Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 9,504
- 20,293
Sio kisiwa, ni eneo lipo mkuranga wilaya ya Pwani, labda kama zipo Kisiju mbiliNi kisiwa kipo huko kilwa kusini.
Sio kisiwa, ni eneo lipo mkuranga wilaya ya Pwani, labda kama zipo Kisiju mbiliNi kisiwa kipo huko kilwa kusini.
Kwanza hakuna popote nilipoandika kwamba kuswali swala tano ni sababu ya kuwa tajiri.Wewe unaye swali hizo swala tano, umesha fikia hata theluthi ya utajiri wa Bakhressa?
Pamoja na kuswali kwako hayo maswala tano yako?
Eeeh eeh eeh.Kama hali yao ya uchumi ni nzuri haina shida!
Lakini kama eneo hilo ni maskini basi dini ni shida!
Akikujib,nitag😄😄😄wewe una utajiri gani kumzidi Bakhresa anayeswali swala tano?
Ni kisiwa kipo huko kilwa kusini.
Kule hakufai kabisa. Pamesahaurika sana. Watu hawaendi shule, badala yake ni Madrasa, akipiga zake Madrasa miaka minne tayari ni msomi wa heshima.
Kinywaji adui kuliko vyote kule ni 'Fanta'[emoji2]. Fanta ina historia yake kule[emoji3]
Ilikua ni kabla ya mwaka 1993. Inasemekana kuna ngalawa au mtumbwi ulipunduka huko Commoro, sasa kama ilivyo kawaida, watu wa Pwani wana msemo unasema bahari haikai na uchafu.
KIle chombo kilichozama kilikua na mzigo mkubwa tu, mzigo ule ulisukwasukwa na mawimbi hadi mizigo mingine ikatokea Pwani ya Kisiju. Katika mzigo ule kulikuwepo na vinywaji vilivyokuwa kwenye kopo.
Pakawa na udadisi sana kuhusiana na kilichokuwemo mule ndani. Hapo mzigo upo mikononi mwa wazee wanao heshimika na kule wazee wanaoheshimika na Shehe, Imam, Ostaadhi na wengineo ambao ni viongozi kwenye dini na wazee ndani ya jamii[emoji3].
Wakati wanajiuliza kuhusu kilichomo mwenye vikopo vile, ikabidi akatafutwe kijana mmoja ambaye ndiye allikua ni mjanja mjanja pale Kisiju maana alikua ni mtu wa kuvuka sana, yaani kwenda sana mjini[emoji3] (Mbagala na Mkuranga 1991 - 1993)[emoji2].
Kijana alipoitwa, akawekwa kati na wazee ambapo wakamuuliza kuhusu vile vikopo. Kijana wa mjini alipoviangalia, akawaambia "aaah hizi ni fanta, ni soda tamu sana hizi" kijana akafungua, akaonja mbele yao akaomba na vikopo kadhaa aondoke navyo wakampatia vikopo vinne akasepa.
Wale wazee kwa kuwa palikua na cartons za kutosha wakaugawa ule mzigo haki bin haki na hata wasiokuwepo wakapelekewa. Basi wazee ma Mwinyi wakaanza kunywa fanta kikopo kimoja baada ya kingine.
Ikafika muda wa azana kimya, muda wa azana nyingine kimya...wanaanza kutafutwa viongozi msikitini wote hawapo, kuanzia Muazini hadi Mnadi swala, waumini ni mmoja mmoja. Walipowafuata majumbani wanakuta watu hawajitambua, kuja kustuka na kurudiwa na akili ni kesho yake.
Ikabidi kiitishwe kikao waulizane ni kipi kilitokea na yule kijana mtaalamu wa mjini naye akaitwa. Wakamleta wamembeba. Maana yeye baada ya kikopo kimoja alitulia , siku hiyo asubuhi ndiyo akanywa.
Yule kijana akaulizwa ina maana wakinywa fanta ndiyo inakuwa vile? Katika vitu viliwakwaza na kuwakasirisha wale wazee ni siku kupita bila azana na kwa ukubwa wa mzigo karibu waumini wengi walikua bwii.
Katika kujadiliana Ilibidi wazee wafikie muafaka wa kuipiga marufuku Fanta pale Kisiju, na hatua kali kuchukuliwa kwa yeyote atakayekutwa anakunywa au hata kuileta Fanta pale Kisiwani.
Kumbe walichokuwa wamekunywa siyo Fanta bali ni beer aina ya Stella Artois ya vikopo ambayo ilikua maarufu sana miaka ile[emoji2]View attachment 2782313
Mpaka hapa wewe ndio unaonekana ni tatizo na sio wana kisijuKama hujui kitu tulia
Dini yetu ya kiislamu ni tofauti na dini yenu.
Sisi hata salamu yetu ni uniform all over the world.
Mfumo wetu wa maisha pia ni uniform ukitoa waliodeviate.
Hakuna tofati ya muislamu wa kusiju Mbagala Bagamoyo Kilwa Masaki na hata misri kwenye suala zima la ibada.
Kwahiyo nilichomjibu kipo relevant.
Tatizo lenu mna chuki na amuupendi uislamu kila failure ya muislamu mnapenda kuihusisha na dini yake which is very wrong.
Unataka kusema nini?Una uhakika na unayosema,unawajua shia,sunni,ahmadiya etc??
Rejeeni mashirika ya umma kuendeshwa na wachaga na kuajiri wachaga na wakistru.imefika mahali waislam ni wa kuwahesabu.
Alipojaribu Dr Dau na Nssf kuajiri anao wapenda yeye mlimbebesha chuki kuwa kuna uislam umeshika nssf na waislam. huku data za mashirika mengine kama CRDB,TANESCO,Azania bank. na mengineyo mkificha.JPM aliendesha zoezi la vyeti feki malengo ni serikalini lkn kukubwa ni kuona nssf wanapukutishwa sababu ya waislam haaana vyeti,matokeo yake wakaone waishie tu sababu wangeshuka chini zaidi ni nchi ingesimama,wakisrto wengi wameajiliwa kwa kuletwa kwanza.
Kuhusu KISIJU ndio mjue na mjitafakari watapata wapi kazi ?zaidi ya ujasiria mali mdogo mdogo wapate cha kula na sio serikalini wanalipwa na kuiibia serikali ili wawe matajiri kama wewe andrew 123.
Siku hizi mijadala hii imenitoka, baada ya kuona watu humu huanzisha tu mada ilimradi.
Suala la mleta mada wala halitafsiriki hivyo kama anavyotaka yeye, ila ndio hivyo hawa jamaa tu hupenda ligi zisizo na maana.
Mtu kuswali swala tano hakumuondolei umasikini na wala kutokuswali hakumfanyi mtu kuwa tajiri, na wangapi wanaswali lakini wanauchumi mzuri na wangapi hawaswali lakini wanauchumi mmbovu?
Na kwani kuswali mtu inamchukua masaa mangapi katika siku? mpaka useme wanaswali kuliko kufanya kazi? kwani wanashinda misikitini!?
Na wasichokijua, hata kutafuta rizki katika uislamu ni ibada.
Ziwe shule nyingi kuna watoto wangapi?Nipo Kisiju idadi ya misikiti Ni mingi kuliko shule na hospitali. Wananchi wanaswali kuliko shughuli za kuingiza kipato. Kiuchumi hii ipoje? Kilimanjaro wenzetu wanapiga kazi na kulipa kodi. Hapa Kisiju ni tofauti Sana
Acha uongo na wewe. Kisiju sio KilwaNi kisiwa kipo huko kilwa kusini.
Wewe endesha maisha yako, huwalishi na wala hawapati ruzuku ya kodi yako kuwasaidia maisha. Ni wewe ndio unaona hawafanyi kazi kwa upofu wako au unadhani wanapataje mahitaji yao ya kila siku?Nipo Kisiju idadi ya misikiti Ni mingi kuliko shule na hospitali. Wananchi wanaswali kuliko shughuli za kuingiza kipato. Kiuchumi hii ipoje? Kilimanjaro wenzetu wanapiga kazi na kulipa kodi. Hapa Kisiju ni tofauti Sana