Kitwanga: Kuna kundi linalomshauri vibaya Rais Samia

Kitwanga: Kuna kundi linalomshauri vibaya Rais Samia

Na kama Rais kila mara anakubali huo ushauri mbaya, basi naye ndie hafai kabisa, ametokea kukiamini kikundi cha watu wachache no matter what bado anaendelea kukiamini tu, anajiharibia kabisa.

Anaonekana ameshikiwa akili, na members wa hicho kikundi nao sasa wanajua wamemshika akili, hivyo wanafanya watakavyo, matokeo yake nao sasa wamejigeuza "marais" kwenye idara zao.

Hayo ndio matokeo ya kuwa na Rais dhaifu, ni sawa na baba nyumbani asiewakanya wanae, anawaacha wafanye vile watakavyo, matokeo yake kila mtoto atajiamulia cha kufanya.
Uzi ulitakiwa uishie hapa
 
Kwamba Hadi yule Mzee asiye na wizara maalum naye anatoa ushauri mbaya au anashauri bt hasikizwi?

Maombi juu ya nchi, viongozi na KANISA ndo yatalitoa Taifa letu ktk mkwamo tuliopo.

Amen
Mtu kama kitwanga KWA Taifa letu ni asset inayotumiwa na wakubwa wa NCHI kutaka Badilikoe FULANI!

Mtu kama msukuma nalieambatana na gwajima kule Mwanza ni muelekeo FULANI kuelekea March 20 ya yoga!

Kitwanga na haiba yake alivyo anafaa Sana kutumika kupeleka ujumbe FULANI KWA Lengo lililokusudiwa!!!!
 
Nyerere alishauriwa na washauri wake ataifishe maduka yote, yani maduka yote mpaka ya Uswahilini yawe ya ushirika au chama.
Na hivi ndivyo ilivyokua, labda kama umehadithiwa sivyo, au aliyekuhadithia hajui, au ni kupamba tu, lakini ukweli kipindi hichi maduka yalikua ni ya ushirika na chama na bidhaa tulinunua kwa kadi ya ration na kwa wiki au wiki mbili mara moja tu

Yaani kama alishauriwa kweli basi ni kinyume na ulivyosema wewe
Ukiritimba uliwepo
 
Binafsi Kitwanga sijawai kumwamini, angemuacha Mama atekeleze majukumu yake tafadhali.

Mama yuko vizuri sana, sioni matatizo ya Mama ingawa kila binadamu ana mapungufu yake.
Huyaoni matatizo ya mama yupi?
Au mama yako mzazi?

Nchi ya watu milioni sitini,unataka watembelee unavyojisikia wewe?

Na tutajuaje kama anaowasema kitwanga ndio kina wewe?

Shat ap [emoji67]
View attachment 2527543
 
Na kama Rais kila mara anakubali huo ushauri mbaya, basi naye ndie hafai kabisa, ametokea kukiamini kikundi cha watu wachache no matter what bado anaendelea kukiamini tu, anajiharibia kabisa.

Anaonekana ameshikiwa akili, na members wa hicho kikundi nao sasa wanajua wamemshika akili, hivyo wanafanya watakavyo, matokeo yake nao sasa wamejigeuza "marais" kwenye idara zao.

Hayo ndio matokeo ya kuwa na Rais dhaifu, ni sawa na baba nyumbani asiewakanya wanae, anawaacha wafanye vile watakavyo, matokeo yake kila mtoto atajiamulia cha kufanya.
Unaaminije maneno ya Kitwanga?
Huyu bwana tangu rafiki yake aliyemshawishi agombee urais Magufuli afe ana stress na frustration ya kukosa sikio la rais kama zamani.
Huyu na Mayanga Construction wanahitaji nasaha za kitabibu
 
Na hivi ndivyo ilivyokua, labda kama umehadithiwa sivyo, au aliyekuhadithia hajui, au ni kupamba tu, lakini ukweli kipindi hichi maduka yalikua ni ya ushirika na chama na bidhaa tulinunua kwa kadi ya ration na kwa wiki au wiki mbili mara moja tu

Yaani kama alishauriwa kweli basi ni kinyume na ulivyosema wewe
Ukiritimba uliwepo
Hapana, si kweli, labda kwenu tu.

Upanga tulikuwa na duka la baba Taybal, kulikuwa na duka la wahindi nimewasahau jina Four Flats jeshini watoto wa Muhimbili Primary tulikuwa tunakwenda kununua Peramaziwa.

Uswahilini kulikuwa na maduka ya watu binafsi. Hayakuwa mengi kama sasa lakini yalikuwapo.

Mkuu hii habari imeandikwa na Shivji katika kitabu chake "Development As Rebellion: A Biography of Julis Nyerere" si habari ya vijiweni.
 
Kitwanga anasema kuna kundi ambalo limejipenyeza kwa rais na kila mahala linamshauri vibaya Rais.

==========

WAZIRI wa zamani wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, amesema kuna kundi linalomzunguka Rais Samia Suluhu Hassan ambalo limekuwa likiweka vigingi kwa watu, wakiwamo wataalamu, wanaotaka kushauri kuhusu mambo mema ya kuipeleka nchini pazuri zaidi.

Kitwanga amesema mbali na kuweka vigingi kwa watu wenye nia njema, kundi hilo limekuwa likiwaona tishio, hivyo kuwachafua, ili kulinda masilahi binafsi. Amemwomba Rais kuwa makini na kundi hilo.

Kitwanga alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mambo mbalimbali yanayoendelea nchini na kwamba ameona kuna umuhimu wa kumshauri Rais Samia kupitia vyombo vya habari.

Alisema kundi hilo limejipenyeza katika kila sekta zikiwamo taasisi za umma na kwamba lengo lake ni kuharibu nchi kwa maslahi binafsi.

Chanzo: Nipashe
Kikwete ni mtu hatari sana, mama ni mtu dhaifu sana
 
Hakuna wa kumshauri vibaya Rais! Yanayo endelea ni matokeo ya uwezo wake na utendaji wake na fikra zake tusiwasingizie watu!
Yanayoendelea yepi? Acheni majungu. Nchi inaenda vizuri.
 
Acha majungu wewe. Chuki zako za kuwa nje ya circle zisitulazimishe tumuone mbaya. Na hakuna lolote baya kwa rais kupata ushauri kutoka kwa mtangulizi wake, tena gentleman kama JK.
Kikwete ni mtu hatari sana, Samia ni mtu dhaifu sana
 
Kusema hakuna kufunga mipaka halafu unaruhusu wakanunue chakula nje walete ndani , hiyo ni akili au mavi
Ulitaka wakulima wafungiwe soko ili wapate hasara kukukulisha wewe? Kuagiza kutoka nje ili kustabilize prices ni sawa tu, na Samia si wa kwanza. Haya mambo ya kumlazimisha mkulima auze kwa bei unayoitaka yamepitwa na wakati. Ukiona unapata shida mapori yapo mengi, kalime.
 
Hapa kidiplomasia, Kitwanga amemwambia Rais anafanya mambo hovyo hovyo au anakosea kosea katika mambo yake.

Mara nyingi sana watu wanatumia lugha ya kuwasema vibaya washauri wa Rais ili kumwambia Rais haupo sawa, unakosea.

Wataalamu mnaweza kunisahihisha.
 
Binafsi Kitwanga sijawai kumwamini, angemuacha Mama atekeleze majukumu yake tafadhali.

Mama yuko vizuri sana, sioni matatizo ya Mama ingawa kila binadamu ana mapungufu yake.
Hawa jamaa ni wale waliokuwa na fursa awamu ya tano. Wanamuandama mama kwa visirani vyao tu lakini yuko vizuri mno.
 
Rais kwa mdomo wake

" Kun wengine mnakosea, mkiondolewa mnakimbilia kwa magodfather wenu, nao mbio hadi kwa Rais..."

Inaonekana kuna watu wako nyuma wanapush

Ndo maana kuna mambo ya ajabu ajabu yanayotokea
 
Tunahitaji taasisi imara zaidi kuliko wote
Tatizo analimited capacity of thinking so anaacha wamsaidie kufikiri... hii nchi inahitaji kichwa kilichotulia na chenye msimamo madhubuti. Sio hivi tunavyoenda watu wanamapembe mpaka aibu. Tuliojikoni kazi yetu kuchochea kuni tu.
 
Back
Top Bottom