Kituko kutoka Zimbabwe: Tanzania yatambulika kama Islamic Republic (Jamhuri ya Kiislamu ya Tanzania)

Kituko kutoka Zimbabwe: Tanzania yatambulika kama Islamic Republic (Jamhuri ya Kiislamu ya Tanzania)

kwa udini huu wa taasisi ya kifedha nchi itaacha kuitwa jamhuri ya kiislam? Mara kampuni ya simu nayo imeandaa futari kwa wadau wake, ni udini mtupu kwenye mambo ya umma. Kule zanzibar kuna magazeti ya huko yanaonesha serikali ya huko na uislam ni kitu kimoja. Kila mara mwinyi yuko msikiti fulani, mara kakutana na imamu gani, mara kaswali msikiti gani inakuwa habari kubwa kwenye magazeti hayo. Udini umekuwa waziwazi na unatamalaki hakuna wa kuukemea. Akina mnangagwa wanaona hii ni jamhuri ya kiislam
Msisahau kuwa hayati Magufuli alifanya hayohayo, kuhutubia taifa na kutoa misimamo yake ya kazi akiwa madhabahuni. Mara kwa mara alipoenda kusali kanisani, baada ya ibada alikaribishwa kuongea na waumini, na hotuba zake hizo zilirushwa kwenye tv zikaenea nchi nzima.
Kama tunachukizwa na tabia ya kuleta siasa kwenye dini, tuikatae na kuikemea kwa yeyote atakayefanya hivyo. Wakati wa Magufuli wakristo walinyamazia haya mambo kana kwamba yalikuwa sahihi.
 
Wewe ni Extremist Galatian
Fafanua.....mimi nina qkili timamu ya kuona mbele hayo mambo wengi wenu kwa kukosa akili hamuoni madhara yake...je akija rais mkristo akafanya kinyume chake msije mkalia...maana ndivyo itakavyo kuwa....kuna vitu tuna sema ni NONSENSE ndiyo hivi mnavyo shabikia maana vitakuja kuwaumiza nyinyi wenyewe mara 3 ya mlivyo waumiza wengine ...kumbukeni kwa sasa duniani hakuna nchi ya waislamu yenye nguvu isipokuwa Iran tu nayo ishukuru urussi maana wairani walitumia akili kujikomba kwa warusi ambao ni wakristo.
Hivyo ukimuona mtu anashabikia mambo ya dini kuingizwa serikalini jua huyo mtu ni mpumbavu au ana ajenda ya kulisambalatisha taifa ...kumbuka nilitoa onyo hapa kuwa nchi yetu ipo mikononi mwa RAIA FEKI hao raia feki kwao Tanzania siyo kitu wanachowaza ni kuifisidi nchi usiku na mchana na kutorosha pesa kwenye nchi zao wanazo zipenda
 
View attachment 3274634

Wakati Waziri wa Mambo ya Nje Thabit Mohammed Kombo alipomtambulisha Dr Janabi kwa Rais Emerson Mnangagwa. Taarifa ya ukurasa wake wa Facebook iliutambua ugeni huo kama wa kutoka Jamhuri ya kiislamu ya Tanzania.

Ama iwe makosa ya kiuandishi (typo), kupitiwa, kudhania, kuitambua Tanzania kama Jamhuri ya Kiislamu ni kosa kubwa kwa watumishi wanaosimamia akaunti ya social media ya Rais Emerson Mnangagwa.

Nashauri Wizara ya Mambo ya Nje iwalazimishe Ikulu ya Zimbabwe watuombe radhi.
Nadhani kakosea yeye mwenyewe tu
 
hii salamu tu ni udini tosha
Hii salamu wala siyo udini, na kama ina dini basi inafaa kwa dini zote. Tafsiri yake ni kumtakia amani anayesalimiwa. Kwani kuna mtu asiyependa amani? Hata katika Biblia imeandikwa Yesu alipokuwa akiwatokea wafuasi wake aliwasalimu "amani iwe kwenu", ndiyo "assalaam alaykum".
Lakini ukisalimia "Bwana Yesu asifiwe" au "Tumsifu Yesu Kristo" unamwalika unayemsalimia ajumuike nawe katika imani yako ya kumsifu Yesu Kristo, ambayo pengine hakubaliani nayo. Salamu hii inafaa kwa wenye imani moja kwa Yesu, lakini kwa wengine inaweza kuwa makwazo.
Hata wapagani wanahitaji amani, kwa hiyo salamu ya kutakiana amani ningeichagua iwe ndiyo standard maana inawafaa wote, wenye dini na wasio na dini. Mnaonaje ikatafsiriwa kiswahili "Amani iwe nanyi" na tukaitumia badala ya ile salamu ya mama ya "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania......"
 
View attachment 3274634

Wakati Waziri wa Mambo ya Nje Thabit Mohammed Kombo alipomtambulisha Dr Janabi kwa Rais Emerson Mnangagwa. Taarifa ya ukurasa wake wa Facebook iliutambua ugeni huo kama wa kutoka Jamhuri ya kiislamu ya Tanzania.

Ama iwe makosa ya kiuandishi (typo), kupitiwa, kudhania, kuitambua Tanzania kama Jamhuri ya Kiislamu ni kosa kubwa kwa watumishi wanaosimamia akaunti ya social media ya Rais Emerson Mnangagwa.

Nashauri Wizara ya Mambo ya Nje iwalazimishe Ikulu ya Zimbabwe watuombe radhi.
Kwa mtazamo mwingine, naona kama Rais Mnangagwa amefanya makusudi ili avuruge fikra za wapiga kura huko tukose hiyo nafasi. Hao hao SADC ndio waliomkosesha Odinga nafasi ya uenyekiti wa AU kwa mbinu ya kugawa kura.
 
WAZIRI KOMBO AWASILISHA UJUMBE MAALUM WA RAIS SAMIA KWA RAIS WA ZIMBABWE

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, amewasilisha Ujumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe, Mhe. Emmerson Mnangagwa katika Ikulu ya Harare.

Katika mazungumzo yao, Mhe. Waziri Kombo amemshukuru Rais Mnangagwa na wananchi wa Zimbabwe kwa mapokezi yao mazuri, huku akimfikishia salamu za upendo na mshikamano kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza na vyombo vya habari baada ya kuwasilisha ujumbe huo, Mhe. Kombo ameeleza kuwa lengo la ziara yake lilikuwa ni kumtambulisha rasmi Prof. Mohammed Janabi, Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, kama Mgombea wa SADC kwa nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Kanda ya Afrika wa Shirika la Afya Duniani (WHO).

Kwa upande wake, Prof. Janabi ameeleza kuwa, endapo atachaguliwa kuongoza taasisi hiyo, ataweka msisitizo katika kuimarisha sekta ya afya barani Afrika kwa kushirikiana na nchi wanachama wa SADC Kujenga Afrika yenye afya kwa pamoja.
 

Attachments

  • publer-1742277712624.jpg
    publer-1742277712624.jpg
    83.1 KB · Views: 27
  • publer-1742277714122.jpg
    publer-1742277714122.jpg
    80.1 KB · Views: 23
  • publer-1742277715531.jpg
    publer-1742277715531.jpg
    72.2 KB · Views: 25
  • publer-1742277719730.jpg
    publer-1742277719730.jpg
    111.3 KB · Views: 29
  • publer-1742277718719.jpg
    publer-1742277718719.jpg
    107.8 KB · Views: 33
  • publer-1742277717120.jpg
    publer-1742277717120.jpg
    110.1 KB · Views: 18
Halafu eti huyo ni mwalimu na alikuwa waziri.
Vilaza wanapenyaje mpaka kuwa viongozi!!!????
Kama sio madhara ya copy-edit and paste, basi itakuwa wamelipa kisasi maana Kuna Waziri mmoja wa Tanzania aliwahi kusema Tanzania ni union ya Tanganyika na visiwa vya Zimbabwe
 
Hii salamu wala siyo udini, na kama ina dini basi inafaa kwa dini zote. Tafsiri yake ni kumtakia amani anayesalimiwa. Kwani kuna mtu asiyependa amani? Hata katika Biblia imeandikwa Yesu alipokuwa akiwatokea wafuasi wake aliwasalimu "amani iwe kwenu", ndiyo "assalaam alaykum".
Lakini ukisalimia "Bwana Yesu asifiwe" au "Tumsifu Yesu Kristo" unamwalika unayemsalimia ajumuike nawe katika imani yako ya kumsifu Yesu Kristo, ambayo pengine hakubaliani nayo. Salamu hii inafaa kwa wenye imani moja kwa Yesu, lakini kwa wengine inaweza kuwa makwazo.
Hata wapagani wanahitaji amani, kwa hiyo salamu ya kutakiana amani ningeichagua iwe ndiyo standard maana inawafaa wote, wenye dini na wasio na dini. Mnaonaje ikatafsiriwa kiswahili "Amani iwe nanyi" na tukaitumia badala ya ile salamu ya mama ya "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania......"
Mkuu nakushangaa unapo poteza muda wake kumjibu huyo mgojwa wa akili na aliye jaa chuki dhidi ya waislam mpaka kwenye matako.
 
View attachment 3274634

Wakati Waziri wa Mambo ya Nje Thabit Mohammed Kombo alipomtambulisha Dr Janabi kwa Rais Emerson Mnangagwa. Taarifa ya ukurasa wake wa Facebook iliutambua ugeni huo kama wa kutoka Jamhuri ya kiislamu ya Tanzania.

Ama iwe makosa ya kiuandishi (typo), kupitiwa, kudhania, kuitambua Tanzania kama Jamhuri ya Kiislamu ni kosa kubwa kwa watumishi wanaosimamia akaunti ya social media ya Rais Emerson Mnangagwa.

Nashauri Wizara ya Mambo ya Nje iwalazimishe Ikulu ya Zimbabwe watuombe radhi.
Waziri wetu anapaswa kujitokeza na kutolea maelezo, je ni yeye ameurambulisha ujumbe wake kuwa unatokea Jamhuri ya kiislam?
 
Back
Top Bottom