisaidiwa na viongozi wao.
Ili vita tushinde tunahitaji viongozi shupavu, jasiri, mashujaa, na wenye misimamo isiyoyumba.
Ndugu msomaji unapoenda Kanisani, au Msikitini alafu ukamuona kiongozi wako wa dini anashindwa kupambana, kukemea, kukosoa, kupigia kelele maovu yaliyomo ndani ya jamii yako ikiwemo nchi basi jua hapo huna jemedari, jua upande wenu mmeshazidiwa.
Jemadari wako wa vita anakufundisha kuwaogopa waovu, anakufundisha kuwaheshimu watu wanaofanya uovu na ndio maana maovu ndani ya jamii hayaishi.
Ukiona kiongozi wako wa dini(jemadari wako katika imani anayekuongoza kwenye vita vya kutokomeza uovu) anashindwa kukemea viongozi wenzake wafanyapo maovu, au viongozi wa serikali jua huyo anataka upande wenu ushindwe, na hakika utashindwa tuu!
Sheikh Ponda Issa ni miongoni mwa majemadari ninaowakubali kabisa katika mapambano ya kukemea, kuupigia kelele uovu kama utajitokeza. Nafikiri kuongozwa na mtu kama yeye ni ufahari, kwani anaujasiri na hodari wa kupambana kwenye kupinga uovu.
Maovu yanaongezeka kwa sababu upande wa waovu hawaoni shida kuwatishia upande wa wema. Uovu unaongezeka kwa sababu asilimia 90% ya viongozi wa dini wameshindwa kuongoza mapambano. Wamekubali yaishe, wamekabidhi kombe kwa wahuni.
Ndio maana siku hizi sio ajabu kuona watu wakitembea uchi barabarani, sio ajabu kuona picha za uchi mitandaoni, sio ajabu kuona video za wasanii zisizo na maadili, na viongozi wa kidini wapo wamezubaa zubaa tuu. Wao kwa asilimia kubwa huendekeza pesa, na bahati nzuri wenye pesa ndio hao hao watenda uovu, mwisho wanasaliti kambi ya wema wamebaki kuitwa sheikhe ubwabwa au Mchungaji wa Upako hewa.
Unaingia kwenye kanisa au msikiti ambao kiongozi wake anakufundisha wewe Askari(muumini) kuwa mwoga kupambana na adui(waovu).
Taikon kama Taikon tangu aone hilo gap, hajawahi kutoa sadaka au zaka chini ya viongozi wa namna hiyo. Huwezi mlipa Jemadari anayekufundisha kuwaogopa waovu kuliko kumuogopa Mungu.
Yohana Mbatizaji ambaye ni Jemedari alimchana makavu Mfalme Herode kuwa anakosea kulala na Mke wa kakaake. Yohana hakuogopa matokeo.
Nabii Daniel hakuogopa kumchana Mfalme Nebukadreza
Nabii Isaya hakuogopa Kumchana Mfalme Daudi alipolala na mke wa mtumishi wake.
Nabii eliya hakuogopa kumchana Malikia Yezebeli
Nabii Yeremia hakuogopa kuwachana wafalme wa Yuda na Yerusalemu
Nabii Yona baada ya kuadhibiwa na Mungu hakuogopa tena kuwachana waovu wa Ninawi.
Nabii Musa hakuogopa kumchana Nduli Farao.
Hao ni majemadari walioongoza vita waliokuwa upande wa wema wakipambana na baadhi ya waovu.
Sasa wewe unaenda kuwa Sheikh sijui Mchungaji, alafu hujui fani hizo ni taaluma za kijeshi katika falme za kiimani. Yaani usomee usheikhe au uchungaji alafu ushindwe kupinga uovu wewe si mpuuzi tuu, tena unapaswa kudharauliwa na kutemewa mate.
Yaani ni sawa na Mtu aende kozi ya jeshi pale monduli au asomee kozi ya upolisi pale CCP moshi alafu aogope kupambana na wahalifu sijui majambazi. Sasa wewe ni polisi gani au mwanajeshi gani kama sio mpuuzi tuu wa kudharauliwa.
Viongozi wa dini mubadilike, sio kazi kudai Sadaka na zaka za watu alafu mkiambiwa mtoke hata mtoe tuu tamko kuwa jambo fulani ni baya na kulikemea mnashindwa.
Mimi Taikon hamtalamba sadaka na zaka yangu hasa kwa yale makanisa yasiyoweza hata kukemea maovu, kazi kutaja maovu ya zamani yaliyomo kwenye biblia wakati mtaani kuna mifano ya kutosha tuu.
Viongozi wa dini wanashindwa kuondoa upuuzi uliomo kwenye muziki wa bongo Fleva, watu wanakaa uchi, zinaa zinafanywa hadharani, ati wanawategemea wanasiasa. Duuuh! Kazi za wanasiasa tangu zamani sio kukemea masuala ya maadili, wao huyakemea kwa mgongo wa viongozi wa dini.
Viongozi wa dini kama majemadari wa vita, walipaswa kuongoza mapambano, kuwekea vikwazo wale wote wanaoenda kinyume na maadili. Ikiwemo viongozi wa kisiasa.
Lakini unakuta kiongozi wa dini akiitwa na mwanasiasa anaanza kujichekesha chekesha kama mpumbavu, Unaanza kusifia sifia tuu unasahau kukosoa.
Uovu hauonywi kwa kubembelezwa, uovu unakemewa na kukaripiwa kwa kinywa kipana chenye pumzi ya uhai. Unakuta kiongozi wa dini anaonya akisema; tunawaomba wale viongozi wa dini tafadhalini, muwe mfano bora, muache dhambi, sijui wizi.
Taja kabisa na kemea kuwa fulani acha tabia fulani, usidhani hiyo nafasi yako ya Uwaziri ndio tutakuonea aibu kukukemea.
Muovu hana cheo, muovu ni muovu tuu. Ni dhambi kubwa kumheshimu mtu muovu.
Lakini kwa uzembe wa viongozi wa leo, waovu na watendao mambo ya kipuuuzi ndio wanaheshimika. Sishangai kwa nini hata yakitokea matamasha ya kidunia watu hukimbilia huko kuliko matamasha ya dini.
Zamani ilikuwa ni aibu kwa kijana kwenda Kwenye matamasha ya muziki, au aibu kwa kijana chini ya miaka kumi na nane kwenda Klabu na hii ni kutokana na viongozi wa zamani walikuwa shupavu, wakali wenye misimamo mikali.
Lakini unapopenda pesa unauza utu wako.
Sheikhe Ponda Issa Mimi ni Mkristo ila nakukubali sana mzee wa mapambano.
Katika maisha usikubali kuongozwa na kiongozi mwoga, huyo atakufundisha kuwaogopa waovu, atakufundisha kuwaabudu waovu kwa sababu kadhaa.
Miwisho; Nimemtumia Mzee Ponda kama mfano wa viongozi wa dini hapa nchini ambaye kwa kweli ameonyesha msimamo wake kwa muda mrefu.
Nafahamu wapo viongozi wa dini kama yeye ambao wapo mbele kuhakikisha jamii yetu inakuwa jamii bora.
Wito: Viongozi wengine wa dini ambao mnashindwa kukemea maovu muache mara moja. Na sisi waumini tusikubali kuabudu au kufundishwa maneno ya Mungu na watu waoga. Watatufundisha kumuogopa shetani badala ya kumuogopa Mungu.
Na nipumzike sasa;
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Dodoma