Na Mwandishi wetu.
Mkurugenzi mtendaji wa Coca-Cola kwanza ndugu. Andrew Musingo aliyeteuliwa na wamiliki wa kampuni ya Coca-Cola kwanza ambao ni Coca-Cola beverages Africa kutoka nchini Afrika ya Kusini amenyimwa kibali na mamlaka ya nchi ya Tanzania kwa kile wasemacho kuwa watanzania wanauwezo wa kufanya hivyo.
Katika mazingira ya mwendelezo wa ushindani wa kibiashara na kiuchumi baina ya Tanzania na kenya kwa mara nyingine kiongozi mkuu wa taasisi binafsi kutoka nchi ya kenya anakataliwa kibali cha kufanya kazi katika taifa la Tanzania baada wa yule wa VODACOM (sylivia Mulinge) kukataliwa kutokana na sababu ambazo mamlaka imeziweka kwa ufupi kama watanzania wanauwezo wa kufanya kazi hizo.
Imeelezwa na mwandishi wetu kuwa miezi kadhaa nyuma kampuni ya cocacola beverages Afrika ilimtanganaza Andrew Musingo raia wa kenya kama mkurugenzi mpya wa kampuni yao kwa tawi la Tanzania ifahamikayo kama Coca-Cola Kwanza. Hii ni baaada ya raia wa Afrika kusini Ndugu Basil Gadzios kumaliza muda wake nchini Tanzania na kuhamia Zambia kwa majukumu mengine.
Kwa maelezo ya watu wa ndani baada ya kutangazwa, kumekuwa na maombi ya vibali vya kufanya kazi nchini yaliotumwa na kampuni hiyo kwa wizara na Zaidi ya mara 4 wizara imekataa maombi hayo na kusema haiwezi kumpa kibali kwani watanzania wanaweza kufanya kazi hizo.
Tangu kunyimwa kwake vibali vya kufanya kazi katika taifa la Tanzania amekuwa akija kwa visa ya kibiashara na kufanya kazi kwa muda mfupi mpaka pale mamlaka ya uhamiaji ilipofika na kumkamata kwenye ofisi na kumtoa kwa nguvu na kumrudisha kenya.
Mnamo tarehe 23/11/2020 akitokea Nairobi kenya na shirika la ndege la Kenya Airways Mkurugenzi mpya wa Coca-Cola kwanza Andrew Musingo amekataliwa na mamlaka uhamiaji ya Tanzania kuingia nchini kutekeleza majuku yake mapya kwa maelezo kuwa anapaswa kupata kibali cha kufanya kazi nchini ndipo aweze kuja nchi, hivyo Raia huyo wa kenya amelazimika kuondoka tena nchini kurudi kwako kutokana na kukataliwa kuingia taifa la Tanzania.