Friends and Our Enemies,
Serikali kupitia wizara ya mambo ya nje imetuma ujumbe kwenda kwa kiongozi wa kanisa katoliki duniani.
Ingawa hajifahamika zaidi undani wa mazungumzo katika ujumbe huo kwenda kwa papa lakini itoshe tuh kusema kwamba serikali yetu ni serikali iliyojawa na hekima na busara katika kuongoza taifa letu.
Mara baada ya kuonekana kwa taarifa hiyo vijana mbali mbali wenye mtazamo hasi dhidi ya serikali wamenasibisha ziara hiyo eti kwamba serikali imeenda kujisafisha kwa kanisa huko vatican kutokana na mahusiano yake na kanisa hapa nchini kuzorota.
Tungependa kuwaambia wafuasi wa kanisa katoliki na wafia dini wenzao kwamba siyo mara ya kwanza serikali kutuma ujumbe kwa papa vatican.
Soma Pia: Papa Leo aahidi kuiombea Tanzania amani na Utulivu
Hata Rais Samia kabla ya uchaguzi alishawahi fanya ziara vatican na kukutana na papa.
Pili,serikali haina ugomvi na kanisa katoliki nchini hapa,wanaoutafuta ugomvi na serikali ni wao wenyewe kanisa kwa kutaka kujiingiza kwenye uhasama na serikali kwa kisingizio cha kupigania haki za binadamu na demokrasia huku ikihamasisha chuki na utengano kwa waumini wake dhidi ya serikali.
Ilichofanya serikali ni muendelezo wa taratibu zake za siku zote hazina uhusiano wowote na hizo propaganda wanazozusha hao wafia dini.
Kanisa katoliki Tanzania na viongozi wake watambue kuwa wao hawawezi kuwa juu ya serikali,serikali ina mkono mrefu wa kuweza kutuma waziri wake na kiongozi wao mkuu duniani akaitika wito na kuwapa heshima.
Wao ni nani hadi wajifanye wana nguvu dhidi ya serikali???
ANAANDIKA ASKOFU BAGONZA
NADHANI TUNAJICHANGANYA?! Au ni Mimi Najichanganya?!
1. SAFARI YA VATICAN
Tungepatana nyumbani kwanza na wawakilishi wa Papa kabla ya kwenda kwa Papa. Tumempiga Padre wake; Tumetengeneza Wakatoliki Vijora; Tunamdhalilisha Kitima, halafu tunaenda kwa Papa. Hatari ipo ya kuambiwa, “Kama hamkumsikiliza Musa na Manabii, hamtaweza kushawishika hata mtu akifufuka”(Luka 16:31). Patana na mshtaki wako kabla ya kwenda kwa Kadhi.
2. MABEBERU:
Tumezoea kuzizodoa nchi za Ulaya kuwa ni mabeberu. Vatican iko Ulaya. Je, Hata Papa ni Beberu? Naye anataka kuchimba Uranium yetu?
3. AMANI YA NCHI
Wizara ya Mambo ya Nje inamuomba Papa aiombee nchi yetu iwe na Amani na Utulivu. Wizara ya Mambo ya Ndani inasema nchi iko salama imetulia. Hawawasiliani? Nani msemaji wa nchi?
4.MARIDHIANO
Wazee wa Chama wanataka Maridhiano. Bunge linasema nchi iko sawa. Tume iko kazini kuchunguza. Nani mkweli? Je kuna ukweli tusioujua hadi tuumulike kwa tochi ya Tume? Je tunataka maridhiano kabla ya ukweli?
5. CHADEMA na CCM
Wapo wanaosema Chadema Imekufa lakini wanaisema kila siku. Huyu ni marehemu mwenye nguvu. Makada wa CCM wanasema CCM tunatamba nayo. Ukiiangalia unaiona ni mfungwa asiye na pingu. Nani zaidi kati ya marehemu anayeishi na aliye hai lakini amekufa?
6. YALIYOTOKEA OKTOBA 29
Siku hii inatusumbua mpaka tunaenda Vatican. Bado kwenda Mecca. Kama waliokufa hawajulikani; waliowaua wanajijua. Dunia inajua makundi yote mawili. Hekima ya WAJALUO inasema, “kuchelewa kwenda kujisaidia, hakuzuii njaa kuuma”. Tukubali: Tuliua, Walikufa; tuombe radhi, tuwajibishane na kusonga mbele.
7. TUNDU LISU
Waliompiga risasi hawajapatikana lakini walioiba michango yake wamekamatwa. Yeye yuko rumande. Mahakama imeenda likizo na haki yake iko likizo. Fikiria daktari akienda kupumzika katikati ya operesheni mgonjwa?!
8. WIZARA YA MAMBO YA NJE
Hii Wizara inaonyesha tuko vitani. Kimsingi ina mawaziri 4: Kombo, Kabudi, Nyalandu na JK. Msiniulize JK ni nani maana mtamuona anatumwa katika masuala magumu nje. Waliobaki 3 na manaibu 2, wanaunda kikosi kazi cha mawaziri wa wizara. Msiniulize nani ni Boss maana Kabudi anaweza kujikuta ni Naibu Waziri. TUNAJIKANYAGA MNO.
9. Taifa likiwa katika mtifuano kama tulio nao, linakuwa kama mgonjwa. Hawezi kwenda kwa daktari akagoma kuvua nguo. Tuvue zote na madaktari watuingizie vidole kila mahali ili kubaini ugonjwa ulipo ndipo tutibiwe.
Wajaluo wakibanwa TEZI DUME husingizia wanaumwa kichwa.
Sasa Wajaluo wa TEZI JIKE hao usiseme!