Kitu gani umejiuliza sana lakini hupati majibu?

Kitu gani umejiuliza sana lakini hupati majibu?

Kwanini mtu hata akiwa mwizi, malaya, mlevi asiyetunza familia akifa bado atapewa sifa nzuri kwamba alikuwa mtu wa watu, mpenda amani, alipendwa na kila mtu? ili hali alipokuwa hai pengine jamii ilikuwa inaomba hata apotee maana amekuwa kero
😀😀😀 kuna mshkaji wangu alikufa kwa sababu ya kunywa bia kali bila kula chakula cha kutosha, siku ya msiba sababu ya kifo ikasemwa ni sukari ilishuka mwilini sio ulevi
 
Kwa nini mademu hawanitongozi hata kama wananipenda bali wanataka mi nianze kuwatongoza, why?
 
Kwenye miji mikubwa, lazima utakuta wahindi wanamiliki pikipiki, wengine zile kubwa.
Sasa kwanini huwezi kusikia mhindi kafa/kapata ajali ya pikipiki wakati dereva boda boda wanadondoka kama nzi.
1.Ni suala la idadi yao ndogo takwimu hazishtui.
2. Wanajifunza vyombo vya moto kwa hatua na tahadhari zake.
3. Ni jamii ya wenye nidhamu kuanzia ngazi ya familia na maisha.
Katika maisha kila kitu ni NIDHAMU!
 
Mi najiulizaga watu wanaendeshaje maisha Kwa shughuli ndogo ndogo wanazofanya? Unakuta mtu anauza shanga, maji, anatembeza vitumbua au kuuza viatu kama waha hapo hapo apate nauli, Kodi, bills (maji, umeme, msos na etc). Nawaza kwamba faida anayopata inatosha kuendesha maisha?
 
Alimuomba (ALLAH) amuache hai, aka kubaliwa kuwa afe mwisho wa Dunia, maana yeye hana pepo hata iweje, yake ni moto hivo ana jitahidi apate wa kumpa kampani huko Motoni
Hadithi za Abunuasi
 
Back
Top Bottom