Kiwanda cha Silaha cha Rwanda. Wapo mbali sana hawa jamaa

Kiwanda cha Silaha cha Rwanda. Wapo mbali sana hawa jamaa

Kila dalili iko wazi kuwa hakuna kitu.

Ila mnadhani likitokea jambo utafanyika muujiza.

View attachment 3340723
Ndio waziri wa ulinzi hata binocular inashikwaje hajui... Kuweka mama zetu kwenye hizi position kiushoga ni janga. Taaluma tu ya kijeshi hana sidhani hata kama alipitia mafunzi ya awali alipoingia kwenye uwaziriwa ulinzi. Ndio utegemee kuona matokeo chanya!! Eeeh Mungu shuka
 
Hiyo kampuni ya Rwanda ina ubia na kampuni ya silaha ya Israel, hivyo ubora kwa silaha hauepukiki.
Waisraeli watoa ujuzi na maarifa na vijana wa Rwanda wajidhihirisha ujuzi na maarifa yao kutoa kifaa cha maana.

Nchi 16 zimehudhuria maonyesho hayo na wageni walikuwa ni wa aina mbalibali wajuzi wa masuala ya usalama, wasomi, wataalam na wageni waalikwa wengine.

Rwanda imelipia gharama zote na leo ni mwisho na wageni watapelekwa kutembelea makumbusho ya mauaji ya Kimbari kabla ya kurudi makwao.

Jana mada zilikuwa ni za kusisimua pale maofisa wa kijeshi kutoka kwenye nchi hizi walipokuwa wakijadili mada iitwayo - Precision Strikes in The Digital Age: Reimagining Offensive and Defensive Capabilities

Kisha ikaja mada ingine iitwayo "Kampuni za jeshi la mamluki na Vituo vya Kijeshi barani Afrika na athari zake kwa Usalama wa nchi za Afrika" . Hii mada ilichangiwa na Jenerali Muhoozi, Luteni jenerali Daniel Sidiki Traore, Murithi Mutiga na mchangiaji mwingine kwa jina la Kagoro.

Kulikuwa na mada zingine kalikali kama mada ihusuyo kulinda miundombinu dhidi ya mashambulizi ya kimtandao na zingine.

Sidhani kama Tanzania ilituma mwakilishi yoyote
 
Hiyo kampuni ya Rwanda ina ubia na kampuni ya silaha ya Israel, hivyo ubora kwa silaha hauepukiki.
Hata Uganda kampuni yao ya silaha ina ubia na kampuni ya UAE ambao sisi tumeingia nao ubia wa kufukuza Wamasai pale Ngorongoro.

Kenya wanataka ubia na South Africa kuunda armoured vehicles. Kwa vitu ambavyo hatujui ni vyema kuingia ubia, na miradi ya silaha iko hivyo unanunua units kadhaa nyingine unataka ziwe assembled kwako au unafanya tech transfer. Inafanyika sana kwa nchi serious.
 
Tatizo lako ni chuki bimafsi na uongo,hivi unajua kuwa majeshi ya Tanzania yanatengeneza vitu na bidhaa nyingi sana? Kabla hujatoa lawama tujifunze kufanya utafiti kwanza

Chuki iko wapi mkuu .
Tangu mzalendo Magufuli afariki umeona mradi gani mkubwa umefanywa na Jeshi la wananchi au Magereza.?

Mnafikiri kazi ya Jeshi ni kufanya usafi na kupambana na Wananchi Ili CCM ishinde ?
Mnafifisha ubunifu halafu aliambiwa mnasema ni chuki .
Nyie ndio mnaichukia hii nchi ndio maana anauza bandari ili magaidi wenu waingie kirahisi .

Unajua kitu kilichosababisha Muungano ilikua ni ulinzi wa lango la bajari na sio Ushindi wa CCM kupata kura za kiitikadi na uchawa kwa pesa za Waarabu?

Je,Kiwanda cha Nyumbu kinazalisha Magari ?
Karne hii tulitegemea tuwe tunazalisha magari sio kuagiza Magari ya kizamani kabisa toka India ambayo tungeweza kutengeneza wenyewe ?
Hapo ishi ni 10% upitia manunuzi ?

Je, uniform mnatengeza wapi ?
Mpaka kushona ?
Buti zinatoka wapi ?
Kofia zinatoka wapi ?
Hivyo vitu vidogo kanisa vinanunuliwa nje hiyo unavyosema ni vipi vinatengenezwa humu nchini ?

Unajua JKT ilianzishwa kwa malengo gani ?
Mashamba wanayo tangu uhuru mpaka leo na nguvu kazi ipo ya Bure kwa nini bei ya chakula nchini inakua juu ?
Kwa ni ni hakuna viwanda vya kusindika vyakula mpaka sasa ?Mnalinda uchumi wa taifa au wa watu watano walioshika mfuko wa serikali mikononi mwao ?

Uzalendo unajengwa hautokani na kujenga taifa lenye mgawanyiko wa kidini na kisiasa.
Leo hii kuna Makada wa CCM ndani ya majeshi wanawaaminisha askari wao kuwa adui wa nchi ni wapinzani wakati wapinzani ni watanzania kama walivyo CCM . Hapo huoni kuwa mnaligawa Taifa kiusalama pia . Leo tukivamiwa na Oman hamuoni kuwa kuna watu wanawaona kama ndio miungu wao ?
Au tukivamiwa na Kenya au Rwanda hamuoni hakuna tena ule moyo kabla ya silaha na kundi kubwa haliwezi kusimama kupigania taifa maana kuna wanaowaza maisha yao na kuna wanaowaza kupigania taifa na wanaowaza kulindwa wao waishi na wengine wafe kwa gharama za wengine wakati wanaonufaika ni wachache ?
Kwa hali hiyo unategemea kuna umoja kwenye siasa za kuwaona wanaokosoa kama adui wakati wanaokosolewa ndio wanaligawa taifa kwa misingi ya kujiwekea kinga wao dhidi ya wengine katika nchi moja ?
 
Tanzania haina majeshi nane bali moja tu ambalo ni jeshi la Ulinzi.
Jeshi la wananchi ,
Jeshi la kujenga Taifa ,
Jeshi la Polisi ,
Jeshi la magereza,
Jeshi la Uhamiaji
Jeshi la Zimamoto na uokoaji ,
Jeshi la wanyama pori (Jeshi usu )
Jeshi la akiba la mgambo .
na Usalama wa Taifa .

Bado Kule Zanzibar kuna :
Jeshi la Kujenga uchumi .
na Vikosi maalumu

Yote yanaitwa Jeshi ,Jeshi ,Jeshi Ndivyo yanayoitwa sio mimi nimeyaona leo .
Na Yamewekwa hivyo kwa makusudi ya kulinda usalama wa nchi ndani na nje ya mipaka. Hii nchi ina rasilimali nyingi sana kuliko nchi nyingi sana duniani kwa hiyo Mwalimu aliona mbali sana kuweka majeshi mengi kulinda mipaka yetu na rasilimali zetu na watu wetu . Leo yamegeuzwa kuwa ni majeshi ya kulinda watu wachache na kwa ajili ya Maslahi yao na madaraka yao .
 
Wabongo kwa unafki mpo vizuri basi hapa tena kashfa kama zote. Maisha sio mashindano sio lazima nchi zote tutengeneze silaha.
 
Rais Paul Kagame akitembelea kituo cha Shirika la Uhandisi na Uzalishaji la Rwanda (REMCO) wakati wa maonyesho katika Kongamano la Kimataifa la Usalama la Afrika (ISCA), lililoanza Jumatatu, Mei 19 mjini Kigali.

Rwanda yaanza kuonyesha silaha zilizotengenezwa na kampuni ya ndani ya REMCO katika hatua ya kujenga sekta ya ulinzi ya nchi hiyo.

View attachment 3340185
Wanatengeneza au wana assemble? Kama wanatengeneza zinaitwaje? Amahoro?
 
Waacheni na viwanda vya silaha wawekeze kwenye viwanda vya bidhaa za matumizi ya amani​
 
Rais Paul Kagame akitembelea kituo cha Shirika la Uhandisi na Uzalishaji la Rwanda (REMCO) wakati wa maonyesho katika Kongamano la Kimataifa la Usalama la Afrika (ISCA), lililoanza Jumatatu, Mei 19 mjini Kigali.

Rwanda yaanza kuonyesha silaha zilizotengenezwa na kampuni ya ndani ya REMCO katika hatua ya kujenga sekta ya ulinzi ya nchi hiyo.

View attachment 3340185
Badala wawekeze kwenye vitu vya maana, wao ni vita tena ya kumalizana wao kwa wao. Akili au matope? Heri wangeanzisha kiwanda cha majembe au kalamu kuliko silaha.
 
Tanzania ni noma tuko vizuri, mambo yetu huwa tunafanya siri hatupendi kujitangazatangaza.

Raia msione mna Amani, kuna watu hawalali.

Hahahaha
 
Bila shaka utakuwa unakizungumzia kile cha Mzinga Morogoro.

Swali je silaha zao wanazotengeneza ni za kisasa au wanatengeneza magobore tu?
Ukifika pale watakuonesha kama ni za kisasa au gobore
 
Back
Top Bottom