Kituko kutoka Zimbabwe: Tanzania yatambulika kama Islamic Republic (Jamhuri ya Kiislamu ya Tanzania)

Kituko kutoka Zimbabwe: Tanzania yatambulika kama Islamic Republic (Jamhuri ya Kiislamu ya Tanzania)

View attachment 3274634

Wakati Waziri wa Mambo ya Nje Thabit Mohammed Kombo alipomtambulisha Dr Janabi kwa Rais Emerson Mnangagwa. Taarifa ya ukurasa wake wa Facebook iliutambua ugeni huo kama wa kutoka Jamhuri ya kiislamu ya Tanzania.

Ama iwe makosa ya kiuandishi (typo), kupitiwa, kudhania, kuitambua Tanzania kama Jamhuri ya Kiislamu ni kosa kubwa kwa watumishi wanaosimamia akaunti ya social media ya Rais Emerson Mnangagwa.

Nashauri Wizara ya Mambo ya Nje iwalazimishe Ikulu ya Zimbabwe watuombe radhi.
Ikiitwa jamhuri ya kiislamu ya tanzania, wewe unapungukiwa nini ?


Acheni kupenda vitu petty petty
 
CRDB wanakuletea Al-Barakah huduma ya kibeniki ya kiislamu na ni spesheli kwa watu wa juu wa serikalini. Sio maneno yangu ni maneno yao. Sidhani kama wamekosea maana wamesema lisemwalo lipo kama halipo lipo njiani linakuja.
View attachment 3274799
kwa udini huu wa taasisi ya kifedha nchi itaacha kuitwa jamhuri ya kiislam? Mara kampuni ya simu nayo imeandaa futari kwa wadau wake, ni udini mtupu kwenye mambo ya umma. Kule zanzibar kuna magazeti ya huko yanaonesha serikali ya huko na uislam ni kitu kimoja. Kila mara mwinyi yuko msikiti fulani, mara kakutana na imamu gani, mara kaswali msikiti gani inakuwa habari kubwa kwenye magazeti hayo. Udini umekuwa waziwazi na unatamalaki hakuna wa kuukemea. Akina mnangagwa wanaona hii ni jamhuri ya kiislam
 
Eti "Experienced Cardiologist"....Watu wanachekesha sana....kasomea wapi?...
Public health specialist?...
Hiyo ndio issue. Yani wametutoa kwenye reli.

Janabi, mshauri wa tasnia ya lishe bora, hafai ofisi ya WHO. Kile kichwa hakiwezi ku address ma issue ya afya ya Waafrika. Laiti wangelijua.

Anyhow, mwache aende, huku home hana bosi, Muhimbili ni kama anasukuma walevi tu, watu wafe wasife, kivyao. Kule anaenda kuhenya na kupimwa. Akichemka watam rip out of the chair kama Tibaijuka.
 
View attachment 3274634

Wakati Waziri wa Mambo ya Nje Thabit Mohammed Kombo alipomtambulisha Dr Janabi kwa Rais Emerson Mnangagwa. Taarifa ya ukurasa wake wa Facebook iliutambua ugeni huo kama wa kutoka Jamhuri ya kiislamu ya Tanzania.

Ama iwe makosa ya kiuandishi (typo), kupitiwa, kudhania, kuitambua Tanzania kama Jamhuri ya Kiislamu ni kosa kubwa kwa watumishi wanaosimamia akaunti ya social media ya Rais Emerson Mnangagwa.

Nashauri Wizara ya Mambo ya Nje iwalazimishe Ikulu ya Zimbabwe watuombe radhi.
Ila ukienda nchi zote za southern africa kama botswana, zimbabwe na malawi. ,kwao ukiwatajia tanzania wanachokiwaza ni zanzibar, kiufupi zanzibar ni maarufu kuliko dar es salaam kimataifa, na watu wengi wana picha ya zanzibar ni sehemu ya kiislamu tu
 
Sioni tatizo kwenye hilo, as far tuna Imani zaidi ya 14 na Uhuru wa kuabudu kuanzia Ibada za kawaida hadi fellowship za Jioni na asubuhi

Naweza kukiri kwamba itakuwa ni typing error tu

Tuwasamehe bure
 
Back
Top Bottom